Kanisa la KKKT limekuwa na migogoro mingi chini ya uongozi wa Askofu Shoo, Maaskofu waazimie kumuondoa

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,223
20,986
Kama kuna heshima iliyobaki ya kanisa hili, basi imeshikwa na yule mchungaji wa kijitonyama, pamoja na kwaya ya kanisa Hilo, kwingine kote ni aibu.

Uongozi wa Askofu Shoo umezalisha migogoro Kila mahala, vurugu Kila mahala, nahisi kiatu Cha ukuu wa kanisa hakimtoshi.

Nashauri kikao Cha dharura kiitishwe kumfukuza kwenye kazi ya ukuu wa kanisa. Ameshindwa.
 
Kwa yanayotokea Mbeya, huwezi kusema Hilo ni kanisa la Mungu, wachungaji wanafukuzwa kama mbwa, ngumi zinapigwa kanisani, wachungaji wanatukanwa! Aibu !
Weka ushahidi, kisa Askofu wenu ameondolewa kwa mujibu wa taratibu za kanisa mnaleta chuki zenu kwa baba Askofu hamtaweza
 
Naweza kukibaliana na wewe upande mmoja japo kuna uwezekano mkubwa kuwa wewe ni mshabiki wa malasusa.

Kanisa limechafuka, na hivyo itafanya Roho wa Bwana aondoke.
 
Hajaondolewa, bado ni askofu halali, Mwakihaba apewe uaskofu wa machame
Fanyeni fujo huko mbeya mtajua ni yupi atalindwa na dola kati ya Mwakihaba na Mwaikali.Na huyo Mwaipopo wa sumbawanga haipiti miaka miwili atakuwa nje ya mfumo.Mbinafsi na mchochezi sana.Sikiliza kauli yake baada ya mkutano wa maaskofu Dodoma.
 
Mnamuonea Askofu Shoo. System ya uongozi KKKT Askofu mkuu hana mamlaka ya kuingilia utawala wa Dayosis yeye ni kama mshauri tu
 
KKKT inapenda pesa sana.nimeacha kwenda kanisani kwa ajili ya sadaka za ovyo na watu kugeuza sehemu za vipavyo vyao.

KKKT imekuwa ofisi za walanguzi sasa
 
Mpuuzi wewe umetumwa na mafisadi wenzako kuharibu kanisa la MUNGU, Dr Shoo hanunuliki tulieni wapuuzi nyie
Huyu hata haelewi anachosema; achana naye. KKKT ndiyo inayoongoza Tanzania kwa sasa kwa kuwa na watumishi wa Mungu wengi mahiri, bora sana na waadilifu pia. Inaonyesha hata wachungaji wa KKKT hawafahamu vizuri. Huwezi ukamtenganisha Mchungaji Kimaro na yule wa Mbezi Beach pamoja na mwingine yule wa Azania Front, na wengine wengi walioko kwenye kanisa hili. KKKT nawakubali sana wachungaji wao. Mtu akiichambua KKKT kwa namna hii, unaona wazi kabisa kuwa hajuia kabisa ni nini kinaendelea huko kwingine!
 
Back
Top Bottom