Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema katika mwaka wa masomo 2023/2024 Serikali imetenga Tsh. bilioni 48 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa Wanafunzi wa ngazi ya stashahada.
Amesema hayo leo Jumanne, Januari 16, 2024 wakati wa ufunguzi wa Chuo Kikuu Katoliki Mbeya (CUoM) Mkoani Mbeya ambapo amesema kuwa mpango huo ambao ni maono na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan unalenga kuhakikisha elimu inayotolewa inakuwa bora na kuwezesha Wahitimu wa Vyuo nchini kujiamini na kumudu ushindani wa kitaifa na kimataifa.
“Lengo jingine la Rais Dkt. Samia ni kuona Vijana wengi wanapata elimu itakayowapa ujuzi na uwezo wa kushiriki katika ujenzi wa Taifa” PM Majaliwa amesema kuwa Serikali imetenga Dola za Kimarekani milioni moja kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) ambazo zinasomesha Wahadhiri 27 kutoka Vyuo Vikuu visivyo vya Serikali.