Shauri la Hall of Fame Boxing and Promotion dhidi ya Azam Media ushahidi kuaza kuwasilishwa kwa maandishi

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Kesi ya madai namba 100/2023 iliyofunguliwa na Kampuni ya 'Hall of Fame Boxing and Promotion' ambayo inajihusisha na uandaaji wa mapambano ya ngumi za kulipwa dhidi ya Azam Media imeendelea kusikilizwa Oktoba 24, 2023 ambapo Mahakama imeelekeza kuwa kesi hiyo itaendela kusikilizwa kwa njia ya maandishi kabla ya pande zote kufika Mahakamani Desemba 6, 2023.

Kwenye kesi hiyo walalamikaji wanahitaji Azam Media kuwalipa kiasi cha Shilingi Tsh.Bilioni 2 kwa kurusha maudhui yao kinyume na makubaliano ya kimkataba.

Katika kesi hiyo upande wa wadai wanawakilishwa na Wakili Winnie Kawanakamo kutoka ofisi ya 'ABC Attorneys' huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili kutoka Ofisi ya wanasheria 'Ndumbaro Advocates'.
 
Back
Top Bottom