Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Uzinduzi wa Mradi wa Minara ya Kurusha Matangazo ya Televisheni Ardhini(DTT) ya Kampuni ya Azam Media Limited, Makao Makuu ya Azam Media Limited- Tabata Dares Salaam leo tarehe 18 Mei, 2023.
Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kuongeza Fedha za Motisha kwa Yanga SC inayoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kutoka Tsh. Milioni 10 hadi Tsh. Milioni 20 kwa kila goli la ushindi.
Uamuzi huo unafuatia ushindi wa Magoli 4-1 dhidi ya Marumo Gallants FC ya Afrika Kusini ulioipeleka Yanga SC katika Fainali ikiwa ni Timu ya kwanza kutoka Tanzania kufanikiwa kufika hatua hiyo lakini amesisitiza kuwa fedha hizo zitatolewa ikiwa magoli yataipa ushindi timu.
Pia, Serikali imetoa ndege itakayobeba mashabiki na wachezaji kama Sehemu ya kuwatia moyo ili wafanye vizuri zaidi. Ndege hiyo itawapeleka, kuwasubiri na kuwarejesha.
Ameipongeza Azam kwa uwekezaji mkubwa waliofanya kwenye Sekta ya Habari na Mawasiliano. Teknolojia hii waliyoanzisha haitaongeza ubora wa picha pekee, bali pamoja na wingi wa chaneli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo wakati Mtoto Georgina Magesa (8) akiwa ameketi kwenye Kiti cha Rais mara baada ya kukutana naye katika hafla ya uzinduzi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Azam Media iliyofanyika katika Ofisi zao zilizopo katika Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya King’amuzi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Ndugu Abubakar Said Salim Bakhresa kwa ajili ya kuangalia maudhui mbalimbali ya Azam TV mara baada ya kuzindua mradi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni hiyo kwenye hafla iliyofanyika katika Ofisi zao zilizopo Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wafanyakazi wa Azam Media mara baada ya kufungua Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni hiyo kwenye hafla iliyofanyika katika Ofisi za Kampuni hiyo zilizopo Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2023.
Pia soma: Rais Samia kununua kila goli Tsh. Milioni 5 mechi za Simba, Yanga CAF