Kanisa la Kristo Morroco na Magomeni

Kanisa la Kristo Morroco na Magomeni

FB_IMG_1541079420776.jpg
 
Nini maana ya neno kanisa? Kanisa sio jengo la ibada la wakristo, la! Bali neno kanisa limetokana na neno la kigiriki; *ekklesia* lenye maana: _mkusanyiko wa watu walioitwa_.

Waisraeli waliitwa _kanisa jangwani_ kwa kuwa ni mkusanyiko wa watu walioitwa watoke Misri na kwenda Kaanani, Matendo7:38
Wakristo leo hii wanaitwa kanisa pia kwa kuwa ni mkusanyiko wa watu walioitwa watoke katika _ufalme wa shetan na kuingia ufalme wa Yesu Kristo_, Kol. 1:13-14.

Yesu alsema kwenye Mathayo 16:18 kuwa: "nitalijenga kanisa langu". Hakumaanisha kuwa atalijenga juu ya Petro, la! Kwa kuwa Petro hajawahi kuitwa *mwamba* kwenye bblia na maana ya jina Petro ni _jiwe_ na si mwamba maana vina utofauti, tazama Yohana 1:42. Yesu alimaanisha kuwa atalijenga juu yake mwenyewe maana yeye ndiye mwamba, tazama 1 Wakorntho 10:4.

Kazi ya mitume na manabii ilkuwa ni kuweka msingi tu ambao ndio Yesu kristo mwenyewe, tazama Efeso 2:20, 1 Korntho 3:10.

KWANINI KANISA NI LA KRISTO?

Kwa kuwa Yesu *amelijenga* kanisa lake mwenyewe juu yake mwenyewe na *kulinunua* kwa damu yake mwenyewe ya thaman kama panavyosema Matendo 20:28 basi kanisa ni *mali yake* mwenyewe na linafaa kuitwa kwa _jina lake mwenyewe_; Kwa kuwa ndilo jina pekee ambalo *latuokoa*, soma Matendo 4:10-12 na pia tunampa *utukufu* Mungu kwa jina hilo, 1 Petro 4:15-16.

Na pia kwa kuwa _tumeposwa_ kiroho na Bwana wetu Yesu kristo, soma 2 Kor 11:2. Na uhusiano uliopo kati ya yeye na kanisa lake ni kama ule wa mume na mke, Efeso 5:25-29 basi hatuna budi kutumia _jina lake_ kama mke anavyotumia _jina la mumewe_. Sidhani kama kuna mume atakayependa mke wake apewe jina la mume mwingine.

Na ndio maana pia tumepewa jina kuwa sisi ni _Wa-Kristo_ kwa hivyo kanisa pia lazima liwe ni la Kristo.

Kanisa ni Mwili wa Kristo(Wakolsai 1:24, Efeso 1:22-23).

Kanisa linaitwa ni mwili wake kwa kuwa ni watu waliomvaa Yesu Kristo kwa njia ya ubatizo; Gal 3:27. Na pia linaitwa hivyo kwa kuwa wakristo wamefananishwa na viungo katika mwili wake ambao yeye ndiye kichwa; 1 Wakorntho 12:12-31, Warumi 12:4-5, Efeso 5:23-24.

Je! Yesu Kristo anayo miili mingapi basi? Jibu ni mmoja tu; Efeso 4:4, 1 Wakorntho 12:12-13, 20. Kwa hyo kanisa lake ni moja tu kwa kuwa *mwili na kanisa ni mamoja*.

Je! Kuna ulazima wa kuwepo katka kanisa lake hilo moja "pekee"? Jibu ni ndiyo; kwa maana alisema mtu haji kwa baba ila kwa " njia" ya yeye, Yoh 14:6. Kwa maana yeye ndiye *mwokozi wa mwili* yaani wa kanisa, Efeso 5:23. Na waliookolewa wamo ndani ya kanisa; Matendo 2:47.

Kwa hiyo ili kwenda kwa baba(mbinguni) lazima tuwe ndani yake yaani ndani ya mwili wake ambao ni kanisa lake.

