Kashfa ya Ufisadi Bandari ya Dar

Kashfa ya Ufisadi Bandari ya Dar

Huo ni ufisadi na hakuna mushkeli. TRA na wafanyakazi wake, kama sikosei asilimia 99 pia wamo kwenye mfumo huo huo. Utakuta mtu katoa jasho na kutuma kimzigo chake, basi atasumbuliwa awape rushwa utafikiri bandari ni mali yao binafsi! Kila mmoja wao anajali mfuko na tumbo lake na hawatazami kuwa wapo pale kwa niaba ya serikali, nchi na wananchi! Ukiangalia huko juu zaidi ndiyo unachoka kwani japo tatizo linajulikana, wahusika hawaguswi kwani ni WANAMTANDAO!! Sijui tutaishia wapi...........
 
Kikwete awamulika wabadhirifu TISCAN

Maulid Ahmed
Daily News; Monday,March 02, 2009 @18:25

Rais Jakaya Kikwete amesema ana orodha ya majina ya wafanyakazi wa kampuni ya ukaguzi na ukadiriaji wa mizigo ya TISCAN, wanaoshirikiana na wafanyabiashara kukwepa mizigo yao kukaguliwa na kuamuru wafanyakazi hao wafukuzwe kazi mara atakapokabidhi majina hayo.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo leo alipofanya ziara ya ghafla katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), ambapo alisema orodha hiyo anaifanyia kazi. “Majina hayo sasa nayafanyia kazi, waambie watu wa Maktaba (makao makuu ya kampuni hiyo) mtindo wanaofanya unajulikana, sitawaumbua hadharani, majina yao nitawapa wakubwa zao na nikiwapa tu watoeni kwenye kazi,” alisema.

Rais Kikwete alisema wafanyakazi hao wamekuwa na tabia ya kushirikiana na wafanyabiashara na kuwapa mbinu za kufanya, ili mizigo yao inayoingia nchini, isiweze kupitishwa kwenye mashine ya ukaguzi inayotumia mionzi, hivyo kutozwa kodi ndogo.

“Tiscan pale maktaba kwa kutumia simu, mfanyakazi anamfundisha mtu aliyepo Dubai (Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE) namna ya kujaza fomu na kontena lake linapoingia nchini, lionekane amebeba mtumba asipitishwe kwenye skana kumbe ndani kuna VX… nikiwa Ikulu naelezwa kila kitu, hii ndiyo Bongoland, nasi tuongeze bongo, wao wanatajirika tu, watoeni kwenye kazi,” alisema.

Mbali na hilo, Rais Kikwete aliagiza TPA kununua eneo la Kampuni ya Wakala wa Meli (NASACO) lililopo ndani ya eneo la bandari hiyo kwa ajili ya kuhifadhi kontena. Eneo hilo la Nasaco, lipo chini ya mufilisi kutokana na kesi inayoendelea mahakamani, iliyosababishwa na deni la mamilioni ya shilingi ambayo kampuni hiyo inadaiwa na watu mbalimbali, hali ambayo Rais Kikwete aliitaka TPA kuwaomba kuzungumza nao nje ya mahakama na kuwalipa deni hilo, ili waweze kulimiliki wao.

Rais Kikwete aliihimiza mamlaka hiyo kufanya kazi kwa lengo la kuleta ufanisi na kuwaeleza kuwa wakati wowote atafanya ziara ya kushitukiza kabla ya mwisho wa mwezi ujao, kuona kama wameongeza ufanisi kama walivyoahidi. Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Ephraim Mgawe, alisema tangu Januari 26 hadi juzi, idadi ya meli zilizokwishapakua mizigo zimepungua kutoka 23 hadi 16.

Akifafanua, alisema meli za kontena zilikuwa 12 sasa 14, meli za mafuta kutoka nne hadi mbili na meli zilizokuwa na mizigo kiujumla kutoka saba na hadi juzi kulikuwa hakuna hata moja. Mgawe alisema muda wa meli kusubiri nje kupakuliwa umepungua kutoka wastani wa siku tisa hadi sita ambapo lengo ni kufikia wastani wa kati ya siku mbili na siku moja ifikapo mwezi ujao.

Alisema chombo cha kupakulia mizigo cha kampuni ya kupakia na kupakua kontena (TICTS) kilichoharibika kwa kipindi cha mwaka mmoja, kilianza kufanya kazi juzi na kuongeza, “tumepata vyombo vipya vya kupakulia kontena vinne, tutawakodisha Ticts viwili kwa lazima, hivyo vyombo vya kupakulia vitakuwa tisa”.

Alisema kati ya Januari 26 hadi juzi, idadi ya kontena zilizopo bandarini imepungua kutoka 10,500 hadi 7,796. Kwa siku kontena 200 hadi 300 hupakuliwa na Ticts wakati zinazoingia ni 1,000 kwa siku. Rais Kikwete aliwataka kuhakikisha kontena zinapakuliwa ndani ya siku saba na zisikae muda mrefu bandarini, ambapo wenye kontena wamegeuza eneo la bandari kama sehemu ya kuhifadhi mizigo yao.

Hivi katika nchi inayoongozwa kwa utawala wa sheria na katiba- Raisi ana mamlaka ya kuamuru mtu atemwe kwenye kibarua chake? tena katika taasisi isiyokuwa ya serekali?
 
Game theory ukitoa chochote wataenda baharini na meli ndogo na kutafuta container lako hata siku mbili nzima watalileta alafu watakuita utalichukua. Wakati wanafanya hivyo hawata fanya kazi nyingine yeyote ndo sabababu mlolongo unakuwa mwingi. Honga utapata unachotaka. Wafanyabiashara wakubwa hawalalamiki kwani meli zao zinaingilia VIP. Amkeni watanzania TPA ni hadithi kubwa ya alfu ulela ulela.
 
Suggestion yangu ni kuwa mindhali KIMEI wa CRDB au jule bosi wa TRA wanafanya kazi nzuri tuuu kwa nini JK asimuapoint mmojawao kwenda kuisort out THA? maana Mgawe na GENGE lake la MAFISANI naona wameshindwa kazi na evidence wee pila SALENDA bridge utaona meli zilivyo jazana kule baharini

GT HII Imetulia kweli... ila one tiny-winy problem...HIVI HAWA NI KABILA GANI TENA VILE??( maana kuna wakabila wa JF wanaoshadidia kushutumu bila kujali performance ya individuals! kazini kwenu!)
 
Tanzania ni kama sahani yenye vinono. Kila mwenye mkono na mdomo anaweza kunyoosha huo mkono kama anaifikia sahani kisha anaweka mdomoni mwake. Wao wanasema kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake.
 
Rushwa ni tatizo kubwa..linafanana na kansa inayotutafuna taratibu. Tuichukie rushwa la sivyo mambo yataenda kombo. Hata boarders, especially Sirari na Horohoro, TRA wamekuwa wanaendekeza sana rushwa kama ilivyokuwa Horiri, Moshi.
 
Thank you Game Theory.

Thank you for a mind wide open enough to correct the besmirching words on the record of Samson Luhigo.

Kama kuna fisadi huko unamjua mlete hapa tumuanike, lakini I assure you GT, Samson Luhigo alikuwa anaogopa rushwa kama ukoma yule mzee. Alikuwa hataki hata kukubali vi appointment appointment na wahindi wahindi mafisadi ambao walikuwa wanamtafuta kiiila wakati.

Jambo moja ambalo namshukuru Athumani Janguo, despite all the allegations of malfeasance that clouded his tenure at Harbors (ambazo sina uhakika nazo zaidi ya utajiri wa familia yake ulioonekana kwa nje ) ninachomshukuru ni kumpendekeza Samson Luhigo kwa Mwinyi wakati anastaafu Bandari. Yule mtu mwingine ambae originally alikuwa groomed to succeed Janguo, the former Chief Financial Officer, appointment track yake ili falter amidst embezzlement allegations when he was the Kaimu Mkurugenzi Mkuu, so then Mwinyi went into a tizzy trying to fill the post. Ndio Janguo akampendekeza Luhigo. Namshukuru Janguo kwa sababu aliangalia merit, at that time ilionekana hakukuwa na mtu anaeijua Harbors na mchapa kazi kama Luhigo. I mean Janguo angeweza kupendekeza swahiba, you know. Na Mwinyi pia, kwa pale alionyesha tremendous leadership, unajua Tanzania huwa hatufati meritorious system.

