Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 59,468
- 119,622
Naona mimi tu ndio sijaelewa
Naona mimi tu ndio sijaelewa
Sio kweliPoleni sana.
Marekebisho kwenye fasihi sio KUIBIWA kwa muktadha wa habari yako ni KUIBWA.
Sawajaribu kutafakari utaelewa
scrub saa moja haiusiani hapa. Kuna watu wana namna mbalimbali za kutengeneza pesa wengine kazi zao ni usiku,wengine madalali. Unaweza kuta huyo ulie muona hapo kazi zake zina mtaka awe smart muda wote.Sinza saa1unamkuta mvulana wa age ya kati anascrub saloon!unajiuliza maswali kibao ...!betting zimewaharibu sana watu..hamjui tu!
Sasa utalala nae chumbani huko sinzaa ?Mimi nimefuga mbwa German sherphad, wapo dolia kila siku night, sasa wewe sogea
Sasa utalala nae chumbani huko sinzaa ?
Wafuge mbwa Koko nyumba moja ikivamiwa tote tunabweka mtaa mzima, uzuri wa Koko huwa anabweka huku anagonga mlango tayari kukimbilia ndani kumbe ndio anakuamsha
Nenda Goba aseeNilifikiria kuja kupanga Sinza, kumbe ushenzini sana. Asante kwa taharifa mkuu. Plain A nimeifuta, naendelea na plan B mbezi beach au Goba
Mkuu Tena Koko hachagui chakula hata mandazi anakula hao German wanakula nyama tu ukimpa ugali haliSikupingi, zamani nilikuwa nafuga koko, nje kukiwa na hatari, wanakuja dirishani kwangu wanaanza kubweka.. mzee unamka chapu na sime yako, unatoka nje, kucheki usalama.
Hawa koko wanaona mbaka wachawi.
Hivi unajua kama hao wanaoibiwa hivi ni wale maskini kwenye nyumba tena za kupanga?Hii ndio suluhisho sahihi. Tatizo watanzania bado tunaishi kizamani mtu unaibiwa kitu halafu bado eti unauliza "nifanye nini" hivi ni kweli kwmb hujui cha kufanya?
Kupitia wizi kwenu umepenyeza CV ya mzee wakoSitasahau siku tulipo ibiwa nyumbani nikiwa na babu yangu chumbani mimi nikiwa kadogo nazani ni mwaka 1993.Hii ya madawa kupuliziwa ilikuwa haijawa insu sana kwa miaka ile ila ndo ilitutokea.
Kutokana na mazingira ya kijijini, mzee wetu alikuwa ana nyumba zaidi ya moja hapo nyumbani na sisi kama wajukuu tulikuwa tukilala na babu mimi pamoja na kaka yangu.Asubui baada ya kuamka ndo tukagundua kuwa tumeibiwa. Babu alikuwa na bunduki moja ambayo alikuwa ameiegemeshea ukutani karibu na kitanda,magunia kama manne ya mpungu na mahindi,wakachukua na vitu vingine vidogo dogo, tuliamka saa mbili asubui tena kwa kuamshwa maana haikuwa kawaida ya mzee kulala usingizi wa namna hiyo, kawaida yake yeye alikuwa mtu wa kukaa macho sana wakati wa usiku kutokana na hali ya kuwa na mifugo hapo nyumbani.
Babu alishangaa, alisema mara moja tu alipo amka" tumeibiwa" kuangaria bunduki haipo kutoka nje mlango umevunjwa sijui na mashine gani hiyo. Polisi wakaja wakamchukua babu hadi kituoni baada ya kuangalia mazingira ya huo uporaji.Walienda kumuweka hapo kituoni lakini mkuu wa kituo sijui na nani wakasema haiwezekani mzee kufunguriwa mashitaka kwa kosa la upotezefu wa siraha, mana wengine walijaji ya kwamba huenda ameamua kuiuza kwa majambazi kwa kuwa amezeeka,ila huyo jamaa alikataa akasema huyu mzee kamiliki silaha tangu serikali ya mkoloni na ameshirikiana na sisi aiku nyingi kwa mambo ya kiusalama haiwezekani kumhisia vibaya katika tukio hilo, ikabidi wamuachie, wakamrudisha home mida ya saa nne usiku. Hiyo bunduki ilikuja kukamatwa na polisi katika tukio moja la kijambazi ikiwa imekatwa ule mtutu na kuwa fupi, yani ikipigwa risasi mita mia tatu utazani imepigiwa mgongoni mwako.
Sifa ya mzee ilikuwa ni shabaya, alikuwa mlengaji, sniper, hakuna wa kuweza kumfuata kwa uwezo wake na hivyo alikuwa akitumika a serikali kwa mambo ya kupiga wanyama waliotoka hifadhini na kuanza kuleta madhara kwa raia, mana mnyama mkari ilitakiwa umpige kichwa na ukikosea ukapiga hewa hapo kitimu timu lazima kiwepo mana na yeye anaanza kujihami, walio kaa kalibu na mapori wanajua, utasikia anasema nina hasira kama nyati aliyekoswa na risasi. Sasa huyo mzee alikuwa nauwezo wa kupiga kichwa cha mnyama hata kama anakimbia.
