Kanusho la Dorothy Gwajima kuhusu kuzushiwa kusema Polepole alikuwa rafiki wa kweli linaongea mengi sana

Kanusho la Dorothy Gwajima kuhusu kuzushiwa kusema Polepole alikuwa rafiki wa kweli linaongea mengi sana

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
352
Reaction score
1,028
Kwanza kabisa sikubaliani na watu wanaosambaza uzushi wa aina yoyote ikiwemo kuwalisha watu maneno kwa njia yoyote ile, ila pia nadhani Gwajima alitakiwa kukanusha uzushi kwa maneno mafupi sana kuwa, Sijawahi kutoa kauli hiyo na pia si sahihi kusambaza taarifa za uzushi iwapo kulikuwa na ulazima sana wa kukemea poster hiyo.

Lakini alichokifanya hapo kwenye kanusho lake kinaongea kuwa kwanza alipaniki kuona kuwa kahusishwa na mtu ambaye ukihusishwa naye pengine nawe waweza kuwa hatarini iwapo utasema kuwa hakuwa mtu mbaya,

Majibu yake yanaonesha kupaniki, kukosa busara na mtu ambaye anaona kabisa kibarua chake kiko hatarini kama uhai na maisha yake, yanatoa jibu kuwa huenda aliyefanya Polepole asiwepo ni yule anayedhaniwa maana sio kwa hofu hiyo.

Hapa chini ni kanusho lake na baadhi ya majibu kwa waliochangia mada yake, yapo mengi sana

1774345148482.png

1774345195099.png

1774345084384.png

1774345565398.png

1774345620128.png

1774345273913.png

1774345351105.png

1774345387730.png

1774345490717.png


1774345823215.png

1774345852575.png
 
Ndugu wabaya wangu kokote mliko, nawasalimu.

Halafu nataka kusema hivi, naomba tusitengenezeane habari za uongo uongo kwa malengo binafsi. Kama ni habari inayonihusu mimi, naweza kuisema mwenyewe kwenye kurasa zangu zote.

Hivyo, habari hii kwenye picha na maneno yaliyokuwa yameandikwa chini yake na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ni ya kutengeneza yaani ni ya uongo, IPUUZWE, na nitashtaki Polisi ili, walioniwekea maneno haya mdomoni watafutwe kwa mujibu wa Sheria wakajibu uongo wao.

Na katika habari ya kutungiana maneno ya uongo, SITAKUBALI....... maana uongo ni ufitini na adui wa haki na UONGO HAUJAWAHI KUWA MTAJI WA MAENDELEO.

Tafadhali MNAONITHAMINI mkiona habari tata kuhusu mimi kokote iliko NILETEENI link nione ili nichukue hatua stahiki za kisheria.

@polisi.tanzania tafadhali naomba kuwasilisha kwa uchunguzi na kesho nitaripoti rasmi.

FB_IMG_1774344171799.jpg
 
Sina maneno mengi kuhusu huyu mama.

Ila nawakumbusha jambo moja tu kuhusu huyu mama.

Hivi mnakumbuka kipindi cha hayati JPM kuhusu suala la kutochanja chanjo ya corona badala yake tujifukize mnakumbukuka huyu mama alikuwa ni waziri na alishadadia sana hilo suala?

Mnakumbuka JPM alipofariki na huyu mama akabakia wizara hiyo hiyo na lilipokuja suala la kuchanja alilishadadia ili amfurahishe samia kana kwamba si yeye aliyekuwa akimuunga mkono JPM badala yake alimkataa vibaya sana?
 
Huyo ni kati ya watu wa hovyo tu.
Kwanza mropokaji na mpayukaji.
Kumpa muda hapa wa kumjadili hatujitendei haki.
Kinachomsaidia uongozi wake kidogo ni ile tabia ya ufuatiliaji matukio yanayo mpa 'trending' mengine sifuri kabisa. Inamfaa kazi ya social media content creator, public relations, na mengine ya muundo huo.
 
Back
Top Bottom