Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Hapa mkuu umepigilia msumari. Hawa wanapofungua vinywa kutamka haya wajue japo tunakubaliana nao kwa asilimia kubwa lakini lazima upande wa pili wa shilingi tuuangalie. Walioivamia siasa nao waachie ngazi au sio?Vile vile kwa wanasiasa na viongozi au huko si lazima?? tuwe na viongozi waliosomea uongozi na kuwa na wanasiasa waliosomea siasa.
Mbavu sina mwenzio. Hii logic umeleta iko interesting japo ina ujumbe mkubwa tu. Kudos bro!1984 inaanza pole pole,
Kwanza watasema wasomee, halafu watasema wawe wanachama wa guild lao, halafu watasema guild lazima lipitishwe na NEC, halafu watasema lazima wawe na kadi za CCM, halafu watasema lazima waonyeshe shahada ya kura na ushahidi kuwa walimpigia kura mgombea wa CCM wa urais na ubunge... there is no stopping this.
Mwandishi wa habari lazima asomee, asomee nini sasa? Uandishi? Ina maana mtu mwenye PhD ya Philosophy hawezi kuwa mwandishi under that system? Kigezo cha kusoma kitakuwa nini?
Uandishi zaidi ya kuwa taaluma, ni kipaji na sanaa.Kuna watu hawajaenda shule lakini wanaandika vizuri kuliko waliosomea and vice versa.Sasa kwa nini kuweka mtego wa panya utakaowapata wanaotakiwa na wasiotakiwa?
Kama issue ni kukabili quality mbaya ya uandishi tuwa judge watu kwa kazi zao, siyo kwa ma shahada na ma stashahada ambayo hata Waziri wetu wa fedha kanunua Almeida.
Pundit, it is about control. Sasa hivi hawana control ya waandishi wa habari. Watakaposema wawe digrii, na ukakutwa unafanya kazi ya uandishi wa habari wakati hauna digrii ya uandishi wa habari si watakufuta kama wanavyofanyiwa wahandisi au madaktari?
Lengo kubwa siyo ubora wa waandishi bali uwezo wa serikali kuweza kuwacontrol.
Pundit, it is about control. Sasa hivi hawana control ya waandishi wa habari. Watakaposema wawe digrii, na ukakutwa unafanya kazi ya uandishi wa habari wakati hauna digrii ya uandishi wa habari si watakufuta kama wanavyofanyiwa wahandisi au madaktari?
Lengo kubwa siyo ubora wa waandishi bali uwezo wa serikali kuweza kuwacontrol.
Hivi Tom Brokaw alisomea nini?
Tim Russert alisomea nini?
Katie Couric alisomea nini?
Tim Russert alikuwa lawyer.
Kuhani,Peter Jennings alikuwa nani na alisoma nini? Kama alisoma at all!
Hivi Tom Brokaw alisomea nini?
Tim Russert alisomea nini?
Katie Couric alisomea nini?
Nadhani kinachotakiwa hapa ni kwamba wawe na elimu ya kiwango fulani inayowasaidia kuchambua mambo ya kuandika au kutangaza, siyo lazima elimu hiyo iwe ni katika Journalism tu. Sehemu nyingi duniani wanahabari maarufu hawakuosema journalism lakini wana taaluma fulani inayohusiana na aina ya journalism wanaofanya.
Watangazaji maarufu kule CNN hawana digrii za journalism lakini wana digrii zinazoendana na utangazaji wao: Dr. Sanjay Gupta ana M.D. (hivyo hutangaza mambo ya afya na tiba), Wolf Blitzer an M.A. katika international relations (na hupenda kutangaza habari za namna hiyo) , Lou Dobbs an M.A ya Economics (utangazaji wake unaendana na taaluma hiyo), Bill Schneider ana Ph.D ya political Science (hutangaza mambo ya siasa tu), Fareed Zakaria ana Ph.D ya international relations (hufanya inteviews zinazohusu mambo ya kimataifa).
Wote hao uliowataja walikuwa na digrii zinazoendana na utangazaji wao. Tom Brokaw ana digrii ya Political Science (kabla ya kuwa mtangazaji mkuu wa habari alikuwa akishughulika na habari za kisiasa), Tim Russert alikuwa na Juris Doctor (hivyo alikuwa akifanya interviews za kisiasa kwa mtindo wa cross-examination), na Katie Couric ana digrii ya American Studies (naye kabla ya kupanga ngazi alianza kama mtangazi wa mambo ya mitaani huko Miami).