Mara ya mwisho alimpiga mwewe aliyekuwa anachukua vifaranga vya kuku alikuwa ametuakwenye mti pembeni na nyumbani,alipigwa kichwa kikasambaa kwa risasi, yani ilibaki shingo tu kichwa hakipo,wakamchokonoa kwa selele yale ma miti malefu yanayoota katikati ya katani ndo akaanguka mana alikuwa amenasa miguu yake ivo ivo kama alivyokuwa hai kule mtini. R.i.p babu yetu.
Mkuu Tena Koko hachagui chakula hata mandazi anakula hao German wanakula nyama tu ukimpa ugali hali
Sitasahau siku tulipo ibiwa nyumbani nikiwa na babu yangu chumbani mimi nikiwa kadogo nazani ni mwaka 1993.Hii ya madawa kupuliziwa ilikuwa haijawa insu sana kwa miaka ile ila ndo ilitutokea.
Kutokana na mazingira ya kijijini, mzee wetu alikuwa ana nyumba zaidi ya moja hapo nyumbani na sisi kama wajukuu tulikuwa tukilala na babu mimi pamoja na kaka yangu.Asubui baada ya kuamka ndo tukagundua kuwa tumeibiwa. Babu alikuwa na bunduki moja ambayo alikuwa ameiegemeshea ukutani karibu na kitanda,magunia kama manne ya mpungu na mahindi,wakachukua na vitu vingine vidogo dogo, tuliamka saa mbili asubui tena kwa kuamshwa maana haikuwa kawaida ya mzee kulala usingizi wa namna hiyo, kawaida yake yeye alikuwa mtu wa kukaa macho sana wakati wa usiku kutokana na hali ya kuwa na mifugo hapo nyumbani.
Babu alishangaa, alisema mara moja tu alipo amka" tumeibiwa" kuangaria bunduki haipo kutoka nje mlango umevunjwa sijui na mashine gani hiyo. Polisi wakaja wakamchukua babu hadi kituoni baada ya kuangalia mazingira ya huo uporaji.Walienda kumuweka hapo kituoni lakini mkuu wa kituo sijui na nani wakasema haiwezekani mzee kufunguriwa mashitaka kwa kosa la upotezefu wa siraha, mana wengine walijaji ya kwamba huenda ameamua kuiuza kwa majambazi kwa kuwa amezeeka,ila huyo jamaa alikataa akasema huyu mzee kamiliki silaha tangu serikali ya mkoloni na ameshirikiana na sisi aiku nyingi kwa mambo ya kiusalama haiwezekani kumhisia vibaya katika tukio hilo, ikabidi wamuachie, wakamrudisha home mida ya saa nne usiku. Hiyo bunduki ilikuja kukamatwa na polisi katika tukio moja la kijambazi ikiwa imekatwa ule mtutu na kuwa fupi, yani ikipigwa risasi mita mia tatu utazani imepigiwa mgongoni mwako.
Sifa ya mzee ilikuwa ni shabaya, alikuwa mlengaji, sniper, hakuna wa kuweza kumfuata kwa uwezo wake na hivyo alikuwa akitumika a serikali kwa mambo ya kupiga wanyama waliotoka hifadhini na kuanza kuleta madhara kwa raia, mana mnyama mkari ilitakiwa umpige kichwa na ukikosea ukapiga hewa hapo kitimu timu lazima kiwepo mana na yeye anaanza kujihami, walio kaa kalibu na mapori wanajua, utasikia anasema nina hasira kama nyati aliyekoswa na risasi. Sasa huyo mzee alikuwa nauwezo wa kupiga kichwa cha mnyama hata kama anakimbia.
Mara ya mwisho alimpiga mwewe aliyekuwa anachukua vifaranga vya kuku alikuwa ametuakwenye mti pembeni na nyumbani,alipigwa kichwa kikasambaa kwa risasi, yani ilibaki shingo tu kichwa hakipo,wakamchokonoa kwa selele yale ma miti malefu yanayoota katikati ya katani ndo akaanguka mana alikuwa amenasa miguu yake ivo ivo kama alivyokuwa hai kule mtini. R.i.p babu yetu.
cha muhimi ni marinda tu jamani yabaki salama
Kuna namna ingine, grill yako iweze kufunguka kwa ndani. Yaani unapodesign dirisha lako, unahakikisha grill inafungukia ndani. Then baada ya grill ndio unaweka aluminium frame. Hizo grill ziwe na kikomeo kwa ndani kwa ajili ya kulock
Hivi unajua kama hao wanaoibiwa hivi ni wale maskini kwenye nyumba tena za kupanga?
Kwa akili yako unaona ni tz wangapi wanaweza kufanya hayo