Kataa unafiki wa SMS za Mwisho wa Mwaka: Kataa Drama za Dakika za Mwisho

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Bado masaa machache tu kuaga mwaka wa 2025 na kuukaribisha mwaka 2026, wakuu ndipo simu zinapoanza kulia kwa fujo. Ghafla, watu waliokuwa kimya na jeuri kwa siku 364 na zaidi wanakumbuka uwepo wako.
1766686624132.jpg

Unakutana na liujumbe refu: “Kama nimekukosea nisamehe,” “tusameheane kabla ya mwaka kuisha,” “maisha ni mafupi ndugu yangu mpendwa, mwaka 2026 ukawe baraka kwako na familia yako, tuendelee kupendana.” Ajabu ni kwamba Krismasi ilipita kimya, Pasaka ilipita kimya, hata kuugua kwako hawakujua wala kujali unaendeleaje—lakini tarehe 31 Desemba wanakuwa watakatifu wa ghafla.
images - 2025-12-30T135355.570.jpeg

Hii si toba, ni maigizo. Ni unafiki unaovaa koti la unyenyekevu. Ni watu wachache wanaojitengeneza kuwa wahanga wa kutowasiliana, ilhali wao wenyewe walichagua kunyamaza kwa mwaka mzima. Wengine hata namba zao ulikwishazifuta, lakini wanatuma sms ndefu kama thread kana kwamba walikuwa karibu nawe kila siku.
images - 2025-12-30T135556.029.jpeg

Leo langu wala kukataa msamaha—la hasha, msamahani jambo la msingi. Lakini ninakosoa msamaha wa dakika za mwisho unaotumwa kwa wingi, bila dhamira ya kubadili tabia. Mwaka huu 2025 unapofunga pazia, acha unyonge. Ingia mwaka 2026 kibabe sio kinyonge.
2026_Tech_Predictions_Whats_Coming_Whats_Changing_Whats_Next.jpg

Kataa SMS za kinafiki au kutoka kwa watu ambao wanakuletea unafiki. Usikubali kulazimishwa kusamehe ili watu wajisikie vizuri na kuingia 2026 bila mzigo wa dhamira. Msamaha wa kweli huanza na kuwasiliana, sio sms nyingi tarehe 31 Disemba.
 
Bado masaa machache tu kuaga mwaka wa 2025 na kuukaribisha mwaka 2026, wakuu ndipo simu zinapoanza kulia kwa fujo. Ghafla, watu waliokuwa kimya na jeuri kwa siku 364 na zaidi wanakumbuka uwepo wako.
View attachment 3522697
Unakutana na liujumbe refu: “Kama nimekukosea nisamehe,” “tusameheane kabla ya mwaka kuisha,” “maisha ni mafupi ndugu yangu mpendwa, mwaka 2026 ukawe baraka kwako na familia yako, tuendelee kupendana.” Ajabu ni kwamba Krismasi ilipita kimya, Pasaka ilipita kimya, hata kuugua kwako hawakujua wala kujali unaendeleaje—lakini tarehe 31 Desemba wanakuwa watakatifu wa ghafla.
View attachment 3522694
Hii si toba, ni maigizo. Ni unafiki unaovaa koti la unyenyekevu. Ni watu wachache wanaojitengeneza kuwa wahanga wa kutowasiliana, ilhali wao wenyewe walichagua kunyamaza kwa mwaka mzima. Wengine hata namba zao ulikwishazifuta, lakini wanatuma sms ndefu kama thread kana kwamba walikuwa karibu nawe kila siku.
View attachment 3522695
Leo langu wala kukataa msamaha—la hasha, msamahani jambo la msingi. Lakini ninakosoa msamaha wa dakika za mwisho unaotumwa kwa wingi, bila dhamira ya kubadili tabia. Mwaka huu 2025 unapofunga pazia, acha unyonge. Ingia mwaka 2026 kibabe sio kinyonge.
View attachment 3522696
Kataa SMS za kinafiki au kutoka kwa watu ambao wanakuletea unafiki. Usikubali kulazimishwa kusamehe ili watu wajisikie vizuri na kuingia 2026 bila mzigo wa dhamira. Msamaha wa kweli huanza na kuwasiliana, sio sms nyingi tarehe 31 Disemba.
Umenena vyema... Kama mtu ulichagua kuwa kimya throughout The uear basi ni vyema uka maintain ukimya hivyohivyo
 
, don't entertain negativity Nigger

People are too busy (Occupied) Kama anakutumia SMS hata mara moja don't take it for granted.
Kabsa Mkuu! Kesho watu wataanza kupokea sms unashindwa kuelewa mbona mwaka mzma walikuwa kimya
 
Sijui Kama umeelewa

Nimemaanisha it is okay kama kaamua kukumbuka ni jambo zuri

Maisha ya sasa yanatufanya Kuwait very busy in making money and life up

Kwahiyo usitegemee kutumia sms every time with no reasons.
 
, don't entertain negativity Nigger

People are too busy (Occupied) Kama anakutumia SMS hata mara moja don't take it for granted.
Hizi nasaha zako za kisoro inabidi mshauriane na Abdul huko mkiwa faraghani.
 
Back
Top Bottom