Serikali itamke pia nyongeza ya Kima cha chini kwa Pensheni za wastaafu

danimutta

JF-Expert Member
Nov 4, 2011
264
326
Kwa ujumla hali za wafanyakazi na wastaafu kwa kipindi cha miaka 7 iliyopita ziliathirika sana kutokana na ukosefu wa nyongeza ya malipo hayo.

Baada ya tangazo la Rais Samia kuongeza mishahara kcc kwa asilimia 23.3% ni matarajio ya wastaafu kwamba serikali nao pia itawakumbuka na kutekeleza ongezeko la pensheni kcc kwa mujibu wa The Public Services Retirement Benefits Act (Minimum Pensions).

Mara ya mwisho ongezeko la pensheni lilitekelezwa 2015 kwa agizo la Mh. Saada Mkuya Salum kutoka Tshs. 50,000/= hadi Tshs. 100,000/= hadi sasa.

Ni matarajio ya wastaafu wa Tanzania kwamba mama huyu ambaye kwa bahati nzuri ni Waziri wa fedha huko visiwani atatumia ushawishi wake katika Serikali ya CCM ili kuongeza pensheni za wastaafu kama alivyofanya 2015 kutoka chini ya dola 50 wanazolipwa kwa mwezi.
 
Back
Top Bottom