Kapt. Mkuchika na Maagizo yake!

...wamkumbushe nchi inaongozwa kwa sheria sio amri za watu tuu kwa sababu ni mawaziri au wenye cheo,na akumbuke hakuna sheria kama hiyo!
 
Date::8/4/2008
Waziri apiga marufuku wimbo wa taifa katika simu
Na Clara Alphonce
Mwananchi

WAZIRI wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika amepiga marufuku wananchi kuweka wimbo wa taifa katika simu zao za mkononi.

...dah! kaazi kweli kweli, itabidi nibadilishe ringtone to Nkosi sikelel'iafrika!

:(
 
Huyu anafaa alaniwe ni adui wa Taifa hili la Tanzania , hata sijui kama linafahamu kuwa nchi imevamiwa na mafisadi ? Kama kuna mawaziri wanapuliza basi huyu ni mmojawao yaani mambo ya kiCCM kukurupuka tu,yule mmoja kaulizwa kasema Zanzibar si nchi Nyerere na ujuaji wake wote hajawahi kutamka hivyo ,eti katiba ,hivi Katiba inasema nini juu ya watu wa dizaini ya mafisadi WaTz tunataka muheshimiwa Pinda atamke na ailinde katiba kama kweli anafuata na kuyaheshimu yalio ndani ya Katiba.
halafu huyu waziri aliesema mambo ya wimbo ivi ana akili timamu huyu ,au ndio wanaosaboteji utawala wa Mh.Kikwete kwa kuzusha mambo ambayo yataleta na kuonyesha kama serikali imejaa mambumbu na hivyo moja kwa moja kumlengesha Mheshimiwa Kikwete ,inawezekana kabisa haya ni mambo ya mtandano unaokwenda agaist our Leaders who are trying to their best to keep the country on the track again ,wanafanya kila mbinu alimradi kuharibu ,huyu ni Waziri katika Serikali anakwenda kusema upuuzi kama huu,kama sio saboteji ni kitu gani ? Kitu kidogo tu kinaweza kuivuruga akili ya watu kwa serikali yao na kuiona haina maana,na ndivyo wanavyofanya ,wanachokonoa mambo hayana hata maana , raisi anafaa kuwaangalia watu kama hawa na kuwatenga ikibidi awaondoe mara moja wakatafute shamba walime.
Hata watu wa dini hawajakataza mamboya dini kuwekewa kwenye mobile phones ,ila linazuka jitu hili ambalo eti ana wazifa wa Uwaziri anakwenda kuonya na kutoa tahazari wimbo wa Taifa ni marufuku kuwekwa kwenye phones,eti inawezekana simu ikaita na mziki huo ukawa unaimbwa na simu hiyo sehemu isiyokuwa tohara,hiyo ndio maana yake huwezi kuleta maana nyingine zaidi ya hiyo ,pengine mtu huyu ukimpa filimbi aupige wimbo wa Taifa hawezi atabakia kurusha mate tu ?
Halafu eti amekuwa mtetezi wa kufika kutamka aliyotamka kama si fisadi huyu ni nani ,wanasaboteji na kuipa serikali wakati mgumu sana kwa mambo ya kipuuzi puuzi kama haya,sasa watu baada ya kujadili maendeleo anajadili mambo ambayo hayana kichwa wala miguu ,hiyo wizara yake imeoza inatafuna fedha kwa kuwalipa makocha wa kigeni na hakuna kinachoonekana si ajabu kama mgao mwengine unaingia mfukoni,watu wanaojipendekeza kiaina ni hatari kwa uchumi wa Taifa.
 
Tatizo Watanzania hatuna utamaduni wa kuonyesha uzalendo wetu....sasa mijitu kama hili li Mkuchika inakuwa inapata culture shock ya aina fulani hivi inapoona vijana au watu tu kwa ujumla wanapoanza kuwa patriotic na ku display patriotism kwa njia mbalimbali kwa kutumia teknolojia. Sasa sijui jitu kama hili likiona bikini za bendera ya Tanzania zinauzwa madukani si linaweza likazimia kabisa.....Lol

na kwa kuongezea tu Nyani... watu wanapoanza kutukuza vya wengine kama mbadala..kama kuvaa bendera za marekani..kuvaa t-shirt zimeandikwa "I love UK, USA" etc wanasemwa hawana uzalendo..jamani!
 
Tanzania inatakiwa iongozwe kwa sheria na si amri ya Waziri, Mkuu wa Mkoa au nani.
wazee wengineo nao, mie nilifikiri unapoongeza na busara zinaongezeka.
Naamini aliposema kuwa Tanzania inahitaji journalists waliosomea journalism alisahau kusema Tanzania inahitaji Mawaziri waliosomea leadership pamoja na sheria.

Utagundua kitu kimoja kwenye tamko hili na lile la majuzi kuhusu waandishi. Mara zote Waziri anasema Serikali inaandika sheria za hayo matamko yake na yanakuja kuwa affective by law. Kuna kitu hapa kibovu vibaya mno: huwa serikali ikishaandika miswada basi cha mbele. Bunge linaipiga muhuri tu, a rubber stamp parliament.

Waziri hatakiwi kuwa na confidence eti tunaleta sheria. Hajui kama itapita. Lakini Bunge ndio the weakest link hapa. Sio tu kwamba wabunge hawaandiki za kwao, ila chochote kinachoandikwa na serikali cha mbele. Hivi sivyo mfumo unavyotakiwa kuwa. Tunahitaji wabunge wa upinzani zaidi. Lakini cha kusikitisha ni kwamba hata wapinzani nao hizi ndio zao. Zitto (Mb.) nae akaharibu wakati wa bajeti alipomwambia Mkullo kwamba angetegemea afute misamaha ya kodi. Sasa, why in the heck are you waiting for, or asking, Mkullo to write good laws ? That's your paid job, Mr. Legislator!
 
aroo, hiri rikapteni ripereke hiro rihabari kure kambini.....risituretee mauza uza....damn!
 
Sijui huyu jamaa anajua hata kutumia intaneti....kama anajua I hope huwa anapitia na kusoma hii foramu maana akisoma mada hii atajisikia "funny feeling"....
 
Sijui huyu jamaa anajua hata kutumia intaneti....kama anajua I hope huwa anapitia na kusoma hii foramu maana akisoma mada hii atajisikia "funny feeling"....

...u got it right,huyu na babu yako makopo MCbush wote hawajui internet ni nini!
 
Back
Top Bottom