Mpina alikuwa sahihi alivyomshutumu Waziri Mkuu kupuuzwa maagizo yake

juma30

Senior Member
Jun 25, 2022
149
421
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa amejiridhisha na Mchango wa Mbunge wa Kisesa Mhe. Luhaga Mpina kuhusu maelekezo ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kutofanyiwa kazi na watendaji wa jeshi la Hifadhi

Dkt. Tulia amesema hayo leo June 28,2023 Bunge,Dkt. Tulia amesema kuwa wakati Mhe. Mpina akichangia na maneno aliyokuwa ameyasema alikuwa sahihi kwa sababu maelekezo yale ya Waziri Mkuu yalikuwa hayajaanza kufanyiwa kazi

Dkt. Tulia amesema kuwa Mhe. Mpina alileta vielelezo vyake ofisini kama alivyotakiwa na baada ya kupitia waligundua kuwa alikuwa sahihi hivyo hilo jambo linamalizwa kwa namna hiyo.


 
Wapuuzi wanapiga makofi ya kujishtukia Kwa jinsi wanavyomuonea wivu Mpina 🤣🤣🤣!!.



Makamba ,Mwiguli, Endeleeni kuhangaika na uongo, Rais Ajaye, ni Rais mwenye Uwezo, sio upuuzi na ujanja ujanja .
 
kuna umuhimu mkubwa sana bunge lijalo lijae wapinzani. sijui wananchi watafunguka lini akili wajue hili. ccm mle ndani wanatuchezea sana akili
 
Leo nimesikia Waziri Mkuu akikemea Halmashauri kupora Ardhi haswa Dodoma

Tuone kama maagizo yatatekelezwa

Tuone Matuli Ndachi Mbwanga wananchi wenye hati watapewa maeneoyao yaliyo porwa na Jiji kwakusingizia uvamizi?
Kwanini hao Wavamizi wasibomolewe au wawalipe wenyehati halali?
Hao maafisa Ardhi walio shiriki wafilisiwe malizao mbona zinajulikana
 
Back
Top Bottom