Kampuni ya Huawei yatumia teknolojia yake kusaidia nchi za Afrika katika kuhifadhi matumbawe na wanyamapori

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,035
VCG31N1259073932.jpg


Uhifadhi wa mazingira ya baharini na nchi kavu ni jukumu ambalo binadamu wanapaswa kulitia maanani sana. Tunafahamu kuwa bila kuwa na mazingira mazuri wanyama na binadamu wote watakuwa hatarini. Katika kutimiza wito huo, kampuni kubwa ya teknolojia ya China, Huawei, imekuwa katika harakati na kampeni yake ya kusaidiana na nchi za Afrika ili kuhakikisha mazingira ya baharini ambayo ni chanzo kikuu cha uchumi wa buluu, na mazingira ya nchi kavu ambayo yanahifadhi wanyama na binadamu yanakuwa salama.

Hivi karibuni kampuni ya Huawei, ikishirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira (IUCN) na washirika wengine wakisaidiana na jamii za wenyeji nchini Mauritius, wamekuwa wakitekeleza mradi wa uhifadhi wa matumbawe. Katika nchi nyingi kumekuwa kukishuhudiwa wimbi la uharibifu wa matumbawe baharini. Matatizo makubwa kwa matumbawe, iwe kwa eneo fulani maalum au kwa dunia nzima, yanaibua maswali mazito kuhusu mustakabali wa matumbawe haya.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa awamu mpya ya mradi, waziri wa uchumi wa bluu, rasilimali za baharini, uvuvi na usafirishaji baharini wa Mauritius Sudheer Maudhoo, alisema kama sehemu ya mradi wa ‘Tech4Nature Mauritius’, vipande 25,000 vya matumbawe vilikuzwa kwa mafanikio katika vitalu na kupandwa katika eneo la kilomita za mraba 1.01.

Ili kufuatilia uhamaji wa viumbe kwenye maeneo ya urejeshaji wa matumbawe na kuondoa changamoto ambazo zinazuia kuzaliana kwa mafanikio, hapo ndipo kampuni ya Huawei ya China inapoingiza mkono wake, kwani inaona kuwa suluhu nzuri ni kujumuisha kamera, GPS na 4G katika mradi huo. Aidha matumizi ya akili bandia (AI) ni muhimu katika kutoa mwelekeo wa uhifadhi, kusaidia utafiti wa wanabiolojia baharini, na kuelimisha umma juu ya umuhimu wa uhifadhi na urejeshaji wa matumbawe.

Nchini Tanzania, wataalamu wa sayansi ya baharini wanasema kwamba matumbawe katika mwambao wa Tanzania, hasa kisiwani Zanzibar kwa sasa yanakabiliwa na hatari ya kutoweka kutokana na kukithiri kwa uchafuzi wa mazingira, ikiwemo kwenye maeneo ya fukwe. Iwapo hatua za haraka za kukabilina na athari hizo hazitachukuliwa, janga kubwa la kimazingira linaweza kutokea na hivyo kuathiri shughuli za kiuchumi na ustawi wa jamii, kwa vile matumbawe hivi sasa yanafaida kubwa katika nyanja hizo.

Kwa kuzingatia hilo kampuni ya Huawei, inaona ni bora mradi huu ukitekelezwa na maeneo mengine ambayo matumbawe yake yako hatarini kutoweka kama vile Zanzibar, ambapo faida yake kubwa ni kwamba itakata kiu na kukidhi mahitaji ya watalii, lakini wakati huohuo mradi utakuwa na kazi ya kulinda matumbawe.

Wakazi wengi wa maeneo ya pwani wamekuwa wakitegemea bahari kwa matumizi ya kila siku. Hivyo kulinda mazao ya baharini yakiwemo matumbawe ni suala ambalo linatakiwa kupewa msisitizo, kwa maana hiyo wakazi ama wananchi wanapaswa kupewa elimu ya kutosha ya kulinda mazingira ya baharini.

Mbali na kuangazia uhifadhi wa bahari, kampuni ya Huawei pia inajikita katika kuongeza msaada wake kwenye programu za uhifadhi wa wanyama pori barani Afrika. Kwa kutumia teknolojia yake ya 5G inawezesha ufuatiliaji wa wanyama walio katika hatari ya kutoweka. Huawei inatumia jukwaa lake la teknolojia ya 5G kutoa taarifa moja kwa moja kwa wahifadhi ili kuweza kufuatilia mienendo ya wanyama na kuchukua hatua haraka endapo wanayama hao wanakabiliwa na hali yoyote ya hatari.

Katika juhudi zake, Huawei imewekeza zaidi ya shilingi milioni 100 za Kenya katika programu za kuhifadhi wanyamapori nchini Kenya ndani ya kipindi cha muongo mmoja na nusu uliopita. Teknolojia ya 5G, inathibitisha kuwa ni muhimu sana kwa wahifadhi kuweza kufuatilia wanyamapori katika bara la Afrika. Kwa kutumia kamera ya 5G, wataalam wa uhifadhi wanaweza kuwaona wanyamapori katika harakati zao zote na kusaidia kuzuia matukio mabaya kama vile ujangili.

Pengwini wa Afrika, ambao wanazaliana sana katika Pwani ya Cape nchini Afrika Kusini, wameorodheshwa kama ndege walio hatarini kutoweka na Shirika la Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN). Lakini sasa kutokana na kufungwa vifaa vya 5G vya kampuni ya Huawei, ndege hawa wanaweza kufuatiliwa moja kwa moja na kuongeza idadi yao. Sanjari na hilo, teknolojia hii sio tu inawafanya watalii kupata fursa ya kufurahia pengwini wa kipekee, bali pia kuonesha 5G kuwa ni teknolojia yenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi mazingira.
 

Attachments

  • VCG111439134933.jpg
    VCG111439134933.jpg
    120.6 KB · Views: 5
Back
Top Bottom