Mswahili umeniuliza hivi
Naomba ushahidi wa mtu kuikosoa serikali anaambiwa ni mkristu au mtu wa bara? Vinginevyo utakuwa umeamua kusema uongo.
....................
narudia tena wewe umesema umefundisha chuo kikuu cha Dar miaka zaidi ya kumi nipe ushahidi wa maneno yako kuwa mtu akiikosoa serikali kwa mambo yaliyowazi anaambiwa ni Mkristu?
Mzee Kichuguu naona sasa mnataka kutugombanisha watanzania au kuna njama za kumuhujumu JK na serikali yake. naomba ushahidi kama wewe unavyotaka ushahidi wa kuthibitisha kuwa Zitto alimchukua AC.
Nakukumbusha kuwa ni wewe uliyesema hivi, jambo lililonirusha kwenye kiti na nywele zangu zikasimama kwa mshangao:
Tn.
1.Mwanzo Nilijua vita ni kwa Ditopile kwa vile kaua. baadae nimekuja kugundua kuwa kulikuwa na zaidi ya kifo cha dereva.na mkatumia mkasa huo kupitisha hasira zenu.kisa ni Mswahili mwenzangu.
2. Mzee Mwinyi alipokuwa rais kundi la Mbatia na kimaro wenye asili za kilimanjaro, lilimchora na kuweka picha zake za nguoni-1990s na kuzuka migomo ya nguvu.sababu sikuzijua-sasa napata picha kuwa ni uswahili wake ulikuwa kero kwenu.
3. Mkapa alipokuja hakuna mgomo vyuo vikuu, sababu ni shemeji yenu jibu nimepata.hakukuwa na waraka wa Mbowe wala Kijijini leo hii.
4.Kaja JK migomo upya,na viredio vya uvunguni,nyaraka za mbowe n.k, kumpiga vita na kuchochea wanafunzi kisa ni mswahili.
5. Tanzania njema kumuunganisha Dau kwenye jina langu ni katika mfulilizo huo huo nilioutaja hapo juu.sikushangai kisa mswahili hasitahili kwanini usimuulize Mkapa ndio aliyekuwepo wakati hiyo issue?.
Jamani mmekaribishwa mjini bado mnaona wenye mji hawastahiki na kuwapiga vijembe kiasi hiki? mnataka wahame mji? wake zao ndio hivi mnawachukulia (mpakanjia) bado hamkinai?.
Mambo haya yanazidi kututanabaisha kuwa kadri utakavyowaweka karibu hawa watu na kuwafanyia ihsani wao hawana shukrani wala kheri.
kwa crusades hizi namshauri JK abadili hata madaktari na mabody guard wenye asili za ajabu ajabu.wanaweza kutupotezea rais wetu kwa kumuhujumu, maana wanaona waswahili si mahala pao kuongoza
JK wakumbatie tu usije kujuta watu hawa hawana kheri wala shukrani waangalie kwa macho mawili..
Nafahamu kuwa historically waswahili ni watu wa ukanda wa pwani ambao kwetu unaanzia Mkoani Tanga hadi Mkoani Songea ukijumuisha visiwa vya Unguja, Pemba na Mafia. Kwa hiyo, ndiyo maana viongozi kama Mwinyi wa Unguja, Kikwete wa Bagamoyo, na Kawawa wa Lindi ni waswahili. Kwa tafsiri hiyo hiyo Mkapa wa Mtwara naye ni mswahili, hata hivyo inaelekea uswahili wake kwako una walakini kwa hiyo hahesabiwi kama mswahili wa pwani.
Katika mifano yako ya migomo pale chuo kikuu, bila hata kuangalia kiini cha mgomo wenywe, wewe umesema ni ya kumpinga rais mswahili. Umesahau kuwa kama hakuna rais aliyepata msukosuko wa migomo chuo kikuu kama Nyerere, lakini hukumtaja; tena migomo wakati wa Nyerere ilikuwa ni ya kisiasa zaidi ya hii ya siku hizi ambapo wanafunzi wanadai maslahi.
Migomo wakati wa Mwinyi ulifanyika mimi nikiwapo, haikuwa inalenga serikali, bali ilikuwa inalenga utawala wa chuo. Mwinyi wakati huo akiwa chancellor aliombwa awawajibishe watawala wa pale mlimani kuendana na philosphy yake ya kuwajibika kwa vile walikuwa wanafuja fedha za wanafunzi, lakini yeye akapiga chenga, ndipo wanafunzi wakamwona kumbe naye hakuwa na msimamo katika jambo hilo. Wakati wa utawala wa Mkapa sikuwapo lakini najua kuwa wanafunzi walifanya mgomo fulani uliofanya uongozi wa chuo kujiondoa katika kusimamia fedha ya wanafunzi, nadhani kuanzia hapo wanafunzi wakawa wanapata fedha zao moja kwa moja kutoka wizarani badala ya kupitia chuo kikuu, lakini migomo hiyo ya wakati wa Mkapa hukuiona. Mgomo wa juzi ulikuwa wa wanafunzi kudai yale waliyoahidiwa na Rais Kikwete mwenyewe wakati alipokutana nao pale ukumbi wa Diamond, siyo mgomo wa kisiasa kama ule aliofanyiwa Nyerere kupinga maamuzi kadhaa ya serikali. Lakini wewe umehitimisha kuwa ni kumpinga rais mswahili.
Sasa kama wanafunzi kudai jambo ambalo ni haki yao na waliahidiwa na rais wao wewe unasema ni njama kwa vile rais ni mswahili, na katika uswahili wako umemuengua Mkapa, msomaji atakuwa ameelewa nini kama siyo sawa na nilivyoelewa kwenye post yangu ile?