Kariakoo kwachafuka, maduka yafungwa...

Kariakoo kwachafuka, maduka yafungwa...

niko huku kinondoni magari 4 ya jwtz yakiwa na wanajeshi full na silaha yamepita yanaenda town
 
Ndugu zangu,

Moja ya hadithi za Mtume Muhammad S.A. W ni pale Mtume Muhammad alipokuwa msikitini na maswahaba wake. Mara akaingia msikitini mtu wa kabila la Mabedui na kuanza kukojoa. Maswahaba wa Mtume wakasimama kwa hamaki kutaka kumwadhibu Bedui yule.

Mtume akawasihi maswahaba wake wasifanye jambo lolote litakalomdhuru Bedui yule. Hapo ikavutwa subira. Bedui yule akakojoa na akamaliza. Mtume Muhammad alipomuhoji Bedui yule ikabainika kuwa alikuwa ni mtu wa hovyo na wala hakujua kuwa alimokuwa ni msikitini. Bedui yule akaelimishwa, akaelewa. Akarudi kwenye ustaarabu.

Ndio mkojo ule ulifutwa kwa maji na amani ikawepo. Wahenga walinena; Subira yavuta heri. Siku zote, hamaki si jambo jema. Kwa kutanguliza subira na kutumia hekima Mtume Muhammad aliivuta heri na kuepusha shari.

Maana, kama Mtume alisingewaasa maswahaba wake kuvuta subira, basi, makubwa matatu yangetokea ndani ya msikiti ule; Mosi, zingezuka vurugu na watu kuumizana na hata kutoana roho. Pili, mkojo wa Bedui yule ungesambaa msikitini kwa vile alishaanza kukojoa na isingekuwa rahisi kwake kukatisha mkojo wake. Tatu, Mkojo una madhara ya kiafya pia.

Naam, kwa mwanadamu, ni muhimu kuwa na subra na kutafakari kabla ya kufanya maamuzi. Kwa ndugu zangu Waislamu, tunaona Mtume Muhammad ameweza kuonyesha hilo. Na kwa ndugu zangu Wakristo, kuna mifano pia ya Yesu Kristo kuonyesha subra.

Ndio, Uislamu, kama ilivyo kwa Ukristo na dini nyingi za humu duniani, msingi wake ni amani na upendo. Kitendo cha mtoto yule wa Mbagala kukojolea korani kitazamwe kwa sura ya kitendo kilichofanywa na mtoto .

Na kama ilivyokuwa kwa Bedui yule, kama pale Mbagala subira na hekima vingetangulizwa, basi, yumkini tungebaini kuwa mtoto yule hakujua madhara ya kitendo chake. Naye angekanywa kama tuwakanyavyo watoto wetu. Na hata kitendo hicho kingefanywa na mtu mzima, bado tulikuwa na haja ya kutanguliza subira na hekima kumhoji aliyetenda, yaweza akawa kama Bedui yule kwenye msikiti alimosali Mtume na maswahaba wake.

Na kwa kuangalia picha zile za Mbagala naiona hatari iliyopo sasa, kuwa tuna vijana wengi wasio na kazi; Wakristo kwa Waislamu. Vijana wasio na dogo. Ni kama moto uliofifia. Akipatikana kwa kuchochea kuni wanalipuka.

Ni vijana wanaopatikana wakati wowote na mahali popote. Hata jambo likianza saa tatu asubuhi wao wapo. Hawana ofisi wala bosi wa kumwomba ruhusa ya kwenda kuandamana na kurusha mawe. Ndio hawa wanaonekana wamevaa ' Kata kiuno' na wengi wao hawajahi hata kuingia misikitini au makanisani.

Inakuawaje kijana wa kweli wa Kiislamu achome kanisa na kuiba kompyuta. Inakuawaje kijana na muumini wa kweli wa Kiislamu aonekane saa mchana wa jua kali akivamia baa na kukimbia na kreti za bia? Ni maswali yanayotutaka tutafakari kwa makini.

