Kuna thread nyingine ukizisoma unachefukwa, kuna watu nadhani hawana upendo na nchi yako kabisa. Mapambano wanayoyafanya vyama vya upinzani yamesaidia sana kuibua kashfa nyingi na kuirudisha nchi kwenye mstari, kazi wanayoifanya ni yakizalendo sana. Chama cha mapinduzi kwa kipindi kirefu kimewaangusha watanzania na kwa kifupi watanzania wengi wamekichoka na walitaka kukimwaga 1995 na 2015 huu ni ukweli ulio wazi. Kama siyo kazi ya Kinana na Nape kuzunguka nchi nzima nadhani sasa hivi kingekua chama cha upinzani na wangekua wanauza mali zao kwakukosa kuelewana. Hivyo tueshimu vyama vya upinzani, bila wao sasa hivi tusingekua na Raisi mzalendo anaye piga vita ufisadi na uporaji wa rasilimali za nchi. Ukumbuke kwamba Raisi wetu hajipambanui na chama chake, ata kwenye kampeni zake alisema watu wamchague yeye na si chama hapo ndiyo ujue chama cha mapinduzi kiko ICU. Kwasisi watanzania wazalendo, hatuchagui chama bali mtu mwenye uwezo wa kufanya yale ambayo yatawasaidi watanzania.