DOKEZO Kasoro kubwa katika Ofisi ya Hazina (Kitengo cha Malipo ya Pensheni za Wastaafu)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu sana ya wastaafu walio fukuzwa jeshi, walio staafishwa kwa ugonjwa, waliofariki wakiwa kazini na waliostaafu kwa taratibu za Kawaida za Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambapo kitaratibu kundi hilo lote huwekwa kwenye kundi la wastaafu wanao subiri kulipwa viinua mgongo vyao kutoka Hazina.

Kitu cha kushangaza, yapata zaidi ya miaka miwili na miezi kadhaa watu hao hawajalipwa fedha hizo na huku taratibu zote zimekamilika. Kwa upande wa Jeshi walishatimiza Wajibu wao, kazi iliyobaki ni Hazina kuwalipa tu lakini sababu zinazotolewa na Hazina kwamba watu hao waendelee kusubiria kwa muda usiojulikana maana System za malipo za Hazina zimeelemewa kwahiyo hazifanyi kazi yapata mwezi wa Pili tangu tarehe 22 mwezi Mei 2022 mpaka leo hiii nikiandika uzi huu.

Naomba Wizara ya Fedha ije itoe ufafanuzi kuhusiana na hilii.
 
Kiumbe chenyewe ni UNKNOWN sasa sisi tufanye nini !!??

Tatizo lenu kubwa ni kuendelea kuibeba CCM iendelee kuwepo madarakani.
 
Back
Top Bottom