Leo nimemsikiliza Musukuma akizungumzia kuchelewesha kuhusu jengo la uwanja wa ndege wa Mwanza na miundo mbinu yake kuufanya uwe wa kimataifa.
Hali hii kwa sasa inatoa picha kama alivyosema Msukuma dharau kwa kanda ya ziwa haijalishi Makonda ni Mwenezi au Dotto ni Naibu Waziri Mkuu,kisiasa haitatosha kuwashawishi wananchi ambao ni wazi wanaonekana kutengwa kupitia uwanja huu, Songwe umejengwa, Arusha, Tanga,Dodoma,Tabora, Kigoma lakini kwenye mpango wa sasa uwanja huu haumo.
Ni nani anayeupiga vita. Rais kwa hili tunaomba uingilie kati kwa jinsi utakavyoona inafaa. Aidha barabara njia nne za kuingia jijini zimetupiliwa mbali hakuna anayezungumzia kwenye Mpango. Nadhani miji kama Mwanza Mbeya ni wakati wa kujenga njia nne kama ilivyo kwa Dar.
Kura ziko nyingi sana kwenye maeneo haya siyo ya kufanyia mzaha. Makonda pata maelezo ya miradi hii uondoe lawama.