Kanisa la Kristo Morroco na Magomeni

Kanisa la Kristo Morroco na Magomeni

Na ubatizo wao ni wa maji mengi,ila wapo vizuri maana mchungaji anabadirisha magari ya kutembelea
Kwa mara ya kwanza nasikia kutoka kwako kuwa kanisa la Kristo lina mchungaji. Watu wenye magari wapo, maana wanafanya kazi kama wewe lkn mchungaji ni Yesu pekee mkuu.

Labda unifungue, ni mchungaji nani anaitwa huyo wa huko mbeya?

Wa kanisa gani? Kanisa la Kristo?
 
Mkuu na Mimi ningependa sana kujua kuhusu la Morroco maana niliwahi kusikia story moja ambayo sio nzuri sana
 
Kanisa la moroco na la external kituo cha polisi mbele ni la mitume wa siku zijazo. Hawa jamaa wana ruhusu polygamy au wake wengi. Hakuna kunywa chai na sort of eating healthy.
Hapo kama una mazoea ya kupenda miujiza hapo sio mahala pako hapo ni neno na kujifunza kupitia maandishi sana.
 
Kanisa la Kristo lililopo Magomeni ni tofauti na lile kanisa la Mormon - Morroco. Ratiba ya kanisa la Kristo Magomeni: Jpili saa 3 asubuhi na jioni saa 11. Pia Jtano saa 11 jioni. Ni mojawapo ya makusanyiko mengi yaliyopo duniani kote yenye kuamini mambo ya msingi yafuatayo: (1) Agano Jipya la Yesu Kristo ndio katiba pekee ya kuongoza vitendo vya Wakristo na ibada. Sawasawa na jinsi Yesu alivyowaagiza mitume wake kwamba walipaswa kuwafundisha injili mataifa yote na kushika yote aliyokuwa amewaagiza (Math. 28:18-20). Akiwakataza kuongeza au kupunguza ktk maagizo hayo (Ufu.22:18,19; taz. 1Kor.4:6; Gal.1:6-9). Maandiko yaliyotangulia kuandikwa (Agano la kale) yaliandikwa ili kutufundisha sisi (tunaoishi chini ya Agano Jipya) ili kwa faraja na saburi ya Maandiko tupate kuwa na matumaini (Warumi 15:4). Pia, tunajifunza ktk Agano la kale mifano ya jinsi Mungu alivyoshughulika na watu wema na wabaya hapo nyuma (1Kor.10:1-11).

2) Kanisa la Kristo linaamini kuwa Mwenye mamlaka yote duniani na mbinguni ni Kristo na wala si mwanadamu (Math.28:18). Hakuna nchi yenye maraisi wawili! (Kanisa limetajwa kuwa ni nchi 1Pet.1:15-16). Kanisa la Kristo halina makao makuu duniani. Kwani kanisa linaamini kwamba alipo mkuu wa kanisa, ambaye ni Kristo ndipo yalipo makao makuu. Kila kusanyiko ni "autonomous," linajitegemea kimaamuzi chini yaKristo bila kuingiliwa na kusanyiko lingine lolote. Hivi ndivyo tunavyoona Yesu akiyaonya makanisa 7 ktk Ufunuo 2-3; hapakuwa na makao makuu ya kupokea maagizo yake. Kanisa Linashirikiana katika shida na raha duniani kote, lakini halina kichwa duniani, isipokuwa Kristo peke yake (Efe.2:22-23; Kol.1:18).

Mtu ili awe mshiriki wa kanisa la Kristo anapaswa kufanya sawasawa na jinsi walivyofanya karne ya kwanza, kama tunavyosoma ktk Matendo: Mosi, mwenye dhambi alisikia mahubiri ya injili; pili, aliamini injili (2:37; 8:12-13); tatu, aliambiwa kutubu dhambi (2:38); nne, alimkiri Kristo mbele ya watu kuwa ni Mwana wa Mungu (8:37); na nne, alibatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake (2:38,41; 22:16, nk).

3) Ibada ya kanisa ni sawa na jinsi mitume walivyoabudu: 1) waliimba bila kutumia ala za muziki, nasi tunafanya hivyo; 2) tunasikiza mahubiri kama wao (Mdo.20:7); 3) tunashiriki meza ya Bwana kila siku ya kwanza ya Juma, kama wao (Mdo. 20:7); 4) tunatoa sawasawa na kufanikiwa kwetu bila kulazimishwa au kufanya minada (1Kor.16:1,2; 2Kor.9:7). 5) Wanaume wanaongoza ibada na sala ktk halaiki yenye mchanganyiko wa wanaume na wanawake (1Tim.2:8-15). Semina na kongamano za akina mama wanaongoza wanawake wenyewe. N.k.

