Kanisa la Kristo Morroco na Magomeni

Kanisa la Kristo Morroco na Magomeni

Mkuu nisha eleza mengi sana. halafu jibu lako la kwanza, linatofautiana na jibu lako la pili. Jibu lakwanza umesema nieleze tunavyo sali lkn jibu la pili hutaki kueleza imani uliyoishuhudia.

Anyway, kwa faida yako narudia kukupa ratiba ya wiki nzima, na imerudiwa sana. hii hapa mkuu

Ratiba ya ibada na vipindi vya kanisa, kwa wale walioko dsm, kanisa la Kristo Magomeni ratiba kwa wiki ni hii.

Magomeni CoC- Church of Christ

Ratiba ya Ibada zetu :
Jpili asbh saa tatu - sita mchana,

jioni saa kumi na moja mpaka saa kumi na mbili,

jtano saa kumi na moja mpaka saa kumi na mbili jioni. Mafundisho ya biblia(Bible school)

Karibuni tujifunze neno la Mungu kwa utukufu wake, hautojuta kujifunza neno, bali utajilaumu kwa kuchelewa.
Mkuu tusadie kama unajua mtu anaelijua hili la Morocco
 
Fika pale utapewa utaratibu wote
Nimeona mdau mmoja akiuliza kuhusu Kanisa la Silom na Mimi nikapata wazo la kuuliza kuhusu makanisa mawili niliyotaja hapo juu. Hivi haya makanisa yana waumini kweli maana sijawahi kuona watu wakiingia kuabudu wala kuona magari yamepaki nje pamoja na kuonekana kuwa ni makubwa sana.

Samahani kama nitakuwa nimemkwaza mtu
Kanisa la Kristo lililopo Magomeni ni tofauti na lile kanisa la Mormon - Morroco. Ratiba ya kanisa la Kristo Magomeni: Jpili saa 3 asubuhi na jioni saa 11. Pia Jtano saa 11 jioni. Ni mojawapo ya makusanyiko mengi yaliyopo duniani kote yenye kuamini mambo ya msingi yafuatayo: (1) Agano Jipya la Yesu Kristo ndio katiba pekee ya kuongoza vitendo vya Wakristo na ibada. Sawasawa na jinsi Yesu alivyowaagiza mitume wake kwamba walipaswa kuwafundisha injili mataifa yote na kushika yote aliyokuwa amewaagiza (Math. 28:18-20). Akiwakataza kuongeza au kupunguza ktk maagizo hayo (Ufu.22:18,19; taz. 1Kor.4:6; Gal.1:6-9). Maandiko yaliyotangulia kuandikwa (Agano la kale) yaliandikwa ili kutufundisha sisi (tunaoishi chini ya Agano Jipya) ili kwa faraja na saburi ya Maandiko tupate kuwa na matumaini (Warumi 15:4). Pia, tunajifunza ktk Agano la kale mifano ya jinsi Mungu alivyoshughulika na watu wema na wabaya hapo nyuma (1Kor.10:1-11).

2) Kanisa la Kristo linaamini kuwa Mwenye mamlaka yote duniani na mbinguni ni Kristo na wala si mwanadamu (Math.28:18). Hakuna nchi yenye maraisi wawili! (Kanisa limetajwa kuwa ni nchi 1Pet.1:15-16). Kanisa la Kristo halina makao makuu duniani. Kwani kanisa linaamini kwamba alipo mkuu wa kanisa, ambaye ni Kristo ndipo yalipo makao makuu. Kila kusanyiko ni "autonomous," linajitegemea kimaamuzi chini yaKristo bila kuingiliwa na kusanyiko lingine lolote. Hivi ndivyo tunavyoona Yesu akiyaonya makanisa 7 ktk Ufunuo 2-3; hapakuwa na makao makuu ya kupokea maagizo yake. Kanisa Linashirikiana katika shida na raha duniani kote, lakini halina kichwa duniani, isipokuwa Kristo peke yake (Efe.2:22-23; Kol.1:18).

Mtu ili awe mshiriki wa kanisa la Kristo anapaswa kufanya sawasawa na jinsi walivyofanya karne ya kwanza, kama tunavyosoma ktk Matendo: Mosi, mwenye dhambi alisikia mahubiri ya injili; pili, aliamini injili (2:37; 8:12-13); tatu, aliambiwa kutubu dhambi (2:38); nne, alimkiri Kristo mbele ya watu kuwa ni Mwana wa Mungu (8:37); na nne, alibatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake (2:38,41; 22:16, nk).

3) Ibada ya kanisa ni sawa na jinsi mitume walivyoabudu: 1) waliimba bila kutumia ala za muziki, nasi tunafanya hivyo; 2) tunasikiza mahubiri kama wao (Mdo.20:7); 3) tunashiriki meza ya Bwana kila siku ya kwanza ya Juma, kama wao (Mdo. 20:7); 4) tunatoa sawasawa na kufanikiwa kwetu bila kulazimishwa au kufanya minada (1Kor.16:1,2; 2Kor.9:7). 5) Wanaume wanaongoza ibada na sala ktk halaiki yenye mchanganyiko wa wanaume na wanawake (1Tim.2:8-15). Semina na kongamano za akina mama wanaongoza wanawake wenyewe. N.k.

Karibuni kanisa la Kristo lililopo pande mbalimbali za nchi. Kwa Dar lipo: Magomeni, Temeke Mwembeyanga, Mbagala Rangitatu, Kitunda, Keko, Mbezi, nk. Mbeya mjini Forest, Arusha - Unga Limited, Mwanza - Kishiri na Michungwani, Iringa mjini na Mapogolo, nk.

Mungu awabariki nyote mnaochunguza Maandiko ili kutafuta usahihi wa mambo kama walivyofanya Waberoya (Mdo.17:11).
 
Naskia huwa wanasali usiku wa manane,af nlskia pia kuwa wanaabudu bila kuvaa nguo, Mara y kwanza nlkuw siamin ,bt kwa maswal haya ya wadau naanza kuamin taratib ,itakuw n kwel
sio kwel
 
Nipo hapa Mkristo wa kanisa la Kristo, moja ya tawi lake ni Magomeni. La Morocco siyo Kanisa la Kristo, linaitwa Jesus Christ Church(Kanisa la Yesu Kristo) hawa siwajui, lakini la Magomeni ni Kanisa la Kristo (Church of Christ) nawajua na ni muumini pia.

Hivyo waumini tupo, na tunajielewa kwelekweli, hakuna mafundisho ya upotofu kama kwenye madhehebu, kanisani tunajifunza na kufanya neno yaani Kristo alivyo agiza.

Ukitaka kuja kushiriki nasi unakaribishwa, jumapili ni kuanzia saa tatu hadi saa sita.

Pia kwa magoneni dsm, kuna mafundisho ya biblia kila siku ya jumatano. Namtafta muumini wa pale ntawapa ratiba ya wiki nzima.

Kwa sasa mimi niko Magu mwanza, ila nakusanyika kanisa la Kristo Kishiri Igoma, au kanisa la Kristo michungwani kilimahewa mwanza. Ni mshazali na kwa malisa
good
 
Mkuu nisha eleza mengi sana. halafu jibu lako la kwanza, linatofautiana na jibu lako la pili. Jibu lakwanza umesema nieleze tunavyo sali lkn jibu la pili hutaki kueleza imani uliyoishuhudia.

Anyway, kwa faida yako narudia kukupa ratiba ya wiki nzima, na imerudiwa sana. hii hapa mkuu

Ratiba ya ibada na vipindi vya kanisa, kwa wale walioko dsm, kanisa la Kristo Magomeni ratiba kwa wiki ni hii.

Magomeni CoC- Church of Christ

Ratiba ya Ibada zetu :
Jpili asbh saa tatu - sita mchana,

jioni saa kumi na moja mpaka saa kumi na mbili,

jtano saa kumi na moja mpaka saa kumi na mbili jioni. Mafundisho ya biblia(Bible school)

Karibuni tujifunze neno la Mungu kwa utukufu wake, hautojuta kujifunza neno, bali utajilaumu kwa kuchelewa.
Then you are done brother!
 
Nimeona mdau mmoja akiuliza kuhusu Kanisa la Silom na Mimi nikapata wazo la kuuliza kuhusu makanisa mawili niliyotaja hapo juu. Hivi haya makanisa yana waumini kweli maana sijawahi kuona watu wakiingia kuabudu wala kuona magari yamepaki nje pamoja na kuonekana kuwa ni makubwa sana.

Samahani kama nitakuwa nimemkwaza mtu
Yale makanisa nasikia yana matatizo.
Ni ya mpinga Kristo, na tafuta alama ya msalaba hutauona.
 
Kanisa la Kristo lililopo Magomeni ni tofauti na lile kanisa la Mormon - Morroco. Ratiba ya kanisa la Kristo Magomeni: Jpili saa 3 asubuhi na jioni saa 11. Pia Jtano saa 11 jioni. Ni mojawapo ya makusanyiko mengi yaliyopo duniani kote yenye kuamini mambo ya msingi yafuatayo: (1) Agano Jipya la Yesu Kristo ndio katiba pekee ya kuongoza vitendo vya Wakristo na ibada. Sawasawa na jinsi Yesu alivyowaagiza mitume wake kwamba walipaswa kuwafundisha injili mataifa yote na kushika yote aliyokuwa amewaagiza (Math. 28:18-20). Akiwakataza kuongeza au kupunguza ktk maagizo hayo (Ufu.22:18,19; taz. 1Kor.4:6; Gal.1:6-9). Maandiko yaliyotangulia kuandikwa (Agano la kale) yaliandikwa ili kutufundisha sisi (tunaoishi chini ya Agano Jipya) ili kwa faraja na saburi ya Maandiko tupate kuwa na matumaini (Warumi 15:4). Pia, tunajifunza ktk Agano la kale mifano ya jinsi Mungu alivyoshughulika na watu wema na wabaya hapo nyuma (1Kor.10:1-11).

