Karibia mtaa mzima Sinza A tumeibiwa

Karibia mtaa mzima Sinza A tumeibiwa

Wanapokuja wezi kuwapulizia dawa ya usingizi kusudi mlale fofo na wizi ufanyike, fanyeni hivi kabla hamjalala!
Tia maji kwenye beseni lililo wazi kisha liweke chumbani kwako sehemu ya wazi, endapo wakija wakipulizia dawa tu, Yale maji yaliyopo kwenye ilo beseni basi litanyonya sumu yote iliyopulizwa humo ndani na kukuacha salama.
Na kwa njia iyo utaweza stuka mapema.
Dah...hebu tupe sayansi yake inafanya vipi? Kadeti
 
Kuna jamaa yangu alikuwa kampuni moja ya ulinzi, kila asubuhi akirudi anakuta jamaa wameiba hata suruari,

Akawa anaweka umeme 'live wire' kwenye nondo kwa ndani.

Tangu siku alipokuta yebo yebo dirishani hiyo tabia iliisha hapo.
Ila mwanaume haipaswi kulala fofofo hadi asubuhi. Dawa ya hao vibaka ukiwakamata ni kuwafanyia tohara.
 
Ni shida sana, hata goba nilisikia kuna huu wizi. Inabidi mtu uingie gharama kubwa kulinda mali za ndani, magrill, fence, security guards nk. na vitu vyenyewe unavyolinda humo ndani ni TV, simu na laptop ambavyo havifiki hata milioni mbili. Kama ni umaskini wa watu basi umepindukia, yaani unatumia nguvu kuvunja nyumba ya mtu ili uibe TV ya laki tano!??
 
JF kuna wapumbavu wengi kweli, mada serious watu wanachangia ujinga hadi kero

Dawa ya kudhibiti wezi kama hao ni kuweka zile chuma za dirishani zikiwa zimebanana tu ili asiweze kupitisha simu

Madirisha mengi yana ma grill yenye nafasi kubwa sana na mengine hayana kabisa,
Inabidi kubadili staili ya ujengaji wa nyumba kukabiliana na hatari hii
Na raha ya grili moto utokee na uanzie mlangoni.
 
Huu wizi umerudi tena hapa mjini.

Juzi kati jamaa zangu wa Mbezi kwa msuguli. Juzi kati jamaa zangu wa makuburi external waliibiwa TV, laptops, simu n.k.

Kuna namna tunatakiwa tufanye hapa Dar.

Mwenye dawa ya hawa wahuni ailete hapa.
 
Wanaiba smart phone? Hao wezi ni mafala tu na nyie mlioibiwa nina mashaka na elimu zenu
 
Poleni! hakuna hata nyumba ya mchawi mmoja au mwenye CCTV mtaan kwenu ? akawaokoa? ila nishajizoesha kuficha kila kitu uvunguni tangu niibiwe kwa style hiyo
Nabii Tito pia anaishi Sinza.
 
Poleni! hakuna hata nyumba ya mchawi mmoja au mwenye CCTV mtaan kwenu ? akawaokoa? ila nishajizoesha kuficha kila kitu uvunguni tangu niibiwe kwa style hiyo
CCTV kuna nyumba ilikuwa nazo, lakini imeshindwa kutambua sura kwa maana ilikuwa usiku.
 
Karibu na dirishani funga kamba nyembamba mfano wa Uzi ,harafu kaifunge kwenye chumba kama tatu,ambazo umeziweka juu ya kitu kamba ikiguswa chupa zinaanguka
 
JF kuna wapumbavu wengi kweli, mada serious watu wanachangia ujinga hadi kero

Dawa ya kudhibiti wezi kama hao ni kuweka zile chuma za dirishani zikiwa zimebanana tu ili asiweze kupitisha simu
Madirisha mengi yana ma grill yenye nafasi kubwa sana na mengine hayana kabisa,
Inabidi kubadili staili ya ujengaji wa nyumba kukabiliana na hatari hii

Vipi wewe Mwerevu ,ambaye utajenga kwa mujibu Mawazo yako bila kuzingatia athari za Moto zikitokea atapona mtu kweli ndani ya hiyo Nyumba .
 
Kuna siku nilikuwa nimelala usiku kama wa saa saba hivi mara nikasikia kitu kama kina pekenya pekenya hivi,nikashtuka nikaona fimbo ndefu imepenyezwa dirishani imeitoa suruali kwenye enka ya nguo naiona inavutwa ili ityokee dirishani basi na mimi katika hali ya mshangao na ule usingizi nikairukia ile suruali.kumbe kwenye ile fimbo kwa mbele kule nchani wamechomeka kitu kama ndoano ili kunasia nguo,ikanichoma tukawa tunavutana lakini nilifanikiwa kuiokoa suruali yangu.baada ya hapo sikupata usingizi tena hadi asubuhi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom