Kapuya; Nihurumieni jamani

Kapuya; Nihurumieni jamani

WAKATI serikali ikisuasua kumfungulia mashitaka waziri wa zamani wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Juma Kapuya, kwa tuhuma za kubaka na kutishia kumuua mwanafunzi wa sekondari, kiongozi huyo amempigia magoti mshitaki wake akiomba yaishe. Hatua hiyo mpya ya Kapuya inakuja siku chache baada ya kukanusha kutomfahamu binti huyo, huku akidai kwamba namba ya simu inayotumika kufanya mawasiliano na mlalamikaji alikwishaigawa, jana mbunge huyo wa CCM alituma ujumbe mzito akisihi wamalize tatizo hilo kwa majadiliano.
Akitumia namba ileile 0784993039, ambayo awali aliikana, lakini akaitumia juzi Jumamosi katika taarifa yake ya kukanusha tuhuma hizo kwa vyombo vya habari, Kapuya alimwomba binti huyo wakutane ofisini kwa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP) na huko aseme kuwa hana haja na kesi.
Katika ujumbe uliotumwa kwa binti huyo kupitia namba hiyo, Kapuya amemwahidi msichana huyo kumpa pesa na aende popote nje ya nchi, hivyo kumfanya abaki huru.
Huku akiendeleza vitisho vya kuwaua ikiwa binti huyo hatakubali, katika moja ya ujumbe wake, Kapuya alisema: “Najua kesi ni watu wawili, sasa kwanini hamkubali? Hivi hela nitakayompa mtu akuue si bora nikupe uanze maisha?
“Wakili nimempa hela nyingi, magazeti pia nimewapa, naumia jamani, unaweza kukanusha taarifa hii na kufuta ushahidi halafu mimi nikupe hela uende popote, bungeni sifiki na nitafukuzwa, nyie mtapata nini?
“Nakupa masaa mpaka saa sita nitakuwa nimeshatuma hela, unachukua passport unasepa na hakuna kurudi, ukikaidi roho itakwenda kupumzika, unataka kufa kibudu? Jiangalie.
“Ukienda kwa DPP mwambie kuwa hutaki kesi, mimi niitwe, usipokubali nitakuua, yaani siku si nyingi, na hakuna wa kunifanya lolote, umeshasikia vifo vingapi, unataka kufa wakati huu au kwa ahadi ya Mungu?” alimwandikia ujumbe binti huyo.
Kapuya alizidi kumbembeleza binti huyo akimwomba afikirie namna alivyowasaidia kiasi cha kuwapa gari aina ya Benz, na kwamba hata kama amemwambukiza ukimwi, lakini atambue kuwa maisha hayana spea.
“Sikiliza nawaambieni, kwanini mnatumiwa, maana yake ni kuwa hao watu wa haki za binadamu hawawezi kuwapa hela…hebu tafakari nimetoa Benz, nimekupa ukimwi sawa, maisha hayana spea, mimi nitafungwa, wewe utapata nini? Mimi nina miaka 69 hata nikifa leo, nakubali kwenda popote hata kwa DPP tukae meza moja, najua nitafungwa tu.”
Kwa mujibu wa mawasiliano yaliyonaswa na Tanzania Daima Jumatano, Kapuya hata hivyo ameendelea kutishia kumtoa roho binti huyo hasa baada ya kuona ushauri wake unagonga mwamba.
Moja ya ujumbe uliotumwa kutoka katika namba hiyo unasomeka hivi: “Nitakuua tu huwezi kukimbia milele, si hutaki kunisikiliza, kwani kesi ya Mahita ilikuwaje? Mbona anahudumia na hakuna wa kumfanya lolote, kuwa kimya uone, hujachelewa, kama hutaki lazima mimi na Hamis tukuue.”
Hata hivyo, pamoja na ushahidi wa waziwazi, katika hali ya kushangaza Jeshi la Polisi limeendelea kushikilia msimamo wake wa kutofungua mashitaka ama hata jalada la uchunguzi dhidi ya Kapuya, kwa madai kwamba lilikuwa likisubiri mlalamikaji afungue kesi.
Juzi akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Seleman Kova, alidai kuwa hawawezi kufungua mashitaka bila ya kuwapo mlalamikaji na kwamba watalifanyia kazi suala hilo pindi binti huyo akifungua jalada.
Hata hivyo wakati Kova akisema hayo, jeshi hilo limewahi kufungua kesi na kuwakamata watuhumiwa kutokana na taarifa zilizoripotiwa na magazeti na mitandao ya kijamii.
Jeshi la Polisi liliharakisha na kumkamata kiongozi wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare na kumsafirisha chini ya ulinzi mkali kwa tuhuma za ugaidi na kutishia kuua baada ya kuona picha yake kwenye mtandao wa YOUTUBE.
Aidha, katika tukio jingine, Jeshi la Polisi lilimkamata na kumhoji Evod Justinian, kisha kumfungulia mashitaka baada ya kukaririwa na vyombo vya habari akimwita Mwigulu Nchemba gaidi, bila mlalamikaji kuandikisha maelezo polisi.
Katika tukio linalomkabili Kapuya, uchunguzi umebaini kuwa, binti huyo na dada yake ambaye amekuwa akimsimamia mdogo wake kupata haki, walifikisha suala hilo katika mamlaka za nchi ikiwemo Ofisi ya Bunge.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinasema kuwa msichana anayedai kufanyiwa kitendo hicho alikuwapo Dodoma bungeni, wakati wa Bunge la Kumi, Mkutano wa Kumi na Tatu na alipewa huduma za usafiri na malazi kutoka kwenye Ofisi ya Bunge.
Habari zinasema msichana huyo pamoja na dada yake waliitwa kujadili suala hilo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge chini ya uenyekiti wa Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi, lakini Kapuya hakutokea.
Imedaiwa kuwa kwa kipindi cha wiki mbili jitihada za kuwakutanisha Kapuya na mabinti hao kujadili suala hilo zilikwama, hali iliyosababisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Mwigulu Nchemba, kuingilia kati kuwashauri waende Dar es Salaam kuonana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula.
Emmanuel Mpanda, anayedaiwa kuwa msaidizi wa Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila, ndiye anatajwa kuweka utaratibu wa gharama za kuishi na kulala kwa wasichana hao kwa kipindi cha wiki mbili walipokuwa Dodoma, na utaratibu wa kuwapa gari kwa gharama za Bunge lililowasafirisha hadi Dar es Salaam.
Haijafahamika sababu za Kapuya kushindwa kufika mbele ya kamati hiyo ili kama anasingiziwa ukweli uwekwe wazi.
Aidha, Kapuya hadi sasa ameshindwa kukanusha kuitwa na kamati hiyo ya Bunge, badala yake amezidisha vitisho kwa binti huyo na dada yake, na hata kutishia kulifungulia mashitaka gazeti hili na mitandao mingine ya kijamii iliyoandika tuhuma zake.
Hata hivyo wakati polisi wakishikwa na kigugumiza na kuwasaidia wasichana hao kupata ulinzi, uchunguzi umebaini kuwa ushahidi wa meseji zilizotoka katika namba ya Kapuya unatosha kabisa kumfungulia kiongozi huyo mashitaka.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu katika Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), alisema sheria inaruhusu vyombo vya dola kumfungulia mashitaka mtu yeyote anayetumia namba ya simu kutishia maisha ya mwingine.
Tanzania Daima Jumatano mara kadhaa limekuwa likimpigia simu Kapuya ambaye amekuwa hapokei simu, lakini amekuwa akimpigia binti huyo kila wakati akimshauri wasiendeleze jambo hili, na wakati huo huo akimtisha yeye na dada yake ikiwa watazidi kugoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Brigedia Jenerali Ngwililizi, alipotafutwa kueleza namna walivyolimaliza suala hili bungeni hakuweza kupatikana.
Aidha, simu ya Katibu wa Bunge, Kashilila, ilikuwa inaita bila kupokewa.
Siku tatu zilizopita gazeti hili liliwasiliana na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, kumuuliza kuhusu ufahamu wake juu ya suala hili, kwanza alimwambia mwandishi wa gazeti hili kuwa hilo suala ni ‘complicated’ na kwamba: “Hilo ni suala la mtu binafsi siwezi kulisemea mimi.”

  • inShare​

haya sasa, mabo yanazidi kukorogeka...kumbe mabinti waliwekwa dodoma kwa gharama za bunge? kwanini Bi kiroboto asiunganishwe katika kesi hii kwa kutumia fedha za umma kinyume cha sheria?
 
haya sasa mahakamani tena..huko ndo kwenyewe
 
dah tz daima kama kabakwa mbowe wanavyoshupalia
 

Kapuya kama kweli unaoutu Watanzania wanao utu zaidi wapo tayari kukusamehe na mambo yakaendelea kama kawaida.
Ushauri wangu ni huu, itisha mkutano na vyombo vya habari pale Habari na Maelezo, usijitetee bali omba msamaha kwamba kweli ulikiuka MAADILI YA UONGOZI hivyo ungependa WATANZANIA WAKUSAMEHE. Huwezi amini utasamehewa hapo hapo, hakuna atakaye kuwa na dharau kwako kuanzia pale MAELEZO.
Believe me!

Bubu dada, hapa ninakupa A+++

Cheers.
 
kwa hali halisi ilivo kwa sasa,mtu mwenye akili timam na uelewa wa kufikiri kwa kina atagundua kuna mchezo hapa.hakuna sms ya kapuya wala nn hapo I.T imetumika kufanya namba ionekane n ya kapuya .nawapa siku 6ukwel utajulikana na mtaona nn kinaendelea na nani ni wahusika wa kumchafua huyu babu.

ni kwel kabisa kwamba alikimega kila kidada poli,lakin hii sms ina iliootoka
 
Kapuya kashikwa Pumbu zote mbili, safari hii atajinasua itakuwa kwa msaada wa uonevu na udharimu wa serikali ya CCM vinginevyo pumbu zake zote mbili ni mali yetu.
 
Tanzania Daima limeshuka heshima san kwa kushadadia mambo ya kipuuz kama haya,

Yan katika mambo yote ya umuhimu wao wakaona hii ni yenye tija kuwaandikia watanzania??

Hovyo sana
 
Sasa huyu alhaji kama anaamini kuwa jina lake linachafuliwa ni kwa nini asiwahi mahakamani?

DSC_8159.JPG

Muzeeehe.. Purofesaee omba msamaha faster, yaishe, achia ubunge wao, jipange upya kimaisha.. Unapozidi kukaidi Walah..! Hawa watu wanazidi kutuporomoshea mipicha kede kede wanasema ya "X" wataanza hivi punde kuileta uraiani.. Patakuwa padogo..! Nsikilizie..!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom