Karibuni Wote Regia Mtema Day: Monday 14th Jan 2012; Peacock Hotel

Karibuni Wote Regia Mtema Day: Monday 14th Jan 2012; Peacock Hotel

Joined
Jul 14, 2008
Posts
1,820
Reaction score
1,036
attachment.php

​

Siku ya Jumatatu; tarehe 14 January 2013 ni siku ambayo Regia Mtema Foundation imeitenga maalumu kwa ajili ya kumbukumbu ya Regia Mtema. Katika siku hii maalumu wote mnakaribishwa Peacock Hotel ambako kutakuwa na maada mbalimbali zitakazowasilishwa na kujadiliwa kama alivyozisimamia Regia. Katika siku hii maalumu wageni na wadau mbalimbali wamethibitisha kushiriki.

Hafla hii maalumu itaanza saa 9.00 Alasiri na kumalizika 2.00 usiku na kisha kufuatiwa na chakula cha usiku. Ratiba kamili itahusisha matukio yafuatayo:

  1. Historia ya Regia itakayowasilishwa na Mh. David Kafulila
  2. Mada juu ya Rushwa itakayowakilishwa na Takukuru
  3. Ulemavu Siyo Kutoweza itakayowasilishwa na Bi Shida Salum - Mwenyekiti CHAWATA
  4. Nafasi ya Kijana katika kuchochea maendeleo na demokrasia - Mh. January Makamba
  5. Majadiliano
  6. Documentary za Regia Mtema
  7. Remarks kutoka kwa Mh. Zitto Kabwe; Mh. John Mnyika na Hussein Bashe na Mzee Mtema
  8. Chakula cha jioni
  9. Networking

Wasimamizi wa hafla hii watakuwa: Pascal Mayalla na Lara Williams

Thibitisha kuhudhuria kwako kwako kupitia number: 0713 694 820

CC: Pasco; lara 1; Mzee Mwanakijiji - Naomba msambaze mwaliko huu.

Wasalaam

Sanctus Mtsimbe
Mwenyekiti; Regia Mtema Foundation
Sokoine Drive/Pamba Road
Opposite Luther House or Life House/Tancot House;
2[SUP]nd[/SUP] Floor; Left Wing (3rd Floor including Mezanine)
 
sehemu yenyewe tu inatishia maisha kwa akina kabwela hebu tupe data hapa kabla hatujakurupuka kumaliza vocha kupiga hiyo namba,je kuna kiingilio au ni bure? kama kipo ni kiasi gani?natanguliza shukrani za dhati kwa taarifa.
 
Asante Asnam; hakuna kiingilio, so ni bure.

Karibu sana na naomba uwaalike na wengine.
 
Last edited by a moderator:
I wish ningepata nafasi! Jambo lenye kheri kama hilo linapaswa kupata muitikio mkubwa.

Regia, her legend will never end!
Tangazeni kama kuna mchango kiasi gani kwa ajili ya REGIA MTEMA FOUNDATION. Chakula kitamgharimu mshiriki kiasi gani? Thx.
 
Kiongozi wangu Arushaone asante sana kwa utambuzi wako kuwa jambo hili ni la heri.

Hakika huitaji kiingilio kwa ajili ya hafla hii wala chakula. Hata hivyo RMF inawakaribisha wote wenye mapenzi mema kuchakia chochote watakachoweza!

Tunashukuru sana na tunaomba uwape na taarifa wengine.
 
Last edited by a moderator:
Kila la kheri kwa maandalizi. Hamtaipa nafasi familia kusema machache, hata walau saa za kuangalia documentaries? Tuko pamoja.

Asante sana King'asti. Familia imepewa nafasi. Ukiangalia item No. 7 moja kati ya wasemaji ni Mzee Mtema. Pia documentary imeaandaliwa kwa kushirikiana na familia.
 
Last edited by a moderator:
Wengine CCM Damu wenzenu! Itabidi tuje kushow some love japo kwa makini sanaaa!
lara 1 hakuna itikadi ndani ya RMF ndo maana unaona wote vijana wa CDM na CCM wapo. Na hata vyama vingine wote wanakaribishwa.

Tafadhali tusaidiane kuwaalika wadau wote.
 
Last edited by a moderator:
Wengine CCM Damu wenzenu! Itabidi tuje kushow some love japo kwa makini sanaaa!

lara 1 kwenye list si umeona hakuna itikadi? January Makamba yuko CCM pia wabunge NCCR MAGEUZI et al watakuwepo. Please attend!
 
Last edited by a moderator:
lara 1 kwenye list si umeona hakuna itikadi? January Makamba yuko CCM pia wabunge NCCR MAGEUZI et al watakuwepo. Please attend!

Mimi tena CCM Originale siwezi kukosa!!!!!! Lazima nifike mkuu! Hapo nilitaka tu kuleta mjadala wa kichama ili kuchangamsha jukwaa!
 
Mimi tena CCM Originale siwezi kukosa!!!!!! Lazima nifike mkuu! Hapo nilitaka tu kuleta mjadala wa kichama ili kuchangamsha jukwaa!

Nimekupata lara 1 ila nina wasi na itikadi yako kichama. Mwandiko wako haunipi haha
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom