Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,253
- 44,591
Kanga zina mambo mengi, zina mengi hizo kanga,
Kanga zinaficha vingi, vinavyofichwa na kanga,
Kanga zina siri nyingi, zina siri hizo kanga,
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga!
Kanga zinaona mengi, chumbani ziliko kanga,
Kanga zahifadhi vingi, vyasitiriwa na kanga,
Kanga zafunika mengi, visivyoonwa bila kanga,
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga!
Kanga zinagusa vingi vinavyoguswa na kanga,
Kanga zapangusa pengi, papanguswapo na kanga,
Kanga zina hisa nyingi, za wadau wenye kanga,
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga
Kanga zinaganda vingi, visivyoganduka bila kanga,
Kanga zinashinda nyingi, kweli vitenge si kanga,
Kanga zina rangi nyingi, na misemo kwenye kanga,
Kanga unapoachiwa , ana penzi mwenye kanga.
Kanga hata kama nyingi, atakupa moja kanga,
Kanga itasema mengi, kubwa ni hilo la kanga,
Kanga yatangaza vingi, hakuna kuzidi kanga,
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga.
UKIMPENDA ITUNZE.
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
(picha kutoka Mombasa Events)
ningekuwa hivi wangenikoma
kanizidi urefuKumbe ukoje merytina wangu?
Mzee Umeshaa chiwa khanga?
kanizidi urefu
mzima wewe?
jana mwenye tukio aligomea kuruhusu picha kuwekwa nikaamua kuipotezea sredi.
Ukiteka kipande cha nchi, shurti upandishe bendera!daughter :kumbe kuna haja yakuacha japo kipande kila unakopitia
Ukiteka kipande cha nchi, shurti upandishe bendera!
Inaonekana wewe ni mtu wa visa sana....!ningekuwa hivi wangenikoma
Jamaa kashtuka chumbani kuna kanga akampigia simu haraka mpenzi wake:
"Dear umeacha kanga yako hapa"
"Iache tu" akajibiwa.
Jioni anakuja mpenzi wake mwingine anakuta kanga ndani imesambaa juu ya kitanda kama mkeka. Anaulizwa
"Kanga ya nani hii".
"Ya dadangu" anamjibu...
liasheshe....
Kanga ina raha zake hata kwake mvaaji..
Acha we huko pembeni ulobaki mwangaliaji..
Unaetamani kuona kila saa ikiwa maji..
Hakika kanga jamani...mi naipenda sana!
Yampendeza mnene hata nae mwembamba..
Utashangaa wanaume jinsi inavyowabamba..
Mimacho itawatoka hauwaishi ushamba..
Hakika kanga jamani...mi naipenda sana!
Naifunga kibwebwe shereheni nikienda..
Ikikamata kiuno hakika utaipenda..
Nikiifunga kifuani kesi nimeshaishinda..
Hakika kanga jamani mi naipenda sana!