Trust me, Samson Luhigo's integrity is unimpeachable and unblemished, and has never being questioned.

Thank you again, Game Theory, for being accountable and honorable.

Kuhani. Huyu Mzee Luhigo yuko karibu nawe? I hope this does not cloud your judgement. I am not doubting his integrity but kama kuna kitu hii nchi yetu imetufundisha ni kuwa still waters run deep! I hope and pray that he does not turn out to be another Idris.

Amandla........
 
Mwingine ni Mwanakijiji na stori yake ya uongo kuwa, "JF yafungiwa UDSM!" Hili lilibainika kabla hata ya jua kuzama siku ile kuwa ni famba, fabricated news, u-Rush Limbaugh flani hivi....lakini the one and the only JF Guru hakuomba radhi na kale ka-thread kakafungwa na Mods kuokoa jahazi........

.

Mkubwa huko UDSM kuna baadhi ya IP zilikuwa blocked ,hivyo watu walishindwa ku-access JF wakawa wanafikiri JF imefungiwa
 
Jamani nilianzishas thread niliyowataja mafisadi wa TPA lakini nashangaa siioni...sasa baada ya kimya kirefu i expected kuwa bado tutakuwa tunaendelea kumaintain standards sasa swali langu kama imebadilishwa mbona hatuambiani wakulu? na kama mmeihamisha je mnaweza kutufahamisha iko wapi?

maana naona kuna threads zaidi ya 3 zinazohusu THA lakini naona hatuna mtiririko mzuri na bila kusahau kuwa ile header ya MAFISADI bandari DAR na majina yao ilikaa vizuri zaidi

kulikoni au ndio mmekaliwa kooni na mafisadi?
 
Bado mwendelezo wa malalamiko unaendelea kwa Malmaka yetu ya Bandari hapa Dar. Hivi karibuni Mheshimiwa Rais alikemea kitengo cha Maktaba kwa kupitisha mizigo kinyemela bila kupitia mashine ya mionzi na hivyo kutolipa ushuru
unaostahili na kulikosesha taifa mamilioni ya fedha. Lakini tatizo si hapo tu bali na kwenye kitengo cha uajiri kimeoza kwani kama si hongo au kujuana hupati ajira Bandari. Naongea hivyo kwa confidence kuwa nawafahamu vijana zaidi ya watatu waliomaliza form six na kusomea diploma Chuo cha Bandari wanahangaika kila siku kutafuta ajira Mamlaka ya Bandari bila mafanikio; kinachokatisha tamaa nawaona vijana wasiokuwa na qualification wanapata ajira hapo hapo Bandari japokuwa wana elimu ndogo; mmoja kwa hanari za mtaani anadai kanunua hiyo ajira kwa Mil. 3. Hivi majuzi kuna vijana wamefanya interview wapatao 80, na ilielezwa kuwa 40 kati yao watapata ajira lakini habari za ndani zinasema kuwa wala hongo na rushwa na mambo ya kujuana yameshatawala hivyo si ajabu wakawapa ajira ndugu zao na walionunua hizo ajira. Naomba swala hili lifuatiliwa na wenye habari zaidi watupashe; maendeleo na mabadiliko yataletwa na sisi wenyewe!
 
jamani naomba mpiganaji moja, ambaye ana active network na watu wa bandari afuatilie swala hili pale Bandari,kufahamu ni nini kinaendelea hususan masuala ya ajira,halafu atupe data kamili.

nasikia uchungu sana kwa sababu ni juzi juzi tu walitangaza kazi nyingi sana na mimi niliomba lakini mpaka leo kimya kabisa, miezi kama miwili imepita,isije kuwa ni hako kamchezo kao hako ka kifisadi.
 
sasa mtu kama mimi mzalendo tu na simjui mtu ntafanyaje nami nipate kazi???

Swali lako zuri na ndio maana nimeweka hapa thread hii tusaidiwe na wahusika, haya mambo yanasikitisha kwa kweli; wanapachikana wenyewe kwa wenyewe na wenye sifa wanapigwa chini.
 
Mzee umesahahua sekta zote zenye harufu ya ulaji ni mahsusi kwa watoto wa wanene. Angalia memo zitakapotembea kwenye ajira za Mambo ya nje kwa hizi ajira zilizotangazwa. Watakaoajiriwa ni watoto wa wakulu. Ndo maana tunaishia kusema 'majina ninayo' muwafukuze kazi!
 
Tafadhalini rudisheni hii kwenye siasa

tunataka kujadili ufisadi humu
 
Kitu kingine kinachoboa wakulu ni registration. Kuna thread niliinzisha humu sikupata response. My take ikawa ni kwamba hakuna aliyekutana na hii dhahama iliyonikumba mimi. Hawa wajinga wa TRA wanaboa sana. Kuna gari tumeleta miezi mitatu hatujapata registration card kila siku stories mara wakosee mara wapoteze ili mradi ni kichefuchefu. Sijuwi kama hatuwezi hata kusajiri magari ni kipi tunachoweza? Na hiyo miezi mitatu gari kufanya kazi nani analipa hiyo gharama? Gari hiyo hiyo ingekuwa ndani haiajlipiwa kodo storage charge yake ingekuwa kiama. Jamani TRA mnatukwaza sana sana.
 
Kuna mawili.

1. Clearing agent wako hajui kazi.

2. Au Umeingilia kazi za watu kwa fuatilia usajili mwenyewe

Kuna watu kazi zao ni hizo tu wanakusajilia gari 2-3 days unaondoka na Kadi yako genuine mkononi.
 
Wednesday August 12, 2009
Local News

TICTS sued for 116.9m/- for container disappearance

FAUSTINE KAPAMA, 11th August 2009 @ 01:15, Total Comments: 0, Hits: 306

A BUSINESSMAN from the Democratic Republic of Congo (DRC) and a local clearing and forward agent have sued the Tanzania International Container Terminal Services (TICTS) Limited, demanding refund of 116,779 US dollars for mysterious disappearance of their container imported from China.

The businessman, Mr Ngoike Mubanzo, and Dar es Salaam based Triple D Limited filed the suit at the High Court’s Commercial Division and the matter was mentioned before Judge Robert Makaramba yesterday and has been set for disposal of an objection raised by TICTS.

In the objection, TICTS, through its advocate Dilip Kesaria, are asking the court to reject the said commercial dispute on grounds that the plaint does not disclose a cause of action by the clearing and forwarding agent company against them and it has not been signed by the businessman.

The parties, however, agreed to disposal of the objection by addressing the court through written submissions. The trial judge ordered Mr Kesaria to file his submissions on August 24, while Advocate Carol Tarimo, for the plaintiffs, would file his reply submissions on September 4.

Mr Kesaria would file any rejoinder on September 10 and the court would deliver its ruling on the matter on September 30. In the case, the plaintiffs are also seeking payments of general damages and loss of profit to be assessed by court for negligence by TICTS in the disappearance of the container.

In October last year, the businessman was shipping a container number MAEU 6109085 B/L number 582854447 from Hong Kong, which contained 288 bales of poplin and the same was to be discharged at Dar es Salaam Port by a carrier vessel MAERSK KITHIRA on transit to Lubumbashi in DRC.

The said container arrived at the port on January 6, this year and the next day was discharged from the ship and stocked for custody in TICTS’s terminal yard, waiting for clearing formalities. Triple D Limited, being clearing agent of the businessman, surrendered all documents to the ship’s agent.

It is alleged that delivery order was issued on January 9, this year and after completion of all formalities, including loading procedures, Triple D Limited had to load the container on January 16, this year, for transportation to its destination to Lubumbashi, but the container could not be traced at the yard.

