ALIYEKUWA mume wa Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Chifupa (CCM), Mohammed Mpakanjia amesema kupeana kwao talaka isiwe sababu ya kumfanya mbunge huyo ajifiche na kushindwa kutekeleza majukumu yake ya siasa.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na HabariLeo Dar es Salaam jana, Mpakanjia alisema kupeana talaka ni jambo la kawaida katika maisha hivyo Amina awe huru kufanya shughuli zake za siasa.
Mpakanjia na Amina ambao wamedumu katika ndoa kwa miaka mitano na wana mtoto mmoja wa kiume wa miaka minne, walitalakiana Alhamisi iliyopita kwa sababu ambazo hazijabainishwa rasmi ingawa kuna madai yasiyothibitishwa kwamba ni saa chache baada ya Mpakanjia kudokezwa na Naibu Waziri mmoja madai juu ya mwenendo usiofaa wa mkewe.
"Anaweza kushindwa kufanya kazi zake nyingine na kujikuta anapoteza muda wake mwingi kujificha ama kutopatikana katika simu zake na sehemu muhimu anakotakiwa bila sababu za msingi," alisema Mpakanjia ambaye kwa sasa anauguza majeraha aliyoyapata katika ajali ya gari iliyotokea wiki iliyopita mkoani Morogoro. Alisema anajisikia vibaya kusoma katika magazeti kuwa Amina anajificha ama haonekani mitaani, kutokana na tukio hilo, jambo ambalo anadai limekuzwa kupita kiasi.
Alisema kuwa suala la mtalaka wake ni la kijamii na kuwataka watu waliolirukia, kuliacha na kumuacha Amina, awe huru katika kufanya kazi zake. "Nisingependa kuendelea kuzungumzia suala hili, napenda kulifunga rasmi na Amina awe huru kufanya mambo yake ya kisiasa.
Mpakanjia ambaye alifanya mahojiano na HabariLeo katika kituo kikuu cha mabasi cha Ubungo, Dar es Salaam, alisema licha ya talaka bado ana ushirikiano mzuri na familia ya akina Chifupa akiwamo baba na babu yake.
"Niko hapa kumpokea babu yake Amina. Nimelazimika kuja licha ya kuwa naumwa kwa heshima na mapenzi makubwa ya familia. Ningekuwa na kinyongo nisingekuja," alisema. Wiki mbili zilizopita, Mpakanjia alijeruhiwa kwa kuungua sehemu kadhaa za mwili, baada ya gari lake kuwaka moto ghafla. Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser , liliteketea katika ajali iliyotokea mkoani Morogoro.
Hata hivyo, Mpakanjia, hakupenda kuzungumzia suala la kuwapo kwa barua aliyoiandika kwenda kwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta na kama alitaka lizungumziwe katika chama.
"Kama kutakuwa na suala la nidhamu kichama, litashughulikiwa kichama na vikao vyake. Tatizo ni dogo sana lisikuzwe na kuharibu ‘CV' ya Amina. Nataka awe huru na shughuli zake za kila siku," alisema. Pia hakupenda kuzungumzia zaidi suala la talaka.
Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria za ndoa ya Kiislamu ana nafasi ya kumrudia Amina endapo ametoa talaka moja.
Sheria ya ndoa ya Kiislamu, kuachwa kwa mke kwa talaka tatu ni ngumu kurudiana. Lakini mke huyo akiolewa na mume mwingine, kisha akaachika tena, mume wa kwanza anaweza kupeleka maombi yake tena na kumuoa upya. Lakini, endapo talaka moja itatolewa kwa mke na kuishi zaidi ya miezi, mwaka ama miaka bila kuolewa ama bila kupewa talaka nyingine mbili zilizosalia, inahesabika kuwa mwanamke huyo ameachika rasmi kisheria.
Kwa suala la matunzo ya watoto, sheria hiyo inamlazimisha mwanaume kumtunza mtoto/watoto. Ikiwezekana mke naye anastahili kutunzwa kama ana talaka moja ndani ya miezi kadhaa.
Katika moja ya vipengele vya kisheria, mume ataruhusiwa kuwachukua mtoto/watoto, endapo watatimiza miaka minane. Pia, haimzuii kuchukua mtoto/watoto kutoka kwa mwanamke, endapo itabainika kuwa hali ya mwanamke huyo kwa fedha ama maisha siyo nzuri.
Naona huu mjadala umekuwa udaku, labda na thread ipelekwe huko.interesting...
Hii Habari nzito
Kwa nyepesi nyepesi za haraka kuna watu wanadai bibie hakuwa na hiana tangu akiwa shule.
Maswali ya kujiuliza Mpakanjia alijua lini na why now?
Kama kweli mh. Zitto kale uroda wa huyu bibie, it is a big shame to himself and to my party. Nampa pole na kumtakia uponyaji wa haraka ili asimame tuendelee kukijenga chama chetu. Sio kwamba kula uroda ni kitu kibaya; kibaya hapa ni kula uroda wa mke wa mtu. Mbaya zaidi mke mwenyewe ni Amina Chifupa ambaye maadili yake ni questionable for ages.
