Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,112
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewatoa hofu Watanzania kuhusiana na kuwepo kwa makontena yenye makinikia ambayo yameonekana yakisafirishwa kwenda nje ya nchi kuwa makontena hayo yanasafirishwa kihalali.
Waziri Mkuu amesema hayo bungeni Mkoani Dodoma wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu kitendo ambacho hufanyika kila siku ya alhamisi iwapo waziri mkuu anakuwepo bungeni.
Amesema makontena hayo yanasafirishwa chini ya utaratibu maalum ambao umewekwa na Serikali kupitia kampuni ya umma ya madini ya Twiga kwa kushirikiana na wachimbaji wakubwa wa madini.
Waziri Mkuu amesema kinachofanywa sasa na serikali kwa kilichopo ndani ya makontena hayo kukaguliwa na kupimwa kisha serikali kulipwa inachotakiwa kupata na baada ya hapo wahusika wa makontena hayo yenye makinikia kupewa nyaraka za kuwadhibitisha ambazo hutakiwa kuzionyesha mara zinapohitajika.
Mwaka 2017 hadi mwaka 2018 Serikali tume maalum ya kuchunguza jinsi ambavyo Tanzania inavyonufaika au la na Sekta ya madini ambapo ilibainika uwa sekta hiyo imegubikwa na udanganyifu.