Officials from TICTS informed the clearing agent that the disappearance of the container was reported to the police for investigations. Such disappearance, the plaintiffs allege, was out of untold negligence by TICTS, who ought to have handled the container with due care.

They allege that the act by TICTS of not taking proper care of the said container which resulted into being lost has caused great financial loss and embarrassment to them considering that the businessman was depending on the said container to boost his business, but he has found himself in financial difficulties.

In the written statement of defence, TICTS admits the disappearance of the container, but denies any liability and that the plaintiffs are not entitled to the amount and relief claimed at all. Therefore, TICTS prays to the court to dismiss the commercial dispute in its entirety with costs.

Furthermore, TICTS states that their decision to inform the plaintiffs on the disappearance of the container and advising them to be patient while the incidence was being investigated by the police was not and could not be construed as admission of liability and negligence in mishandling the container.
 
Wednesday August 12, 2009
Local News

TICTS sued for 116.9m/- for container disappearance

FAUSTINE KAPAMA, 11th August 2009 @ 01:15, Total Comments: 0, Hits: 306

A BUSINESSMAN from the Democratic Republic of Congo (DRC) and a local clearing and forward agent have sued the Tanzania International Container Terminal Services (TICTS) Limited, demanding refund of 116,779 US dollars for mysterious disappearance of their container imported from China.

The businessman, Mr Ngoike Mubanzo, and Dar es Salaam based Triple D Limited filed the suit at the High Court's Commercial Division and the matter was mentioned before Judge Robert Makaramba yesterday and has been set for disposal of an objection raised by TICTS.

In the objection, TICTS, through its advocate Dilip Kesaria, are asking the court to reject the said commercial dispute on grounds that the plaint does not disclose a cause of action by the clearing and forwarding agent company against them and it has not been signed by the businessman.

The parties, however, agreed to disposal of the objection by addressing the court through written submissions. The trial judge ordered Mr Kesaria to file his submissions on August 24, while Advocate Carol Tarimo, for the plaintiffs, would file his reply submissions on September 4.

Mr Kesaria would file any rejoinder on September 10 and the court would deliver its ruling on the matter on September 30. In the case, the plaintiffs are also seeking payments of general damages and loss of profit to be assessed by court for negligence by TICTS in the disappearance of the container.

In October last year, the businessman was shipping a container number MAEU 6109085 B/L number 582854447 from Hong Kong, which contained 288 bales of poplin and the same was to be discharged at Dar es Salaam Port by a carrier vessel MAERSK KITHIRA on transit to Lubumbashi in DRC.

The said container arrived at the port on January 6, this year and the next day was discharged from the ship and stocked for custody in TICTS's terminal yard, waiting for clearing formalities. Triple D Limited, being clearing agent of the businessman, surrendered all documents to the ship's agent.

It is alleged that delivery order was issued on January 9, this year and after completion of all formalities, including loading procedures, Triple D Limited had to load the container on January 16, this year, for transportation to its destination to Lubumbashi, but the container could not be traced at the yard.

Officials from TICTS informed the clearing agent that the disappearance of the container was reported to the police for investigations. Such disappearance, the plaintiffs allege, was out of untold negligence by TICTS, who ought to have handled the container with due care.

They allege that the act by TICTS of not taking proper care of the said container which resulted into being lost has caused great financial loss and embarrassment to them considering that the businessman was depending on the said container to boost his business, but he has found himself in financial difficulties.

In the written statement of defence, TICTS admits the disappearance of the container, but denies any liability and that the plaintiffs are not entitled to the amount and relief claimed at all. Therefore, TICTS prays to the court to dismiss the commercial dispute in its entirety with costs.

Furthermore, TICTS states that their decision to inform the plaintiffs on the disappearance of the container and advising them to be patient while the incidence was being investigated by the police was not and could not be construed as admission of liability and negligence in mishandling the container.

hii kesi inaweza kuchukua miaka 2

na hawa jamaa hawatolipwa kitu

sasa hapo ndipo mtakapooona legal system yetu iliyooza
 
Back
Top Bottom