#COVID19 Juhudi za Rais Xi kuhusu ushirikiano kwenye mapambano dhidi ya COVID-19 zazaa matunda

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
MAIN202006301712000054758986122.jpg

VCG111341472162.png

Wiki chache zilizopita zimeshuhudia ongezeko la usambazaji wa chanjo za covid-19, hasa kwa nchi zinazoendelea. Foleni ndefu za watu wanaojipanga kupewa chanjo zinaendelea katika vituo vingi vya afya.

Nchi za kipato cha chini, hasa kutoka barani Afrika, kwa miezi kadhaa zimekuwa katika hali ya sintofahamu kutokana na upungufu wa chanjo, huku ukiritimba wa chanjo ukichukua usukani. Hii ni licha ya ukweli kwamba mataifa tajiri yaliahidi msaada wa pamoja.

Hali hiyo ilipokelewa kwa masikitiko huku pengo la chanjo kati ya mataifa tajiri na nchi masikini likiongezeka. Shinikizo liliongezeka, na mataifa yaliyoendelea yakaombwa kuacha kutoa ahadi hewana badala yake kuchukua hatua za haraka kuokoa hali.

Wakati haya yakiendelea, China, chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping imekuwa ikipigania ushirikino katika mapambano dhidi ya covid-19 na ilitoa ahadi ya kutoa msaada ambao ungesaidia mataifa masikini.

Tangu janga la Covid-19 lilipotokea, China imeonyesha kuwa inachukulia kwa umuhimu mkubwa ushirikiano katika vita dhidi ya virusi hivyo. Pamoja na upatikanaji wa chanjo, China iliahidi usambazaji sawa wa chanjo ya covid-19 kote duniani.

Mbali na hilo, Rais Xi amekuwa akisisitiza kuwa China itatimiza wajibu wake kama nchi kubwa, na hivyo kupigania ushirikiano katika utoaji wa chanjo lilikuwa ni suala la kipaumbele.

Rais Xi aliendelea kuzihakikishia nchi za Afrika kwamba China itaendelea kuunga mkono hatua za kudhibiti Covid-19 barani. China ilinuia kufanya hivyo kupitia utoaji wa msaada wa kiufundi na vifaa vinavyohitajika ili kupambana na virusi barani Afrika. China imekuwa ikitoa chanjo kwa nchi zinazoendelea, na hadi kufikia sasa imesafirisha chanjo kwa zaidi ya nchi 80 masikini kwa mahitaji ya haraka.

Kwa sasa, nchi za Afrika, Asia, na Amerika ya Kusini zinanufaika kwa mamilioni ya dozi za chanjo za Sinopharm na Sinovac.

Ni dhahiri kuwa chanjo kutoka China kuelekea hadi sehemu nyingine duniani, ilichelewa kwa sababu ya kuchelewa kutolewa idhini ya chanjo zake na shirika la afya duniani (WHO). Rais Xi aliahidi kila mara kuhakikisha "utengenezaji na usambazaji wa chanjo ya COVID-19, na mara itakapopatikana, itatumika kwa manufaa ya binadamu,"

Kwa kutimiza ahadi hii, mwezi Mei, baada ya chanjo iliyotengenezewa na kampuni ya Sinopharm kuidhinishwa kwa matumizi ya dharura, China mara moja ilitoa mchango wa chanjo hiyo nchi zilizoruhusu kutumika kwa raia wake.

Aidha, China iliziagiza kampuni zake za kutengeneza chanjo kuhamishia teknolojia katika nchi zinazoendelea kwa lengo la kuimarisha uzalishaji wa pamoja. Akisema hatua "Hii itakuwa mchango wa China katika kuhakikisha upatikanaji wa chanjo na kwa gharama nafuu kwa nchi zinazoendelea".

Muda mfupi baadaye, chanjo kutoka China iliongezwa kwenye mpango wa COVAX, ambao unatoa chanjo hasa kwa nchi maskini, na ambazo zinakabiliwa na matatizo ya upatikanaji wa chanjo.

Kiongozi huyo wa China aliendeleza mapambano dhidi ya kile alichokitaja kama utaifa wa chanjo na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutafuta suluhisho kwa masuala yanayohusu uwezo wa uzalishaji na usambazaji wa chanjo, ili kuwezesha upatikanaji wa chanjo kwa urahisi katika nchi zinazoendelea. Alifanya hivyo huku akiahidi kutoa dola bilioni 3 za Marekani kama msaada wa kimataifa kwa nchi zinazoendelea kusaidia kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 na kusaidia kufufua uchumi katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Itakumbukwa pia kwamba msaada wa China kwa Afrika wakati wa janga la kiafya la sasa unajumuisha misaada ya kusitisha ulipaji wa madeni kulingana na makubaliano ya kundi la G20 na ule wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Si hayo tu, msaada wa serikali ya China kwa Afrika ulidhihirika kupitia ujenzi wa makao makuu ya Kituo cha Afrika cha Kudhibiti Magonjwa Africa CDC jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Wakati huo huo, kiongozi huyo alitangaza kuwa China itatoa dozi bilioni mbili za chanjo ya COVID-19 kwa ulimwengu kwa mwaka mzima na kutoa dola milioni 100 za Marekani kwa mpango wa COVAX. Hii, kwa mujibu wa Xi, hii ni katika juhudi za kujenga jamii yenye mustakabali wa pamoja kwa binadamu.

Kampeni yake ilikuwa na mafanikio kwani hatimaye nchi tajiri zimeanza kuelekeza msaada wao kwa mataifa yenye mahitaji makubwa. Kwa sasa, usafirishaji wa chanjo barani Afrika umeongezeka, kwa karibu mara mia moja.

Nchi kama vile Marekani, Uingereza, Ufaransa, Denmark, Urusi, India, na UAE zimeanza kutoa michango barani Afrika, na kutoa matumaini kwa mamilioni ya watu ambao maisha yao yako hatarini.

Ama kwa kweli, hatua za haraka za serikali ya Rais Xi kuipa Afrika vifaa vya matibabu ikiwa ni pamoja na vifaa vya kupima, vifaa binafsi vya kujiinga (PPEs), na dawa za kusaidia mapambano, mara tu baada ya kutokea kwa virusi vya corona ni jambo la kupongezwa.
 
Back
Top Bottom