***SIFA ZA KANISA LA KRISTO***
(Vinavyotofautisha kati ya KANISA na MADHEHEBU)

#1. Jina la Kanisa hulitukuza jina lake Kristo
(Wakolosai 3:17, Wafilipi 2:9-11)

#2. Kristo ndye Kichwa pekee (hakuna kiongoz mkuu wa kidunia)
(Wakolosai 1:18, 2:6-7)

#3. Makao makuu yake ni mbinguni pekee (hakuna makao makuu ya kidunia)
(Wafilipi 3:20, Waebrania 12:23)

#4. Neno la Mungu(Biblia) ndyo msingi na kanuni pekee(hakuna kitabu cha ziada)

#5. Kila kusanyiko lajitegemea kiuongoz
(Matendo 14:23, 20:17)

#6. Linaendeshwa na utoaji wa hiari wa wakristo(hakuna matoleo ya lazima)
(1 Wakorintho 16:1-2, 2 Wakorintho 9:7)

#7. Uongozi ni wanaume pekee
(1 Wakorintho 14:34-35, 1 Timotheo 2:8-15)

#8. Linaonganishwa kwa imani moja
(Waefeso 4:5, 2 Petro 1:1, 1 Wakorintho 1:10, Wafilipi 1:27, Warumi 15:5-6)

#9. Siku ya kuabudu
(Matendo 20:7, 1 Wakorintho 16:1-2)

#10. Namna ya kuabudu
(Yoh 4:23-24)

#11. Ibada yake:
Kuimba(Waefeso 5:19)
Kusali(1 Timm 2:8)
Mahubiri(Matendo 20:7)
Kutoa/changizo(kwa hiari)1 Wakorintho 16:1-2, 2 Wakorintho 9:7
Meza/chakula ya Bwana(Matendo 20:7)

#12. Jinsi ya kuwa mshiriki:
Uisikie Injili(Rumi 10:17)
Uiamini(Yoh 3:16)
Utubu dhambi(Luka 13:3)
Umkiri Kristo(Rumi 10:9-10)
Ubatzwe(maji mengi)Matendo 2:38

#13. Ndyo njia pekee ya kwenda mbinguni
(Waefeso 5:23, 1 Wakorintho 12:20, 27; Wakolosai 1:18)
 
maneno mengi hapa umehitimisha utakavyo wewe na SIO Maneno ya Yesu mwenyewe wala Biblia haijasema ukisemacho wewe.

Hakuna sehemu yyt Yesu kasema AABUDIWE YEYE bali kaamrisha AABUDIWE MUNGU MMOJA TU.

John 4:23-24 English Standard Version (ESV)

23 But the hour is coming, and is now here, when the true worshipers will worship the Father in spirit and truth, for the Father is seeking such people to worship him. 24 God is spirit, and those who worship him must worship in spirit and truth.”

pia

Hakuna sehemu Yesu kasema MAKANISA yaitwe jina lake. hio umesema wewe . wala Hakuna sehemu Yesu kasema watu WAIMBE kwenye Ibada zao. hizo ni KELELE.

Ibada inayotakiwa ni IBADA YA UKIMYA tena wenye unyenyekevu.

Matayo 6:5-7 Neno: Bibilia Takatifu

Mafundisho Kuhusu Sala

5 “Na mnaposali, msiwe kama wanafiki; maana wao wanapenda kusimama na kusali katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Nawaambieni kweli, wao wamekwisha kupata tuzo yao. 6 Unaposali, nenda chumbani kwako ufunge mlango na umwombe Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini atakupa tha wabu.

Acha kupotosha watu. utahukumiwa siku ya malipo vibaya sana.
 
Ndg, hoja yako ya kwanza:
Ukimuabudu Yesu Kristo ni umemuabudu Mungu, kwa maana Yesu Kristo ni Mungu.
Yohana:1.1
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
3. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
14. Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Yohana:10.30
Mimi na Baba tu umoja.
Yohana:14.7
Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.
8. Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.
9. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
1 Timotheo:3.16
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Wafilipi:2.5
Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
6. ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
7. bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;

Hoja yako ya pili;
Sidhani kama umeyatilia maanani niliyoyaandika awali kuhusu jina la kanisa, maana usingeibua hii hoja.. Labda kama utakuwa hukuelewa ndg.
Yesu Kristo alisema "nitalijenga kanisa langu", je! Hilo kanisa lake litaitwa la nani?
Kama sisi tunaitwa "Wa-Kristo", nalo kanisa ni "La-Nani"?
Mathayo:16.18
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Warumi:16.16
Salimianeni kwa busu takatifu. MAKANISA yote YA KRISTO yawasalimu.

Hoja yako ya tatu;
Waefeso:5.19
mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;

Hoja yako ya mwisho;
Mathayo 6:5-7 umeshindwa kutofautisha sala za pamoja na sala binafsi ndg, hapa Yesu Kristo hakuwa anaongelea sala za ibadani za pamoja bali sala binafsi.
1 Timotheo:2.1
Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;

Matendo ya Mitume:2.42
Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika KUSALI.
47. WAKIMSIFU Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.

Sina haja ya kupotosha watu ndg, injili sio yangu bali ni ya Yesu Kristo; mimi kazi yangu ni kuihubiri tu. Na ahsante kwa kunikumbusha kuwa kuna hukumu siku ya malipo. Ubarkiwe!
 
Unadai unahubiri lkn hujui kuwa Unahibiri maneno ya PAULO mtu ambae hawajawahi kukutana na Yesu wala Kumuona hata mara moja ktk maisha yake yote.
Zaidi ya ile so called Ndoto ya mchana aliyeishuhudia mwenyewe Paulo.

Soma Yesu anatamka nini kwa KAULI YAKE MWENYEWE Kuhusu NANI NI MUNGU.

"Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, MTU ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo."

Yohana 8:40

Katika andiko hilo YESU kwa kinywa chake yeye mwenyewe amejiita kuwa ni "MTU". Kama kuna mtu ana ushahidi wowote katika biblia YESU akijiita MUNGU, basi nami hapo nitaamini kuwa YESU Mungu.

Hata hivyo, mnaweza kusema pia, kuwa YESU alikuwa Mungu na Pia alikuwa mtu. Hata hivyo tukitazama sifa mbalimbali za mungu kama zilivyo tajwa au ainishwa na biblia, utaona hata kiduchu YESU hana sifa hizo.

Mathalani.

"Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza.."

Hesabu 23:19

Tumeona katika Yohana 8:40 Yesu akijiita Mtu, na hapa katika hesabu tunaambiwa Mungu si mtu, sasa wewe unayemuita Yesu Mungu umepata wapi?

NANI KAFUNDISHA YESU NI MUNGU?

"tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; "

Tito 2:13

Hayo maneno katika kitabu cha Tito, kimsingi ni barua ya kimisionari aliyo andika Paulo kwa watu wa Tito, kama tuonavyo katika barua hiyo, pamoja na mambo mengine Paulo anawaambia watu wa Tito kuwa Yesu ni Mungu Mkuu, maneno haya ya Paulo yanakwenda kinyume kabisa na maneno ga Yesu mwenyewe aliyo yasema katika Yohana 8:40 lakini kinyume kabisa na mafundisho ya kinabii kutoka katika kitabu cha Hesabu 23:19.

YESU ANASEMAJE KUHUSU PAULO?

Awali ya yote Paulo hakuwahi kuwa mwanafunzi wa Yesu na hakuwahi kumuona Yesu Kristo. Yesu kabla hajapaa kwenda mbinguni aliwahi kusema maneno haya.

"Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi"

Yohana 16:1-3

Hapa Yesu anatabiri kuwa wanafunzi wake watakuja kuuliwa, anatabiri wakristo na wafuasi wa kanisa lake watakuja kuuliwa, na akasisitiza huyo atajaye wauwa wanafunzi wake hamjui yeye wala Baba(Mungu)

Nani huyo aliyeua wanafunzi wa Yesu? Jawabu ni Sauli ambaye ni Paulo.

"Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu."

Matendo 9:1-3

Kwa hivyo Mtu aliyetajwa na Yesu katika injili ya Yohana 16:1-3 kuwa atawaua wanafunzi wa Yesu si mwingine Paulo, na katika kitabu cha matendo tunaoneshwa ukatili wa Paulo kwa wanafunzi wa Yesu. Hata hivyo, Bwana Yesu anaendelea na utabiri wake juu ya Paulo katika aya hii.

"Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo"

Yohana 8:44

Katika aya hiyo Bwana Yesu anasema huyo Paulo si kwamba ni muuaji tu, lakini pia mtu muongo sana. Na uongo mkubwa alio ufanya Paulo ni pale aliposema kakutana na Yesu na kisha akajifanya kipofu.

"Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda"

Matendo 9:3-7

Baaada ya Paulo kuwaua sana wanafunzi wa Yesu na kuwatesa sana ili waache mafunzo ya Yesu, lakini wanafunzi wa Yesu waligoma na walikataa katakata kuachana na mafunzo Yasu. Pia naomba mjue, mafunzo ya Yesu yalikuwa mwiba kwa serikali(Dola ya Rumi) na Paulo alikuwa anatumiwa na serikali katika kuhakikisha wanafunzi wa Yesu wanaachana na ukristo/uyaudi.

