Hii Ndio Mitaa Iliyonipa Pesa Nyingi Kariakoo

Hii Ndio Mitaa Iliyonipa Pesa Nyingi Kariakoo

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
8,357
Reaction score
14,834
Habari wakuu,

Nikiwa mfanyabiashara wa retail, leo nimeona nitoe shukrani za dhati kwa mitaa ya Kariakoo ambayo imekuwa sehemu kubwa ya mafanikio yangu.

Nilianza nikiwa nimeajiriwa kwenye kampuni ya construction, kitengo cha manunuzi (Procurement). Kazi yangu ilinifanya nizunguke Kariakoo karibu kila siku kutafuta vifaa vya ujenzi na kujenga mahusiano na wauzaji.

Kadri muda ulivyokwenda, niligundua fursa kubwa iliyokuwa mbele yangu. Nikafanya uamuzi mgumu wa kuacha ajira na kuingia kwenye biashara ya hardware kwa muda wote.

Leo nikikumbuka safari yangu, siwezi kuizungumza bila kuitaja Kariakoo.

Kama wewe ni mpya kwenye biashara ya vifaa vya ujenzi au hardware, hizi ndiyo baadhi ya mitaa muhimu ya kuifahamu:

📍 Narung'ombe – Maarufu kwa vifaa vya umeme.

📍 Mchikichini & Gogo – Utapata aina mbalimbali za vifaa vya ujenzi.

📍 Sikukuu & Kipata – Moja ya maeneo makubwa ya biashara ya vifaa vya ujenzi.

📍 Lindi & Sikukuu – Chaguo zuri kwa vifaa mbalimbali vya ujenzi.

📍 Swahili & Kiungani – Maarufu kwa vifaa vya mabomba (plumbing) pamoja na vifaa vya ujenzi.

📍 Lindi & Livingstone – Utapata suppliers wengi wa vifaa vya ujenzi.

📍 Sikukuu & Omary Londo – Eneo lingine lenye maduka mengi ya vifaa vya ujenzi.

📍 Lindi & Nyamwezi – Sehemu nzuri ya kutafuta bidhaa mbalimbali za hardware.

📍 Mitaa ya Gerezani – Usiipuuze, kuna wauzaji wengi wa bidhaa mbalimbali kwa bei za ushindani.

Kariakoo imenifundisha kwamba biashara si mtaji pekee, bali ni kujua taarifa sahihi, kujenga mahusiano, na kuelewa soko.

Kama una ndoto ya kuingia kwenye biashara ya hardware, anza kwa kuifahamu Kariakoo kabla hata hujaanza kutafuta mtaji mkubwa.

Je, ni mtaa gani wa Kariakoo umewahi kukuletea deal kubwa au kukufundisha kitu muhimu? Tuambiane kwenye comment
 
WAHI SASA KABLA BEI HAIJAPANDA, USICHELEWE KUWEKA ODA YAKO

1. ✅ Banner 10,000 / meter
2. ✅ Stika 9000 / meter
3. ✅ Vitabu vya risiti 4000 Tsh size A6
4. ✅ Business cards pc100 Tsh 20,000 tu
5. ✅ Tshirt Tsh 2500 kuanzia pc10
6. ✅ Bango ya 3D Tsh 450,000 Tsh / meter
7. ✅ Rollup banner 120,000 Tsh
8. ✅ Kitambulisho ngumu 4000 Tsh
9. ✅ Vipeperushi pc100 size A6 Tsh 20,000
10. ✅ Kikombe Tsh 8000

Tunapatikana Nyamwezi na Muhoro
📲0675-545-795
 
Nataka nifanye hii biashara tena dodoma God bless hustler wote
Mkuu ni biashara inayolipa sana ,muhimu wekeza zaidi kwenye kujua product na sehemu zinapopatikana, hii biashara ukishaweza kuwa na taarifa za kutosha, mananikio yako hayako mbali
 
Mkuu ni biashara inayolipa sana ,muhimu wekeza zaidi kwenye kujua product na sehemu zinapopatikana, hii biashara ukishaweza kuwa na taarifa za kutosha, mananikio yako hayako mbali
True hii thread yako imeniongezea kitu mimi namiliki taasisi ya construction sema kwa sasa hailipi
 
True hii thread yako imeniongezea kitu mimi namiliki taasisi ya construction sema kwa sasa hailipi
Ni kweli kabisa. Zamani contractor alikuwa anapata faida kwenye vitu viwili; labor na materials. Ukipewa tender ulikuwa una-quote package nzima, hivyo margin ya materials ilikuwa sehemu kubwa ya profit.

Siku hizi hali imebadilika. Wateja wengi, hasa kampuni za construction, wananunua materials wenyewe moja kwa moja kwa supplier ili kupunguza gharama. Contractor unabaki una-quote labor pekee, ambayo margin yake ni ndogo na ushindani wake ni mkubwa.

Mitandao na upatikanaji wa taarifa umeongeza uwazi wa bei za materials, hivyo ile nafasi ya kuongeza margin kama zamani imepungua sana.

Kwa sasa, ukitaka construction company ikuletee faida nzuri, ni muhimu uwe na biashara nyingine inayoi-support, kama hardware. Ukiweza hata kuagiza materials moja kwa moja kutoka China, unakuwa na advantage kubwa. Ikitokea tender inayohitaji u-quote materials na labor kwa pamoja, unaweza kutoa bei ya ushindani lakini bado ukapata faida kubwa kupitia margin ya materials. Walioliona hili mapema ndiyo wanaonekana kufanya vizuri zaidi kwenye soko la sasa.
 
Naam
 
Mkuu kariakoo kwa ujumla ukiweza kui study kuna fursa nyingi mnoo,
Tatizo wengi tunaangukia katika mikono ya wachoyo wa taarifa hivyo mikwamo inakuwa mingi sana. Chimbo la kugusa na kutembea ukiwa na watu sahihi na mtaji anzilishi.

Watu wema bado wapo, tutafikia mafanikio na sisi iwe ya kati au juu zaidi.
 
Mkuu ni biashara inayolipa sana ,muhimu wekeza zaidi kwenye kujua product na sehemu zinapopatikana, hii biashara ukishaweza kuwa na taarifa za kutosha, mananikio yako hayako mbali
Mkuu kwa duka la kueleweka mtaji uwe kiasi gani?
 
Msimbazi na mchikichini urembo wa wadada Leo hii naagiza kamzigo sio kingi ila mdogomdogo kutoka China Kuna watu wanaroho nzur za kusaidia wengine inshallah Mungu azid kuwaongezea
Hivi mkuu kwa mtazamo wako na uzoefu wako kati ya biashara ya urembo na biashara ya vipodozi ipi yenye faida kubwa ?
 
Back
Top Bottom