Karibia mtaa mzima Sinza A tumeibiwa

Karibia mtaa mzima Sinza A tumeibiwa

Kiboko yao ni kuFunga system ya Intruder Alarm kutoka KK Security / Gardaworld, ukipuliza dawa System hailali, akiingiza mkono au kichwa inapiga King'ora, na unaweza kuchagua system itume sms kwenye simu ya watu wako wakaribu kadhaa, pia kwa ulinzi kamili ni kuunganisha system hiyo na control Room yetu ili pindi king'ora kinapolia wanatuma gari yenye Askari wa KK/Gardaworld kwaajili yakuangalia usalama kwenye eneo lako, inafungwa maofisini,nyumbani na pia inaweza kuunganishwa kwenye electricic fence yako. Wasiliana nami kwa WhatsApp number 0743171049 au email victor.valence@garda.com Nchi nzima.
Ungetaja na bei mkuu
 
Namshukuru Mungu tokea nimezaliwa hatujawahi ingiliwa na wezi au majambazi.
Tokea nimeoa sijawahi ingiliwa wala ibiwa.
Nimeishi huko Kigamboni hawajawahi niotea. Nimeishi Kimara hawajawahi niotea
Nimeishi Kinyerezi hawajawahi niotea.
Nimeishi mbezi Beach hawajaniotea
 
grill pana inawashawishi wezi wapate tamaa ya kuiba mpaka sofa
Kuna namna ingine, grill yako iweze kufunguka kwa ndani. Yaani unapodesign dirisha lako, unahakikisha grill inafungukia ndani. Then baada ya grill ndio unaweka aluminium frame. Hizo grill ziwe na kikomeo kwa ndani kwa ajili ya kulock
 
ANAYEJUA JINSI YA KUJIKINGA”
Hilo ombi ni kuwa fungeni hidden cctv
Hata kwa mchango kila nyumba
Wekeni camera ndio dawa ya majizi
Mambo ya sungusungu yalishapitwa sasa ni camera tu
Siku hizi haujitaji "hidden" cctv. Hata ikiwa inaonekana ni ulinzi tosha. Maana watahofia hata kusogelea
 
Mwezi wa 7 tarehe 13 jmosi.. walinipiga kwa njia hyo ndani kila kitu. Bahati nzuri laptop hawakuiona ndani ya backpack nadhani ningewehuka kama ingeibiwa
 
Muwe mnaweka ndoo au mabeseni yaliyojaa maji angalau vyumbani plastic au beseni moja la maji kila chumba pia sebuleni inasaidia ku difuse dawa ya usingizi endapo mtapuliziwa kupitia madirishani
 
JF Siku hizi imejaa watu wako sooo frustrated...
 
Dawa ya kupulizia dawa yake ni maji unaweka kwenye jagi au beseni dogo ikipulizwa ndani yote mvuke wa maji mtakuta Kama povu tena walivyo wapuuzi wakisha puliza wanakata au kuongea kwa sauti wanajua washakupiga nusu kaputi wakianza kukata au kuingiza kitu cha kutolea lazima usikie hawataamini wataona kama mzuka na kukimbia mbaya nilikaa mitaa mibovu kipindi fulani wale wahuni waliwaliza watu kwangu wanakuja na makelele yao maji yalinisaidia...nakumbuka ni Sinza hiyo hiyo maeneo ya makabe....
 
Leo imekuwa ni vilio na hamaki kwa raia wa hapa Sinza A, baada ya kuamka asubuhi na kukuta madirisha yao yametobolewa na kukatwa kwa nyavu.

Inasemekana, walipuliza dawa ya usingizi ndipo wakafanya unyama huo. Watu wameibiwa pesa, laptops, simu, vitu vya ndani kibao.

Hapo unapoishi, kuna wizi wowote umefanyika?

Anayejua jinsi ya kujikinga na hiyo sawa, atupe elimu hapa.

Poleni wahanga wote wa wizi huo.

Nawasilisha!

VERY SIMPLE (wekeni ndoo za maji chumbani zikiwa zimejaa maji) ile dawa ikipulizwa hufuata unyevunyevu na kwahiyo hukimbilia puani kwenye huo unyevunyevu lakini ukiweka maji hiyo dawa inakimbilia kwenye maji.
 
Poleni! hakuna hata nyumba ya mchawi mmoja au mwenye CCTV mtaan kwenu ? akawaokoa? ila nishajizoesha kuficha kila kitu uvunguni tangu niibiwe kwa style hiyo
Kamjulishe makonda yaani asubuhi wezi watadakwa
 
Hivi wewe una akili kweli yaani kila siku uwe unaweka beseni la maji chumbani as if kila siku wezi watakuja si Upuuzi huo? Hebu acha mawazo finyu hivyo badala uwekeze kwenye ulinzi we unaleta mawazo ya Ajabu ajabu
Muwe mnaweka ndoo au mabeseni yaliyojaa maji angalau vyumbani plastic au beseni moja la maji kila chumba pia sebuleni inasaidia ku difuse dawa ya usingizi endapo mtapuliziwa kupitia madirishani
 
JF kuna wapumbavu wengi kweli, mada serious watu wanachangia ujinga hadi kero

Dawa ya kudhibiti wezi kama hao ni kuweka zile chuma za dirishani zikiwa zimebanana tu ili asiweze kupitisha simu

Madirisha mengi yana ma grill yenye nafasi kubwa sana na mengine hayana kabisa,
Inabidi kubadili staili ya ujengaji wa nyumba kukabiliana na hatari hii
Hata wewe hujatoa suluhisho au niseme suluhisho lako halitekelezeki, asilimia kubwa ya watu wa huko wamepanga kwa hiyo wawe wanatembea na madirisha wakifika kwenye nyumba wanaweka madirisha yao?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom