Kampuni ya Hall of Fame Boxing yaishtaki Azam Media, yataka ilipwe Tsh. Bilioni 2 kwa kurusha maudhui kinyume na mkataba

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Kampuni ya Azam Media inashtakiwa Mahamani na Kampuni ya 'Hall of Fame Boxing and Promotion' ambayo inajihusisha na uandaaji wa mapambano ya ngumi za kulipwa wakiitaka iwalipe kiasi cha pesa Tsh. Bilioni 2 kwa kurusha hewani maudhui yao kwenye kipindi kinyume na makubaliano.

Katika kesi hiyo ya madai namba 100/2023 inayosikilizwa kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam waleta maombi hao wanadai Azam Media ilikiuka makubaliano ya kimkataba kwa kurusha maudhui kwenye kipindi (pambano la Hassan Mwakinyo dhidi ya Arnel Tinampay raia wa Uphilipino sambamba na pambano la Twaha Kiduku na Dulla Mbabe) bila haki miliki ya maudhui hayo.

Inadaiwa makubaliano ya kimkataba yaliyokuwepo baina ya wadai hao na Kampuni ya Azam Media ni kurusha mapambano hayo mubashara (live) tu, lakini wanadai Azam Media waliendelea kurusha marudio mapambano hayo kwa nyakati tofauti jambo kinyume na makubaliano yaliyokuwepo, ambapo wanadai Azam Media waliendelea kunufaika na maudhui hayo jambo ambalo linawasukuma kudai fidia hiyo.

Katika madai hayo Azam Media wanatuhumiwa kurusha maudhui yenye kuonesha mapambano hayo bila kuweka 'logo' ya waandaji wa mapambano husika jambo wanadai linakiuka utaratibu makubaliano yao kuhusu haki miliki ya maudhui hayo.

Upande wa waleta maombi unadai hatua na uamuzi wa kufika Mahakamani ulikuja baada kupitia kwenye vyombo mbalimbali ikiwemo COSOTA na TCRA .

Wadai hao wanadai walichukua uamuzi huo baada ya kuiandikia barua Taasisi ya Haki Miliki Tanzania (COSOTA) kuhusu tuhuma dhidi ya Azam Media kurusha maudhui hayo nje ya makubaliano na bila kuweka alama ya utambulisho wao inayolinda haki miliki.

Katika taarifa ya COSOTA iliyoeleza majibu ya mwisho, ilieleza baada ya kupokea madai hayo waliandaa kikao cha usuluhishi ambacho akikuzaa muafaka ambapo Kampuni ya Azam Media walikataa hawakurusha maudhui hayo kama ilivyodaiwa na walalamikaji.

Barua ya COSOTA ilieleza baada kushindwa kupata ukweli wa mgogoro huo Hall of Fame na Azam Media kutokana na COSOTA kutokuwa na mitambo ya kuweza kutambua maudhui gani yamerushwa na yamerushwa wapi na saa ngapi.

Kushindwa kwake kulielezwa kulikuja baada COSOTA kufanya mawasiliano na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia barua inavyodaiwa kutumwa Agosti 23, 2021 ili kuweza kupata rekodi ya maudhui ya kipindi kilichokuwa kikilalamikiwa.

Hata hivyo, katika barua hiyo ya majibu kwa mlalamikaji inaeleza TCRA hawakuweza kupata rekodi hiyo kutokana na kilichodaiwa ni takwa la kisheria lililoeleza kuwa ilitakiwa malalamiko hayo kuwasilishwa kwao ndani ya miezi sita ili TCRA iweze kuyashughulikia kwa mujibu wa sheria.

Ambapo maelezo yaliyodaiwa ni majibu kutoka TCRA yalidai mlalamikiwa hawajibiki kutunza taarifa zilizoombwa nje ya miezi sita kwani zipo nje ya muda, lakini imeeleza TCRA haikuweza kupata taarifa za kuthibitisha suala hilo kwa njia nyingine.

Kufuatia madai hayo Kampuni ya Hall of Fame kupitia wanasheria wake iliamua kufikisha suala hilo mahakamani ili kupata tafsiri za kisheria zaidi katika chombo hicho kilichopewa mamlaka ya juu katika kutafsiri sheria nchini.

