macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 28,227
- 56,848
Hakuna ukweli wowote kuwa eti maji yana uwezo wa kuvuta dawa ya usingizi iliyopo kwenye hewa. Hili ukilisema kwenye wasomi wa ukweli watakucheka sana. Hebu toa mfano wowote wa dawa ya usingizi inayovutwa na maji yaliyo kwenye ndoo. Tuambie ni dawa gani tufanye majaribio.Kuna kipindi hili suala la dawa ya usingizi lilijadiliwa hapa JF. Ufumbuzi ukawekwa hapa jukwaani. Ni hivi, kwa kawaida maji yanafyonza hewa yenye sumu inayopulizwa na kama yataachwa wazi bila kufunikwa yanawezasaidia kuifanya hiyo dawa ishindwe kutoa kusudio lake. Wadau walishauri tukilala tuache ndoo ya maji wazi. Mimi najitahidi sana kutekeleza kufata huo ushauri ili kujilinda. Ingawa sijapata mrejesho wa mtu aliyeacha ndoo ya maji wazi na kuibiwa kwa kupuliziwa dawa ya usingizi, basi yawezekana kuna ukweli na uhalisia katika hilo!