Pundit
JF-Expert Member
- Feb 4, 2007
- 3,733
- 123
Waziri Mkuchika amesema kuwa, waandishi wa habari wa tz, wanatakiwa wawe wametathimiwa ili tupate waandishi wazuri, tusipate watu wasio na elimu ya uandishi wa habari. hii itapunguza kupata habari manung'ayembe. hili suala limezungumziwa sana na nchi ze jirani, kuwa tz hakuna waandishi wa habari.
Chukua mfano, MTU ANAEITWA JERI MURO wa ITV, yule jamaa hana hata akili ya uandishi wa habari, halafu ni mkorofi kishenzi. kuna siku nilimshuhudia akipigana na mgambo walipotaka kumchukulia kipazasauti na mikamera yao...ni mtu mwenye jazba sana mimi namshauri kama anataka kuendelea na uandishi wa habari, aende shule zaidi(tulisoma nae pale udsm).
ukikumbuka siku ile gorofa lilipodondoka kule mnazimmoja, utaona namna alivyokuwa anahoji yule injinia, huwezi amini kama ni mwandishi aliyeenda shule, becuase he does not ask maswali yenye point, anauliza vile yeye anavyofikiri ndivyo bila hata kutafuta uhakika wake. Tatizo,yeye kama mfano wa waandishi wengine, anahoji kwa kuhukumu kila mtu anaemkuta kwenye eneo bila kujua kama ni mhusika au la, matokeo yake anamwaibisha mtu asiyehusika. ndo maana utaona waliokamatwa na polisi ni wengine, yule ambaye JERI MURO alimtuhumu kama ni mzemba hakuhusika. mwisho, yule jamaa alipata jazba halafu akashindwa kumjibu vizuri, ....
Nilimsikia Jeri muro kwa masikio yangu akitamka maneno haya" Aloo, wewe usinijibu hivi, wananchi watakuua sasahivi ukifanya mchezo", kutokana na hilo, yaani kauli ya kichochezi kama hiyo, wananchi waliokuwa wamemzunguka pale, walianza kutaka kumvamia yule jamaa hadi polisi walipomchukua na kumweka kwenye gari yao kama vila wanamwokoa. lakini sio kwamba aliwekwa mle kwasababu alikuwa na kosa.
You are making my point kuwa mtu anaweza "kusoma" na asiwe muandishi mzuri, na "asiyesoma" akawa muandishi mzuri.
Sasa huyu bwana kasoma UDSM, pale ndipo sehemu inaposadikika kutoka "elimu darasa" ya juu kabisa Tanzania, sasa wewe unataka aende kusoma wapi tena? Kama hawa graduates wa UDSM wanakuwa primitive hivi huoni kwamba tatizo si elimu tu, bali hali nzima ya maisha yetu, utamaduni wa kusoma, kutaka kujua mambo, kutaka kuvumbua, kuchunguza unadani wa vitu na si kuchukua vitu juu juu tu kama vinavyoletwa, kuleta vitu vipya na kadhalika.Hivi ni vitu ambavyo havifundishiki darasani, inabidi mtu avifanyie kazi yeye mwenyewe.
Sasa kama na wewe msomi wa UDSM unaweza kuja na a self defeating argument bila kujijua, huku ukimnyooshea kidole mwenzako, this leaves a lot to be desired about the quality of education at the epitomy of our educational institutions, namely UDSM.
Mimi naamini kuwapeleka watu wengine UDSM ni kuwalemaza permanently, labda tukitia mkazo kwenye kuwa na maktaba nyingi zaidi katika kila kitingoji tunaweza kupalilia usomi bila hii monopoly mbaya ya stashahada na shahada za vyuo.