Kapt. Mkuchika na Maagizo yake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kapt. Mkuchika na Maagizo yake!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 28, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 28, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mhe. George Mkuchika amesema kuwa ni lazima kwa waandishi wa habari wa Tanzania kuwa ni wale waliosomea fani hiyo, kwani fani hiyo ni kama fani nyingine muhimu. Amesisitiza kuwa hata sheria mpya ya uhuru wa habari itazingatia jambo hilo. Ameyasema hayo leo katika hotuba yake ya makadirio ya bajeti yake ya mwaka huu. Bunge limepitisha bajeti ya wizara hiyo.
   
  Last edited by a moderator: Aug 4, 2008
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,586
  Likes Received: 1,955
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kuna pengo kubwa kabisa la uandishi wa habari.
  Yani pess imevamiwa hakuna professionalism...Ni vurugu tupu na inachosha...No wonder wabongo hupenda habari za UDAKU maana hizo za kikweli hazi make sense kabisa.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,'
  Waziri ametoa pendekezo gani kuwasaidia waandishi habari waliopo wanoe ujuzi wao?
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Jul 28, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Hivi Tom Brokaw alisomea nini?
  Tim Russert alisomea nini?
  Katie Couric alisomea nini?
   
 5. W

  WembeMkali JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2008
  Joined: Jun 16, 2007
  Messages: 282
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vile vile kwa wanasiasa na viongozi au huko si lazima?? tuwe na viongozi waliosomea uongozi na kuwa na wanasiasa waliosomea siasa.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jul 28, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wembemkali... umenipa subject ya this week!!! great!!!!
   
 7. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #7
  Jul 28, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Hapa mkuu umepigilia msumari. Hawa wanapofungua vinywa kutamka haya wajue japo tunakubaliana nao kwa asilimia kubwa lakini lazima upande wa pili wa shilingi tuuangalie. Walioivamia siasa nao waachie ngazi au sio?
   
 8. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2008
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Mimi sijawahi kuona wabunge wanakaa na wanaongea mambo ya ajabu namna hii!

  Yaani waziri anasema wazi kwamba ni lazima waandishi wawe wamesomea fani hio.

  Hatukatai, ni lazima upate utaalam lakini pia unaweza kuwa na shahada yako ya uhandisi barabara na ukachukua Post Graduate ya Journalism.

  Lakini waziri anasahau kwamba journalism ime-evolve sana kiasi kwamba kuna tofauti kubwa sana kati ya reporter, journalist na correspondent.

  Kwa mfano kuna correspondents ambao ni madaktari, wahasibu na hata wanasiasa achilia mbali wale special correspondents ambao hushughulikia habari nyeti na nzito.

  Sasa kama inatakiwa kila fani iwe na watu walifuzu kufanya kazi hio na tuanze na wanasiasa na tujue walipata wapi sifa za kuitwa wanasiasa.

  Inakuwaje mtu anafanya biashara na leo hii anaruhusiwa kugombea ubunge na sifa ya kuwa mwanasiasa hana hata chembe?

  Waziri asijaribu kufanya spinning mchana kweupe.
   
 9. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  1984 inaanza pole pole,

  Kwanza watasema wasomee, halafu watasema wawe wanachama wa guild lao, halafu watasema guild lazima lipitishwe na NEC, halafu watasema lazima wawe na kadi za CCM, halafu watasema lazima waonyeshe shahada ya kura na ushahidi kuwa walimpigia kura mgombea wa CCM wa urais na ubunge... there is no stopping this.

  Mwandishi wa habari lazima asomee, asomee nini sasa? Uandishi? Ina maana mtu mwenye PhD ya Philosophy hawezi kuwa mwandishi under that system? Kigezo cha kusoma kitakuwa nini?

  Uandishi zaidi ya kuwa taaluma, ni kipaji na sanaa.Kuna watu hawajaenda shule lakini wanaandika vizuri kuliko waliosomea and vice versa.Sasa kwa nini kuweka mtego wa panya utakaowapata wanaotakiwa na wasiotakiwa?

  Kama issue ni kukabili quality mbaya ya uandishi tuwa judge watu kwa kazi zao, siyo kwa ma shahada na ma stashahada ambayo hata Waziri wetu wa fedha kanunua Almeida.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jul 28, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Pundit, it is about control. Sasa hivi hawana control ya waandishi wa habari. Watakaposema wawe digrii, na ukakutwa unafanya kazi ya uandishi wa habari wakati hauna digrii ya uandishi wa habari si watakufuta kama wanavyofanyiwa wahandisi au madaktari?

  Lengo kubwa siyo ubora wa waandishi bali uwezo wa serikali kuweza kuwacontrol.
   
 11. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #11
  Jul 28, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Wasomee nini sasa?
   
 12. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #12
  Jul 28, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Mbavu sina mwenzio. Hii logic umeleta iko interesting japo ina ujumbe mkubwa tu. Kudos bro!
   
 13. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Jinsi waandishi nao walivyokuwa watupu wataukodolea macho huu muswada mpaka utapitishwa.

  Badala ya kuu lambast huu muswada bizarre wataogopa ku sound kama wanatetea vilaza ambao hawajaenda shule.

  Watch!
   
 14. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  I know that, that is why I associate this with totaliatarianism, disguised under the cloth of journalistic standards.

  Mwalimu Nyerere alitafsiri "Merchants of Venice" cha Shakespeare, na kuandika vitabu viingi sana vya ujamaa na kilimo and what not.

  Alisomea uandishi?

  Hivi wanajua percent ya waandishi waliosomea uandishi dunia nzima? Hivi Carl Sagan alisome uandishi? Professor Hawkins alisomea uandishi? Mark Twain alisomea uandishi? Charles Dickens alisomea uandishi?George Bernard Shaw (the only person to have been awarded both the Nobel Prize for Literature (1925) and an Oscar (1938) ) alisomea uandishi? Mohandas Gandhi alisomea uandishi?

  Gimme a break now!
   
 15. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2008
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Ndio pale sasa watakapoona kwamba waandishi ambao ni (special correspondents) ni wale ambao wana upeo na nyenzo ambazo ni vigumu kuzi-control.

  Hayo unayosema yamefanyika nchini Burma na Zimbabwe lakini pamoja na yote waandishi (special correspondents) wameweza kuingia na kutoka na habari nzuri tu ambazo hazijachujwa na pia wale waliomo ndani ya nchi hio wameweza kupiga hata picha kwa kutumia mobile phones na kutumia mtandao wa internet kufikisha habari kwenye umma wa dunia.

  Haitawezekana ku-control waandishi wa habari na hii kwa Tanzania hio wizara kama itachukua hatua hio hio naona itakuwa ni "suicidal mission".

  NB:

  Nizungumzia sana special correspondents kwasababu kwa style ya upashaji habari katika mataifa yetu kwa sasa, waandishi inabidi wawe na ujuzi wa kitaalam zaidi hasa kiteknolojia.
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Jul 29, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nyani,
  Tim Russert alikuwa lawyer. Alianza kazi kama mshauri wa mbunge mmoja Capitol Hill. Tim Russert sijui na Katie kasomea TV journalism. Anyway, acha uvivu na wa-google mwenyewe:-
   
 17. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #17
  Jul 29, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Peter Jennings alikuwa nani na alisoma nini? Kama alisoma at all!
   
 18. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #18
  Jul 29, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kuhani,
  Uandishi na utangazaji ni kipawa. Jennings nasikia alikuwa high school graduate. And he was one of the best.
   
 19. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #19
  Jul 29, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280

  Nadhani kinachotakiwa hapa ni kwamba wawe na elimu ya kiwango fulani inayowasaidia kuchambua mambo ya kuandika au kutangaza, siyo lazima elimu hiyo iwe ni katika Journalism tu. Sehemu nyingi duniani wanahabari maarufu hawakuosema journalism lakini wana taaluma fulani inayohusiana na aina ya journalism wanaofanya.

  Watangazaji maarufu kule CNN hawana digrii za journalism lakini wana digrii zinazoendana na utangazaji wao: Dr. Sanjay Gupta ana M.D. (hivyo hutangaza mambo ya afya na tiba), Wolf Blitzer an M.A. katika international relations (na hupenda kutangaza habari za namna hiyo) , Lou Dobbs an M.A ya Economics (utangazaji wake unaendana na taaluma hiyo), Bill Schneider ana Ph.D ya political Science (hutangaza mambo ya siasa tu), Fareed Zakaria ana Ph.D ya international relations (hufanya inteviews zinazohusu mambo ya kimataifa).


  Wote hao uliowataja walikuwa na digrii zinazoendana na utangazaji wao. Tom Brokaw ana digrii ya Political Science (kabla ya kuwa mtangazaji mkuu wa habari alikuwa akishughulika na habari za kisiasa), Tim Russert alikuwa na Juris Doctor (hivyo alikuwa akifanya interviews za kisiasa kwa mtindo wa cross-examination), na Katie Couric ana digrii ya American Studies (naye kabla ya kupanga ngazi alianza kama mtangazi wa mambo ya mitaani huko Miami).
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Jul 29, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Sasa huyu bwana yeye si inadaiwa kasema waandishi wa habari wasomee uandishi wa habari? it's kinda dumb if you ask me....kwa sababu sidhani kama wote hawa wana bachelor's au Master's za journalism (print au electronic media) au communications au broadcasting.....
   
Loading...