Kanisa la Kristo Morroco na Magomeni

Kanisa la Kristo Morroco na Magomeni

Nimeona mdau mmoja akiuliza kuhusu Kanisa la Silom na Mimi nikapata wazo la kuuliza kuhusu makanisa mawili niliyotaja hapo juu. Hivi haya makanisa yana wahumini kweli maana sijawahi kuona watu wakiingia kuabudu wala kuona magari yamepaki nje pamoja na kuonekana kuwa ni makubwa sana.

Samahani kama nitakuwa nimemkwaza mtu
Nipo hapa Mkristo wa kanisa la Kristo, moja ya tawi lake ni Magomeni. La Morocco siyo Kanisa la Kristo, linaitwa Jesus Christ Church(Kanisa la Yesu Kristo) hawa siwajui, lakini la Magomeni ni Kanisa la Kristo (Church of Christ) nawajua na ni muumini pia.

Hivyo waumini tupo, na tunajielewa kwelekweli, hakuna mafundisho ya upotofu kama kwenye madhehebu, kanisani tunajifunza na kufanya neno yaani Kristo alivyo agiza.

Ukitaka kuja kushiriki nasi unakaribishwa, jumapili ni kuanzia saa tatu hadi saa sita.

Pia kwa magoneni dsm, kuna mafundisho ya biblia kila siku ya jumatano. Namtafta muumini wa pale ntawapa ratiba ya wiki nzima.

Kwa sasa mimi niko Magu mwanza, ila nakusanyika kanisa la Kristo Kishiri Igoma, au kanisa la Kristo michungwani kilimahewa mwanza. Ni mshazali na kwa malisa
 
Ni kwa nini huruhusiwi kukanyaga
Anadanganya, magomeni unaruhusiwa. Tena kuna masomo ya biblia bure kabisa hudaiwi chochote. Ntaweka ratiba soon, kuna mhusika nimemtumia anitumie ratiba ya wiki
 
Kuna jamaa yangu mmoja aliwahi kunisimulia kitambo sana kuwa ukiingia lugha wanayotumia kusali huwezi kuelewa kwa urahisi alafu unapewa msosi wa hatari
Kanisa lipi? La magomeni au la morocco? Maana ni vitu viwili tofauti.

Lugha inayotumika kanisa la kristo popote, ni lugha rahisi na ya kueleweka. Hivyo, hata magomeni ni kiswahili cha kawaida tu
 
Ili uwe muumini hapo ufanyeje..!??nataka sali humo.
Kwa kanisa la Kristo Magomeni, au popote pale, ni kufundishwa habari za Yesu Kristo(haijalishi muda gani), kuziamini na kubatizwa. Ukishwa batizwa, umefanyika kuwa mwanafunzi wa Kristo, hivyo unakuwa na fursa sawa na aliyekibatiza. Ila utahitaji kuendelea kujifunza siku zote ili kiwango cha kulijua neno kiwe kikubwa na cha kuridhisha.
 
Hawa ni CHURCH OF THE LATTER SAINTS wanamwamini sana JOSEPH SMITH, MORMMONS!
 
Tusaidie kufahamu maana hata Mimi sijawahi ona hata wafanya usafi, lakini pako safi sana. Fukunyufukunyu tusaidieni.
Waumini kanisa la Kristo wapo. Sijui kuhusu la morocco, maana siyo kanisa la Kristo, ni kanisa la Yesu Kristo.
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa Maarifa.
Nani wanaangamia? Kwa mimi ambaye ni muumini wa Kanisa la Kristo, nawaona watu wa madhehebu ndio wanaoangamia. Maana wamejitungia ibada zao wenyewe, wameacha kando maagizo ya Kristo. Na ni ngumu mtu kutoka huko kwenye madhehebu, maana watu wamejazwa elimu za upotofu tu.
 
Pastor Gwajima kama sikosei alishasema pale morroco ni waashi huru kama kuna mtu anaona amedaganya amchukulie hatua
 
Nilivyokuwa marekani nili sali sana kwenye haya makanisa, wana upendo wa ajabu! Niliwapenda sana system yao ya upendo!
 
Back
Top Bottom