Baada ya kesi hiyo kufikishwa mahakamani zimefanyika taratibu za kisheria kuleta upatashi (Mediation) baina ya pande hizo mbili lakini bado jambo hilo alikufikia muafaka, kwahiyo Septemba 18, 2023 kesi ya msingi ya baina ya Kampuni ya Hall of Fame na Kampuni ya Azam Media inatarajiwa kusikilizwa kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Ikumbukwe kesi yenye mwelekeo wa aina hiyo sio mara ya kwanza kuikumba Kampuni ya Azam Media ambapo kwa siku za hivi karibuni, Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo alitinga mahakamani kuishtaki kampuni hiyo kwa kurusha maudhui yenye taswira yake (images) bila kumshirikisha wala kuwa na haki miliki.

Hata hivyo inadaiwa kesi hiyo muafaka wake umefikiwa kwenye hatua za upatashi (mediation) mbele ya Mahakama baina ya wanasheria waliokuwa wakimuwakilisha Bondia huyo pamoja na wa Kampuni ya Azam Media.

Kwa kipindi cha hivi karibuni Kampuni ya Azam Media kupitia Chanel zake za michezo imekuwa ikirusha mapambano tofauti tofauti ya ngumi hususani kuyarusha mapambano hayo mubashara na baadae kurusha marudio yake.

Mchezo wa ngumi nchini Tanzania kwa siku za hivi karibuni umekuwa maarufu ambapo watu wengi wameonekana kuvutiwa hususani lika la vijana ikilinganishwa na awali.
CamScanner 10-10-2022 09.04_page-0001.jpg

CamScanner 10-10-2022 09.04_page-0002.jpg

CamScanner 10-10-2022 09.04_page-0003.jpg

HoF vs Azam proof of service of summons-WSD_page-0001.jpg

HoF vs Azam proof of service of summons-WSD_page-0002.jpg
 
Tumezoea kufanya mambo kimazoea sana. Azam Media wanafanya kazi kimazoea mno.

Hata hizi timu zikianza nongwa tutaona mengi. Watangazaji wao nao wajuaji sana. Yule Nyambela mara atangaze ngumi, mara mpira wa miguu; sasa hapo utaacha kuharibikiwa.

Hili suala lazima watawalipa tu.
 
Azam media ndio wanaoleta chachu kwenye michezo lakini pamoja na umuhimu huo wasi take advantage kirahisi tu. Hizi zama hakuna anayetaka kuwa ndugu mtazamaji tu wengine wakipiga pesa.

Wajitahidi kushirikisha wadau kabla ya kurusha matangazo yao na njia rahisi ni kuingia mikataba ya muda mrefu na taasisi au mtu watakayeshirikiana nae kwenye ngumi. Risks zote zibakie kwa promota na haki zote wanunue kwa promota.
 
Kama walalamikaji hawakutunza record basi wasiitegemee record kutoka TCA. Hao ni dugu inakuwa moja, kufuatia ukubwa media yenyewe. Labda iwe imetengalenezwa mchongo.

Halafu hapo imeelezwa mchezo wa ngumi siku za hivi karibuni umekuwa ukipendwa, sababu kubwa ya kufikiwa kupendwa ni ksbb ya Azam kuchukua hatua za makusudi kuubeba kuutangaza. Hivyo muda mwingine wangekuwa wanafikia nae maelewano tu nje ya mahakama. Anaweza akaamua kusitisha kuupromot huo mchezo ukarudi nyuma kabisa na ukaachwa kama zamani. Wawe makini na tamaa za pesa za ghafla.
 
Kampuni ya Azam Media inashtakiwa Mahamani na Kampuni ya 'Hall of Fame Boxing and Promotion' ambayo inajihusisha na uandaaji wa mapambano ya ngumi za kulipwa wakiitaka iwalipe kiasi cha pesa Tsh. Bilioni 2 kwa kurusha hewani maudhui yao kwenye kipindi kinyume na makubaliano.

Katika kesi hiyo ya madai namba 100/2023 inayosikilizwa kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam waleta maombi hao wanadai Azam Media ilikiuka makubaliano ya kimkataba kwa kurusha maudhui kwenye kipindi (pambano la Hassan Mwakinyo dhidi ya Arnel Tinampay raia wa Uphilipino sambamba na pambano la Twaha Kiduku na Dulla Mbabe) bila haki miliki ya maudhui hayo.

