#COVID19 Kampuni ya kutengeneza chanjo za COVID-19, Moderna inatarajia kuanza majaribio ya Chanjo za UKIMWI mwezi huu

Zile mipira za zamani za bure toka family plan ndo zilikuwa ziantembea balaa,ila hizi za kununua naona nyingi zinaozea Dukani hazina wateja sana.

Sasa hivi hazitakuja kabisa hata huko madukani. Huku kwetu wengi tena wachache wanazitumia kwa kuepuka ukimwi sio mimba wala magonjwa ya zinaa.
 
Kwani na yenyewe mwendazake aliitilia mashaka? Shida ya hi ya corona, tuweni tu wa kweli, wataalamu wetu walichangia sana kuhusu haya mashaka ambayo kina Gwajima wanayasema sasa hivi, wanataka tu kumuangushia jumba bovu Gwajima but ukweli ni kwamba haya mambo yameanzia wizarani na Ikulu, wasitufanye wajinga. Wamefanya interview TBC, Wasafi na hata youtubes, kote huko clips zao zipo, leo wanataka kumlaumu askofu wa Ubungo? Watutake radhi kabisa
Chanjo ya korona haipingwi na watanzania pekeee malekani walikutana lini na Magufuli? Mbona wanaipinga au hamwoni? Ulaya walikutana lini na Gwajima mbona wanaipinga? Maoni ya watu hata Kama hawako sahihi yaheshimiwe! Anayefaidi matumizi ya chanjo ni nani kati ya Tanzania na USA? USA anafaidi kiuchumi directly kwa kuuza dawa na kulinda afya za watu wake, Kama asingekuwa na heshima kwa maoni ya watu bila shaka wale wanaipinga na kueneza propaganda za kupinga chanjo wangekuwa gerezani na kesi za kuhujumu uchumi.
 
Back
Top Bottom