Ushirikiano unahitajika zaidi sasa katika kuwalinda wanyamapori walio hatarini

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,032
VCG111409817920.jpg



Siku ya wanyamapori duniani ambayo inaangukia Machi 3 kila mwaka, ni muhimu sana kwani katika siku hii tunapata muda wa kukumbushana uzuri na maajabu ya mimea na wanyamapori waliomo ndani ya sayari yetu lakini vilevile umuhimu wa viumbe hivi duniani.

Mbali na wajibu tulionao wa kudumisha na kuiendeleza dunia yetu, binadamu hutegemea bidhaa na huduma muhimu ambazo zinatokana na mazingira ya asili, kuanzia chakula na maji safi hadi udhibiti wa uchafuzi wa mazingira na hewa ya kaboni au ukaa. Lakini cha kusikitisha ni kwamba hivi sasa mazingira ya asili na wanyamapori wako hatarini. Robo ya aina za wanyama duniani zinakabiliwa na tishio la kutoweka, sababu kubwa ikiwa ni kuharibu karibu nusu ya ikolojia ambayo wanyama hao ndimo wanamoishi.

Ni juhudi gani zinazohitajika ili kuhakikisha tunawajali na kuwalinda wanyamapori?

China ni moja ya nchi zenye aina nyingi zaidi ya viumbe duniani. Katika miaka ya hivi karibuni, imeendelea kuboresha mfumo wake wa sheria na usimamizi wa ulinzi wa wanyamapori, kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimataifa katika ulinzi wa wanyamapori, kutekeleza kwa nguvu ulinzi wa makazi ya wanyamapori na kuokoa uzalishaji wao, ikiwa ni pamoja na kuwarejesha wanyamapori katika mazingira ya asili, kulinda kwa ufanisi asilimia 90 ya aina za mimea na mazingira ya ardhi, na asilimia 85 ya makundi ya wanyamapori muhimu. Idadi ya wanyamapori walio hatarini kutoweka kama vile panda, ndege aina ya ibis, swala wa Tibet na mimea aina ya cycads imefanikiwa kurejeshwa.

Tangu miaka ya 80 ya karne iliyopita, China imeongeza kasi ya ujenzi wa hifadhi za asili, ambapo kwa sasa idadi ya hifadhi hizo imefikia 2,750. Wakati huo huo aina zaidi ya 300 za wanyamapori walioko hatarini kutoweka zimefanikiwa kuzalishwa kwa msaada wa binadamu, na aina zaidi ya 10 za wanyama zimerejeshwa katika mazingira ya asili.

Mwezi Mei mwaka juzi ulifanyika mjadala kule Geneva, Uswisi, kuhusu kila nchi kuwa na hazina maalumu ya kushughulikia na kuwalinda wanyama hasa katika nyakati za majanga, kama vile ukame kiangazi, mafuriko tetemeko la ardhi, maporomoko ya udongo, sanjari na hayo pia na kuwalinda na magonjwa.

Ni kwanini hadi leo bado kuna mgogoro kati ya binadamu na wanyamapori?

Tunafahamu kuwa wanyamapori wengi mathalan tembo wana tabia ya kuondoka kwenye hifadhi zao na kuvamia kwenye makazi ya watu wakiwa na lengo la kujitafutia chakula na maji, jambo ambalo limekuwa likiwabughudhi wakazi wanaoishi karibu na hifadhi za wanyama hao. Lakini tatizo hili limesababishwa na binadamu wenyewe kwani wao ndio wameanza kuvamia makazi ya wanyamapori kwa kujenga nyumba na kuanzisha mashamba ya kilimo, hivyo Ili kuondoa kero hiyo, Tanzania ambayo inasifika kwa utajiri wa rasilimali za wanyamapori, imeamua kutatua mgogoro wa binadamu na wanyamapori, kwa sababu imekuwa ikishuhudia takriban watu 50 wakiuawa na zaidi ya ekari 5,000 za mazao shambani kuharibiwa na wanayamapori kila mwaka. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja anasema pamoja na mbinu nyingine pia wameanzisha vituo maalumu vya askari ili kuangalia wanyama kwenye kingo wanazotokea na kuwazuia wasilete uharibifu kwenye makazi ya watu.

Mamlaka za usimamizi wa wanyamapori zinakabiliwa na changamoto gani zinapowalinda wanyamapori?

Changamoto kubwa inayowakabili askari wa ulinzi wa wanyamapori wakati wakitimiza majukumu yao ya doria ni majangili. Mbali na kushuhudia wanyamapori wakiuliwa na majangili hawa ili kupata meno, mkia au hata nyama, maafisa hawa wa ulinzi pia wanauliwa ama kujeruhiwa wakati wakipambana na majangili. Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA) Yussuf Kabange aliwaasa wananchi wanaovamia makazi ya wanyamapori na majangili kwa ujumla akiwataka kufuata sheria ya uhifadhi wa wanyamapori.

“Wananchi wanapaswa kuheshimu sheria namba 5 inayozuia shughuli za kibinadamu ndani ya maeneo ya hifadhi”.
 
Hapo Guangzhou na Shanghai mumeacha kununua kimagendo pembe za faru na ndovu? Maana mliwamaliza wanyama wa Afrika.
 
Back
Top Bottom