2) Kanisa la Kristo linaamini kuwa Mwenye mamlaka yote duniani na mbinguni ni Kristo na wala si mwanadamu (Math.28:18). Hakuna nchi yenye maraisi wawili! (Kanisa limetajwa kuwa ni nchi 1Pet.1:15-16). Kanisa la Kristo halina makao makuu duniani. Kwani kanisa linaamini kwamba alipo mkuu wa kanisa, ambaye ni Kristo ndipo yalipo makao makuu. Kila kusanyiko ni "autonomous," linajitegemea kimaamuzi chini yaKristo bila kuingiliwa na kusanyiko lingine lolote. Hivi ndivyo tunavyoona Yesu akiyaonya makanisa 7 ktk Ufunuo 2-3; hapakuwa na makao makuu ya kupokea maagizo yake. Kanisa Linashirikiana katika shida na raha duniani kote, lakini halina kichwa duniani, isipokuwa Kristo peke yake (Efe.2:22-23; Kol.1:18).

Mtu ili awe mshiriki wa kanisa la Kristo anapaswa kufanya sawasawa na jinsi walivyofanya karne ya kwanza, kama tunavyosoma ktk Matendo: Mosi, mwenye dhambi alisikia mahubiri ya injili; pili, aliamini injili (2:37; 8:12-13); tatu, aliambiwa kutubu dhambi (2:38); nne, alimkiri Kristo mbele ya watu kuwa ni Mwana wa Mungu (8:37); na nne, alibatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake (2:38,41; 22:16, nk).

3) Ibada ya kanisa ni sawa na jinsi mitume walivyoabudu: 1) waliimba bila kutumia ala za muziki, nasi tunafanya hivyo; 2) tunasikiza mahubiri kama wao (Mdo.20:7); 3) tunashiriki meza ya Bwana kila siku ya kwanza ya Juma, kama wao (Mdo. 20:7); 4) tunatoa sawasawa na kufanikiwa kwetu bila kulazimishwa au kufanya minada (1Kor.16:1,2; 2Kor.9:7). 5) Wanaume wanaongoza ibada na sala ktk halaiki yenye mchanganyiko wa wanaume na wanawake (1Tim.2:8-15). Semina na kongamano za akina mama wanaongoza wanawake wenyewe. N.k.

Karibuni kanisa la Kristo lililopo pande mbalimbali za nchi. Kwa Dar lipo: Magomeni, Temeke Mwembeyanga, Mbagala Rangitatu, Kitunda, Keko, Mbezi, nk. Mbeya mjini Forest, Arusha - Unga Limited, Mwanza - Kishiri na Michungwani, Iringa mjini na Mapogolo, nk.

Mungu awabariki nyote mnaochunguza Maandiko ili kutafuta usahihi wa mambo kama walivyofanya Waberoya (Mdo.17:11).
Aksante sana mwalimu.

Ujumbe kwa wote wenye kutaka kujifunza mengi zaidi, huyu jakigili, ni mwalimu hasa. muulize chochote atakujibu kwa ufasaha. kama mimi nimekujibu na umeridhika, basi ukijibiwa na mwalimu jakigili utaridhika zaidi. mimi pia ni mwanafunzi wake
 
Kanisa la kristo hata mbeya yapo.yana waumini japo sio wengi.kanisa la kristo linaendeshwa na wamishionari,ndio wamiliki wa chimala mission hospital na chuo cha uuguzi chimala.kwa Mbeya lipo forest mkabala na kituo cha mafuta gapco maarufu kama kituo cha daladala esso barabara ya Mbeya Tunduma
 
Mdau usimix makarabrasha... Christ Embassy church na church of last days saints ni kama KKKT na wasabato... Ni makanisa mawili tofauti
Hili analozungumzia mtoa maada linaitwa kanisa la kristo au church of Christ
 
Kanisa la kristo hata mbeya yapo.yana waumini japo sio wengi.kanisa la kristo linaendeshwa na wamishionari,ndio wamiliki wa chimala mission hospital na chuo cha uuguzi chimala.kwa Mbeya lipo forest mkabala na kituo cha mafuta gapco maarufu kama kituo cha daladala esso barabara ya Mbeya Tunduma
Ulishawahi kisali hapo mkuu?
 
Back
Top Bottom