Inadaiwa makubaliano ya kimkataba yaliyokuwepo baina ya wadai hao na Kampuni ya Azam Media ni kurusha mapambano hayo mubashara (live) tu, lakini wanadai Azam Media waliendelea kurusha marudio mapambano hayo kwa nyakati tofauti jambo kinyume na makubaliano yaliyokuwepo, ambapo wanadai Azam Media waliendelea kunufaika na maudhui hayo jambo ambalo linawasukuma kudai fidia hiyo.

Katika madai hayo Azam Media wanatuhumiwa kurusha maudhui yenye kuonesha mapambano hayo bila kuweka 'logo' ya waandaji wa mapambano husika jambo wanadai linakiuka utaratibu makubaliano yao kuhusu haki miliki ya maudhui hayo.

Upande wa waleta maombi unadai hatua na uamuzi wa kufika Mahakamani ulikuja baada kupitia kwenye vyombo mbalimbali ikiwemo COSOTA na TCRA .

Wadai hao wanadai walichukua uamuzi huo baada ya kuiandikia barua Taasisi ya Haki Miliki Tanzania (COSOTA) kuhusu tuhuma dhidi ya Azam Media kurusha maudhui hayo nje ya makubaliano na bila kuweka alama ya utambulisho wao inayolinda haki miliki.

Katika taarifa ya COSOTA iliyoeleza majibu ya mwisho, ilieleza baada ya kupokea madai hayo waliandaa kikao cha usuluhishi ambacho akikuzaa muafaka ambapo Kampuni ya Azam Media walikataa hawakurusha maudhui hayo kama ilivyodaiwa na walalamikaji.

Barua ya COSOTA ilieleza baada kushindwa kupata ukweli wa mgogoro huo Hall of Fame na Azam Media kutokana na COSOTA kutokuwa na mitambo ya kuweza kutambua maudhui gani yamerushwa na yamerushwa wapi na saa ngapi.

Kushindwa kwake kulielezwa kulikuja baada COSOTA kufanya mawasiliano na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia barua inavyodaiwa kutumwa Agosti 23, 2021 ili kuweza kupata rekodi ya maudhui ya kipindi kilichokuwa kikilalamikiwa.

Hata hivyo, katika barua hiyo ya majibu kwa mlalamikaji inaeleza TCRA hawakuweza kupata rekodi hiyo kutokana na kilichodaiwa ni takwa la kisheria lililoeleza kuwa ilitakiwa malalamiko hayo kuwasilishwa kwao ndani ya miezi sita ili TCRA iweze kuyashughulikia kwa mujibu wa sheria.

Ambapo maelezo yaliyodaiwa ni majibu kutoka TCRA yalidai mlalamikiwa hawajibiki kutunza taarifa zilizoombwa nje ya miezi sita kwani zipo nje ya muda, lakini imeeleza TCRA haikuweza kupata taarifa za kuthibitisha suala hilo kwa njia nyingine.

Kufuatia madai hayo Kampuni ya Hall of Fame kupitia wanasheria wake iliamua kufikisha suala hilo mahakamani ili kupata tafsiri za kisheria zaidi katika chombo hicho kilichopewa mamlaka ya juu katika kutafsiri sheria nchini.

Baada ya kesi hiyo kufikishwa mahakamani zimefanyika taratibu za kisheria kuleta upatashi (Mediation) baina ya pande hizo mbili lakini bado jambo hilo alikufikia muafaka, kwahiyo Septemba 18, 2023 kesi ya msingi ya baina ya Kampuni ya Hall of Fame na Kampuni ya Azam Media inatarajiwa kusikilizwa kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Ikumbukwe kesi yenye mwelekeo wa aina hiyo sio mara ya kwanza kuikumba Kampuni ya Azam Media ambapo kwa siku za hivi karibuni, Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo alitinga mahakamani kuishtaki kampuni hiyo kwa kurusha maudhui yenye taswira yake (images) bila kumshirikisha wala kuwa na haki miliki.

Hata hivyo inadaiwa kesi hiyo muafaka wake umefikiwa kwenye hatua za upatashi (mediation) mbele ya Mahakama baina ya wanasheria waliokuwa wakimuwakilisha Bondia huyo pamoja na wa Kampuni ya Azam Media.

Kwa kipindi cha hivi karibuni Kampuni ya Azam Media kupitia Chanel zake za michezo imekuwa ikirusha mapambano tofauti tofauti ya ngumi hususani kuyarusha mapambano hayo mubashara na baadae kurusha marudio yake.