Karibuni kanisa la Kristo lililopo pande mbalimbali za nchi. Kwa Dar lipo: Magomeni, Temeke Mwembeyanga, Mbagala Rangitatu, Kitunda, Keko, Mbezi, nk. Mbeya mjini Forest, Arusha - Unga Limited, Mwanza - Kishiri na Michungwani, Iringa mjini na Mapogolo, nk.

Mungu awabariki nyote mnaochunguza Maandiko ili kutafuta usahihi wa mambo kama walivyofanya Waberoya (Mdo.17:11).[/QUOTE

nasikia kanisa haliamini unabii, wala uponyaji, maana hayo kanisa linaamini zilifanywa na manabii na mitume wa zamani
 
morocco ipi mnazungumzia pale moroko hotel karibu na hosp ya magomen? au
 
Naskia huwa wanasali usiku wa manane,af nlskia pia kuwa wanaabudu bila kuvaa nguo, Mara y kwanza nlkuw siamin ,bt kwa maswal haya ya wadau naanza kuamin taratib ,itakuw n kwel
Nilidhani umeshuhudia kwa macho yako, kumbe umesikia tu?
 
Kama mshana Jr amepost kwenye hii sredi basi hilo kanisa kuna kitu ndani yake katika ule ulimwengu mwingine Wa burudani

[emoji1] [emoji1] [emoji1] ulidhani nini kwanj[emoji12]
hahahaha!
 
Siku ya kwanza ni kwa mujibu wa Gregorian Calenda ambayo ndiyo inahesabu kabla na baada ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. hivyo siku ya Kwanza ya Juma ni JUMAPILI. Siku hii ndipo Yesu alifufuka, ndiyo siku Yesu alipaa na wengine wataalamu wa historia wanasema ndiyo Yesu Kristo alizaliwa.

Kwa kuwa neno Ibada ni kukumbuka, tunakusanyika siku ya jumapili kukumbuka matendo makuu ya Mungu.
Hapa ndipo walipotuweza wazungu hivi ina Jumapili iwe siku ya kwanza katika juma ikiwa yenyewe inatambulishwa pili, au jumamosi iwe siku ya saba wakati inatumbulishwa mosi kwa maana ya kwanza au moja? Usitumie hizo siku sa sunday, monday etc maana ukija hapo nitakuuliza ilikuaje hizo siku ambazo warumi walikua wanaabudu miungu yao wakazibatiza siku kwa majina ya walivyokua wanaabudu aina za miungu na hata kwenye miezi hivyo pia
 
Siku zilikuwepo kama zilivyoubwa, ila majina hutoa wanadamu. Kama vile wanyama Adam ndiye aliyetoa majina ya wanyama hao. Hata watoto wetu sisi ndiye tunatoa majina, mbali na ukweli kwamba Mungu ndiye anayeumba vyote. Ni sawa na nchi Tanganyika iliumbwa na Mungu na ilikuwepo tangu Adam, lakini jina la Tanganyika halijatajwa na Mungu, awali kabisa walilitoa Wajerumani. Siku ya kwanza, ya pili, ya tatu, n.k. ndivyo Wayahudi walivyoziita siku hivyo.

Ikumbukwe kwamba asilia Biblia iliandikwa kwa lugha mbili: Kiebrania (lugha ya Wayahudi au Waisraeli) na sehemu ndogo Kiarami; na Kiyunani (lugha iliyotumika karne ya kwanza). Mataifa mbalimbali yamekuwa huru na utamaduni wa kuzipa siku majina. Kalenda ni nyingi duniani kulingana na utamaduni wa watu. Tarehe 1 January (kwa mujibu wa kalenda ya Papa Gregory) ilikuwa trh 20 mwezi 10, mwaka wa 5,778 kalenda ya Kiyahudi. Kwa Kiebrania inaitwa "Tevet - Shevat 5,778. Wayahudi mwaka mpya ni kati ya March na April wa kalenda hii ya Gregory. Hivi sasa Wayahudi wameingia mwaka 5,779. Tarehe 8 February Wachina walisherehekea mwaka mpya. Kwa sasa Wachina wako mwaka wa 4,714. Octoba 1 mwaka jana Waarabu walisherekea mwaka wa 1,439. n.k.

Kidini kalenda ya Waisraeli ilitofautiana na kalenda iliyoongoza shughuli za kiserikali. Kidini tunasoma, "Mwezi huu utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu" (Kutoka 12:2).

"Ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake; ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele. Amina." (Warumi 9:4-5).

Umejitahidi kutoa maelezo marefu lakini hayajajibu swali na hivi ndivyo watz wengi tulivyo sishangai kwa nini watoto siku hizi wanafeli sana rudia kusoma tena nilichoandika hapo juu halafu linganisha na majibu yako
 
Ndani ya jengo la ibada la kanisa la Kristo magomeni
IMG_20180616_163621.jpg
 
Attachments

  • IMG_20180616_163621.jpg
    IMG_20180616_163621.jpg
    245.7 KB · Views: 29
Back
Top Bottom