Pamoja na juhudi hizo za Paulo lakini alishindwa, hivyo njia aliyo amua kuitumia si nyingine bali ni kujiunga na wanafunzi wa kristo. Na ili aaminike ndipo hapo alipotengeneza stori ya kumuona Yesu na maagizo ya upofu, lakini kubwa zaidi alimnunua Anania ili msaidie kufanikisha lengo lake. Kwa kumtumia Anania na kwa kudanganya kwake kuwa kamuona Yesu, wanafunzi wa Yesu walimkubali.

Na hapo ndipo Paulo alipoanza kuyachakua mafunzo ya Yesu, na ndio maana ukristo wa sasa si ule alio ufundisha Yesu.

YESU NA MFARISAYO.

"Ewe FARISAYO KIPOFU, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi. Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote."

Mathayo 26:23

Paulo msomi mkubwa alikuwa Farisayo, lakini Yesu alisema nini juu mafarisayo? Kama tulivyo ona, Yesu anawaona mafarisayo kama vipofu, lakini kubwa katika andiko hili Yesu anamtabiri pia Paulo na maigizo yake ya upofu.

"Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu"

Matendo 23:6

Kwanza Paulo amekiri kwa kinywa chake kuwa yeye ni farisayo. Lakini hiyo haitoshi Paulo alijitia upofu aso kuwa nao.

"Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi."

Matendo 9:8-9

Katika aya hizi tunaona kuwa Paulo amekiri kuwa Farisayo lakini pia tunaona Paul yuko katika maigizo ya upofu. Yote haya mawili yanakamilisha unabii wa Yesu pale aliposema

"Ewe farisayo kipofu.."

Mathayo 26:23

Katika aya hizo inatajwa sifa kuu au tabia kubwa ya Mafarisayo, na ambayo imethibiti(ilitimia) kwa Paulo. Sifa hiyo si nyingine bali UNAFIKI.

Paulo alikuwa mnafiki, yaani alijifanya muumini wa mafundisho Yesu ili mradi apate kuwapotosha wanafunzi wa Yesu, na hili kwakweli kafanikiwa sababu hakuna hata kanisa moja ambalo linafuata mafunzo ya asili ya Yesu. Kila kanisa lina kituko chake.

MWISHO.

Kwa kifupi huku nikizingatia maelezo yangu yote ya huko juu, kuwa YESU SI MUNGU, lakini hakumaanishi kuwa hakuna wanao muita au wanao amini Yesu Mungu. La kuzingatia kama tukiambiwa kauli ipi ya kushika kati ya YESU mwenyewe na ya Paulo kwa vyovyote vile tunatakiwa kushika kauli ya Yesu.

Kauli zote za Paulo ambazo hazipingani na za Yesu, kauli hizo tutazifuata, lakini kauli yoyote ya Paulo inayo pingana na Yesu, kauli ya Paulo itapuuzwa na kuanguka, alafu watu wote wanatakiwa wafuate kauli ya Yesu.

Hakuna kauli ya Yesu anayo alijiita Mungu, lakini zipo nyingi akijiita Mtu au mwana wa adamu. Na siku zote alijitafautisha na Mungu. Yesu anakata mzizi wa fitina katika andiko hili.

"Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma"
Yohana 17:3

Nasema YESU SI MUNGU, na Paulo ana kesi ya kujibu kwa kudanganya ulimwengu, na kwa kuharibu mafundisho ya Yesu na kubwa zaidi kwa kuwatesa na kuwaua wanafunzi wa Yesu na wafuasi wake.

Katika kuendeleza urongo wa Paulo, watu wameambukizwa urongo, sasa wanatusambazia picha na sanamu za wacheza sinema na kisha wanataka tuziheshimu kama Yesu, kweli watu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
 
Kumbe unaiamini biblia kwa yale unayotaka kuyaamini tu na mengine unayaona ni uongo, mimi naiamini yote kwa hiyo hatutoelewana. Huna nia ya kujifunza bali una misimamo yako na sipo hapa kubishana.
Hata imani yako inakiri Yesu Kristo atarudi kuhukumu, sasa subiri ukweli utaujua hapo; ila ndio utakuwa umeshachelewa.. Endelea kushindana na usichoweza kukishinda.
 
Nimepita sana hapo Morroco iwe mchana au usiku lakini sijawahi kumkuta muumini hata mmoja

Bado utafiti wako haujakamilika, nenda kakeshe hapo wiki nzima ndipo uje, kupita peke yake hakutoshi
 
Back
Top Bottom