Mchezo wa ngumi nchini Tanzania kwa siku za hivi karibuni umekuwa maarufu ambapo watu wengi wameonekana kuvutiwa hususani lika la vijana ikilinganishwa na awali.
Watanzania mnapaswa kuelewa kuwa COSOTA ni mshirika mkubwa wa piracy nchini.

TCRA hawana la kujitetea kwenye hili, ingekuwa ishu ya msanii katukana wangetoa hata kama ingekuwa kipindi kimerushwa zaidi ya mwaka
 
Kama walalamikaji hawakutunza record basi wasiitegemee record kutoka TCA. Hao ni dugu inakuwa moja,kufuatia ukubwa media yenyewe. Labda iwe imetengalenezwa mchongo

Halafu hapo imeelezwa mchezo wa ngumi siku za hivi karibuni umekuwa ukipendwa ,sababu kubwa ya kufikiwa kupendwa ni ksbb ya Azam kuchukua hatua za makusudi kuubeba kuutangaza. Hivyo muda mwingine wangekuwa wanafikia nae maelewano tu nje ya mahakama. Anaweza akaamua kusitisha kuupromot huo mchezo ukarudi nyuma kabisa na ukaachwa kama zamani. Wawe makini na tamaa za pesa za ghafla
Haya ndio mazoea ya kijinga. Inakuwaje Azam anavunja mkataba ambao upo wazi. Anavyopromoti ngumi tambua na yeye anaingiza hela no free lunch ndugu. Wadai lazima wamejipanga wana kila aina ya ushahidi ndio maana wanataka 2B.
 
Watanzania mnapaswa kuelewa kuwa COSOTA ni mshirika mkubwa wa piracy nchini.

TCRA hawana la kujitetea kwenye hili, ingekuwa ishu ya msanii katukana wangetoa hata kama ingekuwa kipindi kimerushwa zaidi ya mwaka
COSOTA hapa anaingiaje ama TCRA? Ebu fafanua
 
Yaani TBC wanavyo vipindi vilivyorekoriwa tangu enzi za Uhuru ndo unaiambie kuwa hiko kipindi hakipo TCRA.

Rushwa mbaya sana
 
Haya ndio mazoea ya kijinga. Inakuwaje Azam anavunja mkataba ambao upo wazi. Anavyopromoti ngumi tambua na yeye anaingiza hela no free lunch ndugu. Wadai lazima wamejipanga wana kila aina ya ushahidi ndio maana wanataka 2B.
Mimi sio azam ndugu. Pambaneni utaleta mrejesho kama mmezichota hizo 2B. Labda kama hawajalishwa zile fitina za ccm
 
Kampuni ya Azam Media inashtakiwa Mahamani na Kampuni ya 'Hall of Fame Boxing and Promotion' ambayo inajihusisha na uandaaji wa mapambano ya ngumi za kulipwa wakiitaka iwalipe kiasi cha pesa Tsh. Bilioni 2 kwa kurusha hewani maudhui yao kwenye kipindi kinyume na makubaliano.

Katika kesi hiyo ya madai namba 100/2023 inayosikilizwa kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam waleta maombi hao wanadai Azam Media ilikiuka makubaliano ya kimkataba kwa kurusha maudhui kwenye kipindi (pambano la Hassan Mwakinyo dhidi ya Arnel Tinampay raia wa Uphilipino sambamba na pambano la Twaha Kiduku na Dulla Mbabe) bila haki miliki ya maudhui hayo.

Inadaiwa makubaliano ya kimkataba yaliyokuwepo baina ya wadai hao na Kampuni ya Azam Media ni kurusha mapambano hayo mubashara (live) tu, lakini wanadai Azam Media waliendelea kurusha marudio mapambano hayo kwa nyakati tofauti jambo kinyume na makubaliano yaliyokuwepo, ambapo wanadai Azam Media waliendelea kunufaika na maudhui hayo jambo ambalo linawasukuma kudai fidia hiyo.

Katika madai hayo Azam Media wanatuhumiwa kurusha maudhui yenye kuonesha mapambano hayo bila kuweka 'logo' ya waandaji wa mapambano husika jambo wanadai linakiuka utaratibu makubaliano yao kuhusu haki miliki ya maudhui hayo.

