Kassim Majaliwa: Makontena ya Makinikia yanayosafirishwa nje ya nchi ni halali

PM anaingizwa chaka baya bila kujua. Ameulizwa general question, na alipaswa kama mtendaji mkuu wa serikali, kupress for more specific details, na wala siyo kuhangaika haraka kuwasilisha maelezo mengi kwa lengo tu la kuwapooza Watanzania...
Hayo ndiyo majibu na msimamo rasmi wa serikali. Ulitaka a press ili aje na majibu gani tofauti.
 
Hakika mkuu P, maana tuliambiwa mchanga hautatoka(kuuzwa) hadi ijengwe "smelter" hapahapa.. hiyo kitu imeshajengwa?

Tumepigwa..nakazia
mpaka mzee anaondoka smelter haijajengwa.
hiyo kitu imeishia wapi?
 
Siasa za nchi hii zinaweza kuwa chanzo kikuu cha kuenea kwa kasi magonjwa yasiyoambukiza..........
 
Nimedokezwa ukweli huu mchungu hadi nikatamani kuzimia:

1. Makontena yameanza kusafirishwa nje ya nchi tangu mwendazake yuko hai.

2. Hakuna kilichobadilika kutoka mfumo uliokuwa unatumiwa na Serikali ya JK kupitia TMAA kusafirisha makinikia hayo nje. Utaratibu huo ulikuwa ni: sampuli kuchukuliwa na kupimwa, thamani ya awali ya madini husika kukokotolewa, mrabaha wa awali kulipwa, makontena kusafirishwa na kusafishwa nje ya nchi kwa vibali maalum, baada ya makinikia hayo kuchakatwa huko nje na thamani yake halisi kujulikana, kama thamani ya awali itakuwa ndogo wawekezaji wanalipa serikalini mrabaha wa mwisho na kama itakuwa chini wanarejeshewa na serikali hela iliyozidi kwenye malipo ya awali. Narudia tena, hakuna kilichobadilika.

3. Madini yanayolipiwa kodi na mrabaha bado ni yaleyale, hakuna kilichoongezeka - ni dhahabu, shaba na fedha.

Nampongeza sana mama yetu SSH kwa kupambana kufufua uchumi wetu na kukataa propaganda za kisiasa ambazo zilichangia sana kuvuruga uchumi wa nchi yetu hususan sekta ya madini. Ingekuwa dunia ya kwanza, wahusika wangeomba msamaha kwa uongo walioupiga kwa umma kuhusu wizi kwenye makinikia wakati mambo yalikuwa under control. KAZI IENDELEE.

Wanaopinga taarifa hii waje na maelezo yafuatayo:
1. Je, yale makontena yaliyozuiliwa kipindi cha mwendazake si tayari yalishapelekwa nje, tuelezwe aina ya madini yaliyopatikana baada ya kusafishwa huko nje na kama kuna utofauti na kile TMAA walichokuwa wamekikadiria kupitia sampuli zilizopimwa.
2. Je, Utaratibu wa sasa wa kusafirisha makontena hayo unaotumika hivi sasa una tofauti gani na ule wa kipindi cha nyuma.
3. Je, tumevuna kiasi gani cha fedha hivi sasa kupitia makinikia na je inatofauti gani na mapato ya awali.
4. Je, sheria yetu ya kuzuia makinikia kusafirishwa nje tumeifuta au bado ipo. Kama ipo yanasafirishwa nje kwa sheria ipi?
PROPAGANDA SAWA LAKINI TUMUOGOPE MUNGU JAMANI.
Kwa maelezo haya unataka kuthibitisha kuwa mwendazake alikuwa anadanganya na ilikuwa propaganda tu?
Pili unathibitisha kuwa aliyesema zile report zilikuwa professorial rubbish alikuwa sahihi?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom