ni kawaida mtu aliyejitoa uhai huwa hafanyiwi ibada kanisani,ukijinyonga,unywe sumu au ujiue kwa namna yoyote ile sahau uwepo wa kasisi au kupelekwa kanisani
Sasa kanisa lina uthibitisho gani kama alijiua au aliuwawa wakati uchunguzi bado kukamilika!!? Huku ni kuchukua sheria mkononi!
Mbona sasa dadaangu unanichanganya. Umeisikia au umeisoma?Nimeisikia hii habari kwenye Nipashe leo
Mbona sasa dadaangu unanichanganya. Umeisikia au umeisoma?
Katoliki mtu akisadikiwa kujiua haombewi... wanataratibu ambazo haziangalii nani ni nani...hata JK juzi kwenye misa ya kumuombea Mwl Nyerere inasemekana hakuhudhuria kwa kuwa alitaka kuja na kiti chake kanisani akachomolewa....chezea katoliki wewe....lililowekwa limewekwa na kama hutaki unalala mbele
acha kujifariji wewe, biblia inasema baada ya kifo ni hukumu!! maombi au sala juu ya marehemu hayasaidii chochote zaidi ya kufariji wafiwa!!
Hakuna sababu ya msingi hapo au ndio mambo ya sadaka mnaweka kipaumbele sana mtu ameshakufa haku na mtu yoyote anaweza kumuhukumu binadamu mwezake!sasa nyinyi mnawaza sadaka tu nakupiga kelele usiku mzima
mi wakatoliki wananifurahisha wanapowaruhusu waumini wao kukamua pombe ili mradi tu uwe unasema wewe siyo mlevi ni mnywaji tu.