Upande wa waleta maombi unadai hatua na uamuzi wa kufika Mahakamani ulikuja baada kupitia kwenye vyombo mbalimbali ikiwemo COSOTA na TCRA .

Wadai hao wanadai walichukua uamuzi huo baada ya kuiandikia barua Taasisi ya Haki Miliki Tanzania (COSOTA) kuhusu tuhuma dhidi ya Azam Media kurusha maudhui hayo nje ya makubaliano na bila kuweka alama ya utambulisho wao inayolinda haki miliki.

Katika taarifa ya COSOTA iliyoeleza majibu ya mwisho, ilieleza baada ya kupokea madai hayo waliandaa kikao cha usuluhishi ambacho akikuzaa muafaka ambapo Kampuni ya Azam Media walikataa hawakurusha maudhui hayo kama ilivyodaiwa na walalamikaji.

Barua ya COSOTA ilieleza baada kushindwa kupata ukweli wa mgogoro huo Hall of Fame na Azam Media kutokana na COSOTA kutokuwa na mitambo ya kuweza kutambua maudhui gani yamerushwa na yamerushwa wapi na saa ngapi.

Kushindwa kwake kulielezwa kulikuja baada COSOTA kufanya mawasiliano na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia barua inavyodaiwa kutumwa Agosti 23, 2021 ili kuweza kupata rekodi ya maudhui ya kipindi kilichokuwa kikilalamikiwa.

Hata hivyo, katika barua hiyo ya majibu kwa mlalamikaji inaeleza TCRA hawakuweza kupata rekodi hiyo kutokana na kilichodaiwa ni takwa la kisheria lililoeleza kuwa ilitakiwa malalamiko hayo kuwasilishwa kwao ndani ya miezi sita ili TCRA iweze kuyashughulikia kwa mujibu wa sheria.

Ambapo maelezo yaliyodaiwa ni majibu kutoka TCRA yalidai mlalamikiwa hawajibiki kutunza taarifa zilizoombwa nje ya miezi sita kwani zipo nje ya muda, lakini imeeleza TCRA haikuweza kupata taarifa za kuthibitisha suala hilo kwa njia nyingine.

Kufuatia madai hayo Kampuni ya Hall of Fame kupitia wanasheria wake iliamua kufikisha suala hilo mahakamani ili kupata tafsiri za kisheria zaidi katika chombo hicho kilichopewa mamlaka ya juu katika kutafsiri sheria nchini.

Baada ya kesi hiyo kufikishwa mahakamani zimefanyika taratibu za kisheria kuleta upatashi (Mediation) baina ya pande hizo mbili lakini bado jambo hilo alikufikia muafaka, kwahiyo Septemba 18, 2023 kesi ya msingi ya baina ya Kampuni ya Hall of Fame na Kampuni ya Azam Media inatarajiwa kusikilizwa kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Ikumbukwe kesi yenye mwelekeo wa aina hiyo sio mara ya kwanza kuikumba Kampuni ya Azam Media ambapo kwa siku za hivi karibuni, Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo alitinga mahakamani kuishtaki kampuni hiyo kwa kurusha maudhui yenye taswira yake (images) bila kumshirikisha wala kuwa na haki miliki.

Hata hivyo inadaiwa kesi hiyo muafaka wake umefikiwa kwenye hatua za upatashi (mediation) mbele ya Mahakama baina ya wanasheria waliokuwa wakimuwakilisha Bondia huyo pamoja na wa Kampuni ya Azam Media.

Kwa kipindi cha hivi karibuni Kampuni ya Azam Media kupitia Chanel zake za michezo imekuwa ikirusha mapambano tofauti tofauti ya ngumi hususani kuyarusha mapambano hayo mubashara na baadae kurusha marudio yake.

Mchezo wa ngumi nchini Tanzania kwa siku za hivi karibuni umekuwa maarufu ambapo watu wengi wameonekana kuvutiwa hususani lika la vijana ikilinganishwa na awali.
Kiukweli Azam hata kwa watazamaji tuakilalamika kuna vitu wanafanya siyo sawa kabisa. Una channel yao moja huwa ni matangazo tu na ni free kuna wakati walikuwa wanaleta movie na kuzima mpaka ulipie buku ndiyo uweze kuona program hiyo. Program ikiisha ndiyo wanarudisha ile free yao. Na kila mara wanaongeza bei ya vingamuzi .
 
Back
Top Bottom