Ukishakuwa mwanasiasa unayeng'ara lazima uwe makini sana. Ujue kuna watu watafurahia mafanikio yako na kuna wengine hawatafurahia tu bali pia watakuchukia na kufanya kila hila ili kukumaliza kisiasa. Hii ni hasa katika nchi kama za kwetu ambazo bado zimekaa kikomunisti komunisti. Sasa Zitto hata kama kweli hajamla uroda huyu binti alipaswa kujua kuwa kuwa naye karibu kiurafiki ingempeleka pabaya. Ni rahisi wote wawili kukanusha, lakini the damage has been done and it should have been possible to prevent it.
Sasa kinachotakiwa hapa kama kweli kosa hili limetokea ni Zitto kukiri na kuomba msamaha kwa Bwana Mpakanjia, kwa mke wake na kwa CHADEMA. Then asimame tuendelee na mapambano. Hakuna njia nyingine ya uponyaji hapa zaidi ya yeye kukiri na kuomba msamaha hadharani!
Zitto amekuwa mtu wa madili kwa muda mrefu sana. Nitasikitika kama kweli atakuwa amefikia hatua ya kuporomoka kimaadili kwa muda mfupi namna hii tangu awe mbunge.
Nasubiri kusikia kwake.
Hii Sasa Itawafanya Wenye Wake Wabunge Wawe Na Khofu, Pia Wale Ambao Wake Zao Watataka Wagombee Watakuwa Na Hali Ngumu Kulikubali hilo
sasa hiyo TV watagawana vipi?
NA JINA LA UNGUJA LINATOKANA NA UNGO JAAA, INAMAANISHA NI KISIWA CHENYE NEEEMA.
Kwako Zitto, sijui ni lini ulikuja Dar, kama ulikuja kimasomo (hukuwa mkazi) basi una mengi ya kujifunza mdogo wangu. Kama kweli umelala naye siwezi kushangaa sana. Ila .... kwa kumchukua mke wa mtu hapo ulikosea. Ma miss wooote wale mzee?!? njoo jijini tukupe vimwana. Ningekushauri ukae kimya wala usijibu hizi tuhuma si kwenye magazeti wala sio humu!FD
FIKIRADUNI WROTE:
Huyo mumewe hana wivu angekuwa na wivu angemuachia TAJIRI MTOTO amchekelee mkewe namna hiyo? Hivi huyu Mumewe ni wawapi? maana sidhani kama ni wa Pwani huyu.
mswahili
JF Senior Expert Member Join Date: Wed Sep 2006
Posts: 427
Rep Power: 21
--------------------------------------------------------------------------------
Heshima zetu wakuu.
Suala la Amina na Zitto halikuwa na kificho ndani ya bunge. kwa mshangao mkubwa Phillimon mikael ambaye ni mtu tuliyekuwa tunamtegea ameamua kumtetea ZITTO kwa vile ni mfuasi wake.
phillimon mikael huoni aibu kumtetea mtu anayekula mke wa mtu mchana wazi?
ina maana mkiingia madarakani wake zetu itakuwa chakula chenu? kama Zitto kaweza kuchukua mke wa mtu atashindwa vipi kuchukua rushwa na kutuingiza kwenye kashfa za Rada? sifa za kiongozi ni kuaminika kwa watu wake na kuwa na sifa njema kwa wananchi, kwa hali hii mtu ukiwa na mkeo wakati wa kampeni usimruhusu aende kwenye kampeni za Chadema.
Mwanakijiji.
Unazidi kujishusha hadhi yako kwa kutetea ujinga yaani unapinga Zitto hajafanya kosa anasingiziwa tu. Phillimon Mikael hajakanusha na anashabikia jambo hilo. Zitto mwenyewe anakubali kuwa yuko karibu na Chifupa kwa vile mtu makini na anafaa kufanya nae kazi. wewe unabisha tu kwa vile aliyefanya ni Chadema. wewe na Phillimon nani chadema zaidi? wewe na Mwanasiasa nani anaijua chadema zaidi? Mwanakijiji kuwa Neutral mke wa mtu anachukuliwa wewe unasema sio issue? jee issue ni kuandika barua kwa Rais JK kisa Tanzania Daima limepewa onyo.
WANABODI.
Huyu ZITTO KABWE ajiuzulu na hafai uongozi labda aongoze wanaume tu.
last week CEO wa BP Lord Browne amejiuzulu kutokana na kashfa hizo hizo za KI ZITTO.
Waziri wa Mambo ya ndani wa U.K David BLUNKETT alilazimika kujiuzulu kwa kujaribu kumsaidia kupata visa mtumishi wa kimada wake ambaye hakuwa mke wa mtu. leo ZITTO kavunja ndoa ya Mpakanjia lakini Phillimon na Mwanakijiji wanafagilia tu.
kama mnafuata sheria za western world wenzenu wamejiuzulu. haya ya kukaa na wake za watu kwa uaminifu yameshinda mnataka tuwape nchi?