Mimi nilicho mfanyia mwizi moja hatokuja kunisahau mpaka siku ya kufa kwake.
Sijui kama yupo hai au amekufa.
kwanza nilikata fekeo nusu kipisi, nikalinoa barabara upande moja. Sio mafekeo yote utaweza kuyafanya hivi, kuna mafekeo muhimu.
Baada ya huyu mwizi kninyima raha, nilimfanyia kazi, mpango maalumu.
Siku ya siku mchana kweupe nilishusha mzigo subufer.
uzuri mwizi wangu nilikwisha mjua, nikajua tu huyu lazima aje aniibie.
Nilicho fanya sasa, chumba changu kilikuwa na kibaraza japo ni nadra sana uswazi kupata chumba cha namna hiyo.
usiku nilitengeneza kitanda juu ya kibaraza, kwa njee. nilipanga mbao furesh na kigodoro kidogo kama cha shule bording nikawa nalala juu.
mlangoni niliweka machuma, vipisi vya spring ya magari. juu ya mlango nilitegesha vichuma ambavyo kitendo cha mlango tu kufunguliw vinadondoka vinapiga machuma ya chini. Machuma ya chini niliyajemgea cement ili mlango ukifunguliwa tu nistuke nikiwa nimelala juu ya dari. pia niliona nikiyaegesha tu mwizi anaweza kuchukua akanidhuru katika mapambano.
Nililinda siku bila mafanikio,
Siku ya siku ikawadia, siku ya nne usiku nilifunga mlango wangu kwa njee, mimi nikapanda juu kitandani kwangu. Nilipanga mbao zangu kwa ustadi mkubwa. Kwa njee nikafunga kufuli la solex ambayo huwa wanayafungua kama kwao. Kuhamanisha ndani hana mtu.
Mida ya saa tisa usiku nikamuona mtu kaja pale mlangoni ananyata. kwa sababu nilikuwa nipo on duty sikuwa nimelala.
Nilicho fanya nilikuwa nasoma mazingira, huyu yupo peke yake au, nikajiridhisha yupo peke yake.
Nilimuacha afungue mlango, ile kufungua tu vyuma viligongana. akashikwa na uwoga akarudi nyuma faster. mimi nipo kwa juu namcheki tu.
Nilishuka darini kininja nikawa nyuma yake. Nikawaza faster huyu nikimsulubu hapa itakuwa msala. Nikampa upenyo anikimbie nikala naye sahani moja. Kona ya kwanza, ya pili, tukawa tunaenda kimya kimya. Karibu na bonde nilimchapa moja takatifu mgongoni alidondoka palepale, hakika nilimchimba sana, nilimwachia fekeo palepale. Nikatafuta njia nyingine nikarudi. Ukweli that time, unikimbie labla uniache hatua 20
Mimi usiku huo huo nilimpigia dereva wa town ice, nikahama kimya kimya. Niliacha tu ujumbe kwa mwenye nyumba kupitia kwa jirani apangishe tu, nimevunja mkatabaa.
Mpaka naondoka, sii jirani wala dereva wa town ice amejua chochote. Mizigo yangu yote nikaipeleka maskani home, mimi nikaenda zangu mozambique coz nilikuwa nipo nampango huo.
Sikurudi, sikutaka kujua kama mwizi wangu yupo hai au kisha tangulia.
Ukweli mwizi wangu alinitesa sana. Kupigwa tochi usoni ilikuwa sehemu ya maisha yangu. Aliniibia smart phone ambayo nilinunua kwa kujibana mnoo.