Karibia mtaa mzima Sinza A tumeibiwa

Karibia mtaa mzima Sinza A tumeibiwa

Leo imekuwa ni vilio na hamaki kwa raia wa hapa Sinza A, baada ya kuamka asubuhi na kukuta madirisha yao yametobolewa na kukatwa kwa nyavu.

Inasemekana, walipuliza dawa ya usingizi ndipo wakafanya unyama huo. Watu wameibiwa pesa, laptops, simu, vitu vya ndani kibao.

Hapo unapoishi, kuna wizi wowote umefanyika?

Anayejua jinsi ya kujikinga na hiyo sawa, atupe elimu hapa.

Poleni wahanga wote wa wizi huo.

Nawasilisha!
Hamia Nyumba zenye madirisha safi ya vioo huo ushamba wa kukaa Nyumba wamebandika manyamvu utazani banda la kuku!! Kama ni Nyumba yako toa huo uchafu weka kioo
 
Wanapokuja wezi kuwapulizia dawa ya usingizi kusudi mlale fofo na wizi ufanyike, fanyeni hivi kabla hamjalala!
Tia maji kwenye beseni lililo wazi kisha liweke chumbani kwako sehemu ya wazi, endapo wakija wakipulizia dawa tu, Yale maji yaliyopo kwenye ilo beseni basi litanyonya sumu yote iliyopulizwa humo ndani na kukuacha salama.
Na kwa njia iyo utaweza stuka mapema.
Duh unatufundisha kukojolea kwenye beseni usiku tukiamka? Acha tabiya ya kishamba ya kukojowa kwenye makopo!! Unalala na maji chumbani kwenye beseni Wewe samaki?
 
ANAYEJUA JINSI YA KUJIKINGA”
Hilo ombi ni kuwa fungeni hidden cctv
Hata kwa mchango kila nyumba
Wekeni camera ndio dawa ya majizi
Mambo ya sungusungu yalishapitwa sasa ni camera tu
Camera zitaondolewa wakiiba kama kule Dodoma kwa lisu
 
JF kuna wapumbavu wengi kweli, mada serious watu wanachangia ujinga hadi kero

Dawa ya kudhibiti wezi kama hao ni kuweka zile chuma za dirishani zikiwa zimebanana tu ili asiweze kupitisha simu

Madirisha mengi yana ma grill yenye nafasi kubwa sana na mengine hayana kabisa,
Inabidi kubadili staili ya ujengaji wa nyumba kukabiliana na hatari hii
Wengine tumepangosha chumba tu au chumba na sebule. Ukiongea habari ya grill meenyenyumba snasema at your own cost
 
Acha ungese wewe, ina maana wakati mnapanga kwenda kuiba Sinza mlikubaliana sababu Sinza kumejaa mashoga? watu wapo serious wewe unaleta kashfa na matusi? Tumia hekima kwa kuwapa pole wahanga na kuchangia nini kifanyike.
sinza mapunga kibao
 
JF kuna wapumbavu wengi kweli, mada serious watu wanachangia ujinga hadi kero

Dawa ya kudhibiti wezi kama hao ni kuweka zile chuma za dirishani zikiwa zimebanana tu ili asiweze kupitisha simu

Madirisha mengi yana ma grill yenye nafasi kubwa sana na mengine hayana kabisa,
Inabidi kubadili staili ya ujengaji wa nyumba kukabiliana na hatari hii
simu weka chini ya mto,kitanda chako kichwa kiwe upande wa dirisha,hatoweza kuchukua simu wala laptop
 
JF kuna wapumbavu wengi kweli, mada serious watu wanachangia ujinga hadi kero

Dawa ya kudhibiti wezi kama hao ni kuweka zile chuma za dirishani zikiwa zimebanana tu ili asiweze kupitisha simu

Madirisha mengi yana ma grill yenye nafasi kubwa sana na mengine hayana kabisa,
Inabidi kubadili staili ya ujengaji wa nyumba kukabiliana na hatari hii
Ushaambiwa nyumba za kupanga...
kubananisha nondo ni gharama...
 
Leo imekuwa ni vilio na hamaki kwa raia wa hapa Sinza A, baada ya kuamka asubuhi na kukuta madirisha yao yametobolewa na kukatwa kwa nyavu.

Inasemekana, walipuliza dawa ya usingizi ndipo wakafanya unyama huo. Watu wameibiwa pesa, laptops, simu, vitu vya ndani kibao.

Hapo unapoishi, kuna wizi wowote umefanyika?

Anayejua jinsi ya kujikinga na hiyo sawa, atupe elimu hapa.

Poleni wahanga wote wa wizi huo.

Nawasilisha!
Kuna kipindi hili suala la dawa ya usingizi lilijadiliwa hapa JF. Ufumbuzi ukawekwa hapa jukwaani. Ni hivi, kwa kawaida maji yanafyonza hewa yenye sumu inayopulizwa na kama yataachwa wazi bila kufunikwa yanawezasaidia kuifanya hiyo dawa ishindwe kutoa kusudio lake. Wadau walishauri tukilala tuache ndoo ya maji wazi. Mimi najitahidi sana kutekeleza kufata huo ushauri ili kujilinda. Ingawa sijapata mrejesho wa mtu aliyeacha ndoo ya maji wazi na kuibiwa kwa kupuliziwa dawa ya usingizi, basi yawezekana kuna ukweli na uhalisia katika hilo!
 
Leo imekuwa ni vilio na hamaki kwa raia wa hapa Sinza A, baada ya kuamka asubuhi na kukuta madirisha yao yametobolewa na kukatwa kwa nyavu.

Inasemekana, walipuliza dawa ya usingizi ndipo wakafanya unyama huo. Watu wameibiwa pesa, laptops, simu, vitu vya ndani kibao.

Hapo unapoishi, kuna wizi wowote umefanyika?

Anayejua jinsi ya kujikinga na hiyo sawa, atupe elimu hapa.

Poleni wahanga wote wa wizi huo.

Nawasilisha!
Msiwe mnalala bila ya kuwa na chombo cha wazi chenye maji mfano beseni ndogo iwe imejaa maji wakipuliza huwa inavuta yote na haiwaathiri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom