Kashfa zote walizoibua CHADEMA juu ya CCM ni za kutunga

Kashfa zote walizoibua CHADEMA juu ya CCM ni za kutunga

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
40,017
Reaction score
51,157
Ni za kutunga kwa lengo la kujipatia umaarufu tu wa kisiasa ili kuonekana mbele ya jamii kama watetezi wa kweli ilhali ni mafisadi tu waliojificha kwenye ngozi za kondoo.

Chadema imekua ikiibua hoja mbali mbali zenye lengo la kuifanya ccm na wanachama wake kuonekana wachafu mbele ya jamii, lakini watu hao hao wanapovuka mpaka kwenda upande wao tuhuma zote hubadilika na kuwa sifa. Makosa Yote yaliyoainishwa juu ya wahusika hufutwa kabisa na kuonekana kama vile jambo hilo halikuwahi kutendwa na mhusika au kuwahi kutokea.

Kitendo hicho cha kufuta shutuma na kashfa juu ya wahusika pindi wanapokua upande wao, inaleta hitimisho kuwa tuhuma walizozitoa hazikuwa na ukweli wowote, na zilitolewa kwa lengo la kupotosha, kukuza umaarufu wa kisiasa wa mtoa tuhuma na kuwatishia wahusika ili wahame kambi.

Aina hii ya siasa za vitisho kwa kashfa za kutunga ni mbaya sana na inatakiwa kupingwa kwa kila namna na wapenda demokrasia wote na siasa safi zenye kuleta changamoto chanya kwenye maendeleo ya Taifa letu.
 
Na Mungu alivyomkubwa

Wana CCM wote waliokuwa wanashutumiwa kwa kashfa kubwa kubwa na Chadema wamehamia Chadema

1) Lowassa
2) Sumaye
3) Mzee Kingunge
4) Makongoro Mahanga
5) Nyalandu
6) Lawrence Masha
7.)...
 
Na Mungu alivyomkubwa

Wana CCM wote waliokuwa wanashutumiwa kwa kashfa kubwa kubwa na Chadema wamehamia Chadema

1) Lowassa
2) Sumaye
3) Mzee Kingunge
4) Makongoro Mahanga
5) Nyalandu
6) ....

Cha ajabu mtuhumiwa mwingine ndiye Rais wa nchi! Watuhumiwa wengine walipewa uwaziri, uenyekiti wa bunge n.k.

Ufisadi ni synonymy ya CCM!
 
Na Mungu alivyomkubwa

Wana CCM wote waliokuwa wanashutumiwa kwa kashfa kubwa kubwa na Chadema wamehamia Chadema

1) Lowassa
2) Sumaye
3) Mzee Kingunge
4) Makongoro Mahanga
5) Nyalandu
6) ....
Kwani hawa hapa CCM wanasemaje? Siyo mafisadi?
 
Unataka kusema kashfa zifuatazo si kweli au una maana gani Stroke?

1. Buzwagi
2. Meremeta
3. Deep Green
4. IPTL
5. NIDA
6. Richmond
7. Escrow
8. EPA
9. Madudu kwenye Halmashauri za Miji + Ripoti za mwaka za CAG.
10. Maliasili, Madini nk nk
 
Mtu yeyote akiwa mtenda dhambi huwa adui wa haki na watenda dhambi wenzie hushangilia wakati watakatifu wakimsakama ili aokoke na siku akiokoka wapenda haki watamoenda na kuwa karibu yake lakini kule alipotoka kwa watenda zambi wenzake watamuona mjinga na kumpa kashfa nyngi, ivyo sishangai kwa wana ccm kuwakejeli wote waliofanikiwa kujitoa kwenye dhambi ya kuumiza wana nchi
 
Unataka kusema kashfa zifuatazo si kweli au una maana gani Stroke?

1. Buzwagi
2. Meremeta
3. Deep Green
4. IPTL
5. NIDA
6. Richmond
7. Escrow
8. EPA
9. Madudu kwenye Halmashauri za Miji + Ripoti za mwaka za CAG.
10. Maliasili, Madini nk nk
Namba 6 na 10 majibu yake mnayo;
 
Chadema ni genge la watafta vyeo na ruzuku kwa kofia ya siasa
Wanachopigania kulinda ni majimbo yao ya uchaguzi tu at any cost, hawana plan nyingine zaidi ya hapo.
 
MASIKINI WA LEO NDIE TAJIRI WA KWESHO..
HIZI KASHFA HIZI............
 
Kuna thread nyingine ukizisoma unachefukwa, kuna watu nadhani hawana upendo na nchi yako kabisa. Mapambano wanayoyafanya vyama vya upinzani yamesaidia sana kuibua kashfa nyingi na kuirudisha nchi kwenye mstari, kazi wanayoifanya ni yakizalendo sana. Chama cha mapinduzi kwa kipindi kirefu kimewaangusha watanzania na kwa kifupi watanzania wengi wamekichoka na walitaka kukimwaga 1995 na 2015 huu ni ukweli ulio wazi. Kama siyo kazi ya Kinana na Nape kuzunguka nchi nzima nadhani sasa hivi kingekua chama cha upinzani na wangekua wanauza mali zao kwakukosa kuelewana. Hivyo tueshimu vyama vya upinzani, bila wao sasa hivi tusingekua na Raisi mzalendo anaye piga vita ufisadi na uporaji wa rasilimali za nchi. Ukumbuke kwamba Raisi wetu hajipambanui na chama chake, ata kwenye kampeni zake alisema watu wamchague yeye na si chama hapo ndiyo ujue chama cha mapinduzi kiko ICU. Kwasisi watanzania wazalendo, hatuchagui chama bali mtu mwenye uwezo wa kufanya yale ambayo yatawasaidi watanzania.
 
CCM hoja pekee waliyobaki nayo ni Chadema kupokea watu ambao waliwahi kuwatuhumu huko nyuma..

Hili ni kosa ambalo linaigharimu Chadema hadi sasa, chadema imekuwa ya kujitetea jambo lililokuwa likifanywa na CCM

CCM wanajishikilia kwenye kahoja hako tu, na imekuwa sio jambo la aibu kumuona kiongozi mkubwa akisema mafisadi yamekimbilia Chadema!
 
Cha ajabu mtuhumiwa mwingine ndiye Rais wa nchi! Watuhumiwa wengine walipewa uwaziri, uenyekiti wa bunge n.k.

Ufisadi ni synonymy ya CCM!
JPM Hakuwa kwenye list of shame na angekuwepo huenda asingekuwa Rais
 
Namba 6 na 10 majibu yake mnayo;

Mimi sina majibu - kama wewe unayo weka hapa kwa vile hili ni jukwaa huru kwa mijadala yenye tija kwa Taifa letu na watu wake.

Nakumbuka kashfa zote zikiwemo hizo mbili zililazimu Kamati za Bunge kuundwa na Ripoti husika kusomwa Bungeni. Kuna baadhi ya wanasiasa na watendaji waliwajibika/waliwajibishwa iwe kinidhamu au kisiasa lakini cha kusikitisha zaidi Serikali imeendelea kuwa na kigugumizi kutekeleza maazimio ya Bunge la JMT kwa vipindi husika, hadi leo hii tunapoandika. Shida ni nini?

Mbali na hizo 2 ulizozigusia, kuna lundo la kashfa nyingine hapo juu ambazo mpaka leo zinaendelea kulitafuna Taifa, mfano mmoja ni IPTL. Unasemaje?
 
Kuna thread nyingine ukizisoma unachefukwa, kuna watu nadhani hawana upendo na nchi yako kabasa. Mapambano wanayoyafanya vyama vya upinzani yamesaidia sana kuibua kashfa nyingi na kuirudisha nchi kwenye mstari, kazi wanayoifanya ni yakizalendo sana. Chama cha mapinduzi kwa kipindi kirefu kimewaangusha watanzania na kwa kifupi watanzania wengi wamekichoka na walitaka kukimwaga 1995 na 2015 huu ni ukweli ulio wazi. Kama siyo kazi ya Kinana na Nape kuzunguka nchi nzima nadhani sasa hivi kingekua chama cha upinzani na wangekua wanauza mali zao kwakukosa kuelewana. Hivyo tueshimu vyama vya upinzani, bila wao sasa hivi tusingekua na Raisi mzalendo anaye piga vita ufisadi na uporaji wa rasilimali za nchi. Ukumbuke kwamba Raisi wetu hajipambanui na chama chake, ata kwenye kampeni zake alisema watu wamchague yeye na si chama hapo ndiyo ujue chama cha mapinduzi kiko ICU. Kwasisi watanzania wazalendo, hatuchagui chama bali mtu mwenye uwezo wa kufanya yale ambayo yatawasaidi watanzania.
Chadema wanatumia mbinu ya kuwatisha wana ccm kwa kashfa hewa kwa ahadi za kuwasafisha pindi wanapohamia huko.
 
Kwani hawa hapa CCM wanasemaje? Siyo mafisadi?

Chadema ndio waliotuhumu kina Nyalandu na Lowassa halafu wao ndio wanasema sasa kuwa walisingiziwa zile tuhuma,

Kwanini nisiamini Jamaa ni wasingiziaji Kama wenyewe wamekiri?
 
Kweli watu wote wakiwa mambumbumbu kama wewe nchi itakuwa na mazezeta mengi sana, umepoteza muda mwingi kuandika upuuzi mtupu!!! Mtu yeyote akiwa mtenda zambi huwa adui wa haki na watenda dhambi wenzie hushangilia wakati watakatifu wakimsakama ili aokoke na siku akiokoka wapenda haki watamoenda na kuwa karibu yake lakini kule alipotoka kwa watenda zambi wenzake watamuona mjinga na kumpa kashfa nyngi, ivyo sishangai kwa wana ccm kuwakejeli wote waliofanikiwa kujitoa kwenye dhambi ya kuumiza wana nchi
Lowassa kaokoka?Tufanye wote walioenda chadema wameokoka,mtu akiokoka huwa mstari wa mbele kukemea dhambi. Ni lini lowasa au sumaye alikemea ufisadi?

Mtu akiokoka kanisa aliachi kukemea dhambi,mbona chadema toka Lowassa alivoingia huko Ile agenda yao ya kupambana na ufisadi wameizima? Au fisadi alikua lowasa tu na sasa huku wameisha?
 
Back
Top Bottom