Maana, ninavyoamini mimi, uchumi na elimu duni ndio hasa vinavyochochea vurugu za kijamii, iwe za kidini au kisiasa, na hususan inapohusisha vijana. Vijana wetu hawana misingi mizuri ya elimu, na wengi hawana ajira pia. Haya ni sawa na makombora yasiyo na gharama kubwa kuweza kutumiwa na wanasiasa wasio waadilifu na hata viongozi wa kidini wenye mitazamo mikali. Ni makombora yaliyoanza kutulipukia. Tuliziona ishara, tukazipuuzia.

Leo Kuna vijana watakaotumiwa au kutumia fursa hiyo kutenda maovu kwa kisingizio cha dini. Ni hawa wataoshiriki kuchafua taswira za dini husika pia. Tujiadhari, kabla ya hatari kubwa inayotujia. Hatujachelewa.

Na hilo ni Neno La Leo.
 
Nipo magomeni polisi wanapiga mabomu ovyo..
 
vijana wa Mwamunyange wamemwagwa hapa Kariakoo na soko la kariakoo limefungwa pamoja na huduma mhimu kama mabenki kupisha zoezi la kutuliza vurugu.
 
Nimeipata hii from tweeter
 

Attachments

  • waislam.jpg
    waislam.jpg
    90.1 KB · Views: 190
nikiwa maeneo ya magomeni naziona gari nne aina ya roli zenye wanajeshi wa kutosha wakiwa na silaha za kutosha wakielekea kariakoo. kwa upande wa hapa magomeni msikiti wa kichangani wametulia baada ya ffu kupiga mabomu ya machozi matatu na gari la kuwasha limepaki katika mlango wa kuingilia msikitini.

Kinachoenda kufanyika sasa ndio ile " operation okoa"
 
Nimeyakumbuka maneno ya maaskofu wa KKKT jana kule mbagala.
''Machozi yenu na majivu haya yatazaa Tanzania mpya yenye watu wanaoheshimiana............
Vita yetu SI YA DAMU NA NYAMA...........Mungu wetu tunayemwamini si Mungu wa kulipiza visasi.''

(WHATEVER YOU DO YOU HAVE TO KEEP MOVING FOWARD). mkuu andrew : Signature yako nimeielewa ingawa mwenyewe huielewi. unaonaje uibadilishe. manake unaonekana haupo tayari kubadilika na wanaoleta mabadiliko chanya.
 
Tatizo kubwa ni kikwete. wanasema muislamu mwenzetu atatulinda.

As long as kikwete is in power this country will become ungovernable.

Let us kick him out of office for the sake of the coming generations.
 
Habari ni kuwa hapa maeneo ya makumbusho waandishi wa blog yangu wamepishana na malori ya wanajeshi JWTZ wanaoelekea kwenye jumba jeupe kudhibiti kundi la waislam wanaotaka kwenda ikulu.Maeneo ya posta kuelekea mambo ya ndani napo kimenuka ni moshi wa mabomu.kariakoo maeneo ya kongo mpaka karibu na msiki wao kimenuka.Makumbusho napo kimenuka ma sheikh kadhaa na wafuasi wao wametiwa nguvuni hali si shwari jijini dar.Picha baadae jamani.
 
Polisi wameweka kambi hapa magomeni kwenye kwenye kituo cha mafuta Gapco kuna magari ya polisi kumi na gari ya maji ya kuwasha.
 
Sisi huku hatujambo tu! Ni hawa watu wa ponda wanatusumbua kudogo.ninyi huko hamjambo!
 
tupo tayari kwa lolote hata mkienda kuchukua jeshi la obama marekani haturudi nyuma tushachoka kufanywa wapangaji wakati nyumba yetu sote
........... Kwa mbaali naona kuona utofauti kati ya waislam na Uislam................:thinking:
 
Back
Top Bottom