Karibuni Wote Regia Mtema Day: Monday 14th Jan 2013; Peacock Hotel

Karibuni Wote Regia Mtema Day: Monday 14th Jan 2013; Peacock Hotel

Joined
Jul 14, 2008
Posts
1,820
Reaction score
1,036
attachment.php
​
​

Siku ya Jumatatu; tarehe 14 January 2013 ni siku ambayo Regia Mtema Foundation imeitenga maalumu kwa ajili ya kumbukumbu ya Regia Mtema. Katika siku hii maalumu wote mnakaribishwa Peacock Hotel ambako kutakuwa na maada mbalimbali zitakazowasilishwa na kujadiliwa kama alivyozisimamia Regia. Katika siku hii maalumu wageni na wadau mbalimbali wamethibitisha kushiriki.

Hafla hii maalumu itaanza saa 9.00 Alasiri na kumalizika 2.00 usiku na kisha kufuatiwa na chakula cha usiku. Ratiba kamili itahusisha matukio yafuatayo:

  1. Historia ya Regia itakayowasilishwa na Mh. David Kafulila
  2. Mada juu ya Rushwa itakayowakilishwa na Takukuru
  3. Ulemavu Siyo Kutoweza itakayowasilishwa na Bi Shida Salum - Mwenyekiti CHAWATA
  4. Nafasi ya Kijana katika kuchochea maendeleo na demokrasia - Mh. January Makamba
  5. Majadiliano
  6. Documentary za Regia Mtema
  7. Remarks kutoka kwa Mh. Zitto Kabwe; Mh. John Mnyika na Hussein Bashe na Mzee Mtema
  8. Chakula cha jioni
  9. Networking

Wasimamizi wa hafla hii watakuwa: Pascal Mayalla na Lara Williams

Thibitisha kuhudhuria kwako kwako kupitia number: 0713 694 820

CC: Pasco; lara 1; Mzee Mwanakijiji - Naomba msambaze mwaliko huu.

Wasalaam

Sanctus Mtsimbe
Mwenyekiti; Regia Mtema Foundation
Sokoine Drive/Pamba Road
Opposite Luther House or Life House/Tancot House;
2[SUP]nd[/SUP] Floor; Left Wing (3rd Floor including Mezanine)

Mods Paw ama wengine mtuwekee thread ya kamanda Regia wakati akitoa majibu ya kazi zake maana nakumbuka Regia alikuwa ni JF na JF ilikuwa ni Regia... RIP Regia
===============
Hii hapa
Niliyoyafanya tangu niwe Mbunge..

Paw
 
Attachments

  • REGIA MTEMA POSTER.jpg
    REGIA MTEMA POSTER.jpg
    68 KB · Views: 772
Hapo Mnyika tuu ndio sio wa wana ukoo wa masalia,wafadhili wa masalia hao watoa mada ni timu inayojieleza kuwa kuna jambo , tumwombee marehemu awe pema peponi Kila la heri mutatuambia yatakayojiri vipi foundation yake iliendelezwa
 
Jamani ulitaka nani awekwe?
 
peacock hotel gharama ya ukumbi si itakuwa gharama, kwa nini tusifanye kijiweni au sehemu affordable au nyumbani kwa great thinker yoyote halafu hiyo pesa ya peacock hotel tusaidiane kupunguza umaskini ? wazo tu
 
Je sh ngapi kiingilo pamoja na chakula cha jioni

Hapo ndipo penye moyo wooote wa hii hafla. Manake bila kujua unatakiwa kujipinda vipi mfukoni mwako inakuwa vigumu kufanya maamuzi. Au ni takrima toka kwenye Foundation?
 
Nakuthibitishia ni kweli hakuna kiingilio mkuu

Unakaribishwa sana kuanzia saa tisa jioni. Ukiwa na hoja ya ku-share na wenzio itakuwa vema zaidi ingawa unaalikwa kusikiliza pia

Mkuu hakuna kiingilio na msosi pamoja na networking unapata? Basi kheri kama kweli
 
peacock hotel gharama ya ukumbi si itakuwa gharama, kwa nini tusifanye kijiweni au sehemu affordable au nyumbani kwa great thinker yoyote halafu hiyo pesa ya peacock hotel tusaidiane kupunguza umaskini ? wazo tu

kweli tumetofautiana sana duniani. Umeona watoa mada, uwapeleke kijiweni au nyumbani kwa mtu, nyumba gani inaaford watu zaidi ya mia kwa mdahalo? umasikini upo tu hata tukisevu vipi.
 
kweli tumetofautiana sana duniani. Umeona watoa mada, uwapeleke kijiweni au nyumbani kwa mtu, nyumba gani inaaford watu zaidi ya mia kwa mdahalo? umasikini upo tu hata tukisevu vipi.
yote ni ya kheri, kikubwa roho yake iwe pema peponi!! heri na baraka ziwe katika siku hiyo! jamani mjitokeze kwa wingi, ningekuwa dar ningehudhuria!
 
Back
Top Bottom