Kampuni ya basi Sauli zinaadimika barabarani shida nini?

Kampuni ya basi Sauli zinaadimika barabarani shida nini?

Gari Zina warrant ya mwaka mmoja.
Life span ni miaka 3 in good condition zinaenda hadi miaka 7 hadi 10.
Faida zinarudi mapema kwa wingi wa mabus uliyonunua.
Mfano Scania moja unapata Mchina mbili moja ya mkopo so jumla siti 180 kwa siku.
Nauli ya elf 50 kwa mfano.
So scania anatoa gari moja anapata milion 3, mchina anatoa gari tatu kauza siti 180 kaingiza milion 9 kwa mwezi scania milion 90 Mchina milioni 270 toa gharama za uendeshaji ndani ya miezi 6 pesa imerudi kwa Mchina unakamata zingine sita.
Scania kurejesha milion 700 itahitaji miezi mingapi.
scania waranty yao ni km 150000 baada ya hapo utajua wewe,hiyo life span ya miaka 3 unasemea hizi scania ambazo ni full umeme alafu hesabu ya basi haiendi kama unavyorahisisha hapo
 
Ni mara ngapi unasikia household names kwenye biashara fulani zinakufa? Ni hotels ngapi au maduka mangapi makubwa on the par na kampuni kama Scandinavia, Hood au Sumry zimekufa?

Kwamba Scandinavia na hood hawakufanya research vizuri? Hadi leo hakuna basi linafikia Scandinavia kwa ubora wa huduma, hawa ndo walikua game changer. Kipindi kile ilikua bora upande hili basi kuliko ndege if you had that choice. Mtu unawaza likizo ifike upande Scandinavia uende mikoani na lilikua linapendeza kweli kweli na mwendo mzuri ila lilikufa kifo cha mende.

Dar express nasikia inapumulia machine, Mbunge Msukuma aliuza basi zake karibu zote. The list is endless mkuu, the writing is on the wall, hii ni biashara kichaa.
fatilia vizuri biashara nyingi za mabasi zilianza kuonekana biashara kichaa baada ya kuanzishwa kwa sumatra na sheria zao
 
Mkuu ungeweka na running cost ya hizo gari kwa mwaka ingelikuwa ni bora sana. Unaweza kuta scania anatumia kiasi kidogo sana kwenye matengenezo kwa mwaka kuliko mchina. Ila mchina kuwa road for 7 years haiwezekani labda awe branded na scania kwa baadhi ya vipuri
michina ya sasa hivi sio kama ile ya mwanzo saizi wameimprove upande wa spea zao hata upatikanaji saiz ni rahisi haina haja ya kupiga mixture na scania
 
Mchina baada ya miaka 3 engine ikizungua Huwa wanafunga ya scania p series au 124 so inakuwa engine msweden body mchina.
Mchina anatumia Cummins engine, Cummins engine haifanyi vizur sana kwenye soko.
Thus wengine wanazing'oa zikianza kusumbua wanafunga engine ya scania.
Running cost zingine zipo sawa ukitoa ya mafuta, Cummins engine inatumia mafuta kidogo kuliko scania.
Cost zingine za uendeshaji nje ya spare hazipishani.
Spea za mchina zimejaa tele kwa Bei chini lakini Sio durable.
So mchina anauzia body na finishing ya Ndani ndicho abiria wanapenda
mchina za saizi ni chache sana zenye vitu vya scania saizi kaamua kuwa serious upande wa engine,gearbox,front axle na diff
 
Gari zake nzuri sana
Ndiye chaguo langu kwa sasa.

Mwendo hapishani sana na Achimwene,anapaa ila siyo kama New force .
Gari inayokimbia kupita kiasi kama new force hapana kwa kweli
New force ndio gari pekee sijawahi kupanda.
Hao new force mnaosema wanakimbia,wanakimbia kwenye barabara zipi akati kila sehemu kuna askari?me nayapanda sana na sijaona hizo speed mnazozisema
 
Huyu mwamba wa ABC route ya Mbeya kaipania juzi kati kashusha vyuma 6, na tayari kashajenga terminal yake pale Mbeya.

Ila ajue abiria wa Mbeya wanachotaka ni mbio mbio sio mwendo kama route za Kaskazini
Huko mbeya bad mna ushamba sana,karne hii mbio zinakupeleka wapi?
 
Hao new force mnaosema wanakimbia,wanakimbia kwenye barabara zipi akati kila sehemu kuna askari?me nayapanda sana na sijaona hizo speed mnazozisema
Panda route ya Dar Kyela, Tunduma, Mbeya hii route ndo wanakimbia sana. Maana hapo kuna ligi flani hivi ya mbio.
 
Shida ya New force ni usafi,magari machafu ndani hatarii.ABC ni gari pendwa kwa sasa kwangu
 
New Force alikuwa na mabasi Dar-Kahama miaka ya nyuma zilikaa kidogo akaziondoa na ishu iliyomwangusha ni ma-agent

Hii biashara ina utawala wa kikanda ujue ikitegemea agents uliowapata

Ni sawa na kuuliza mbona Ally's Star ana mabasi mengi kanda ya ziwa lakini hana route za Mbeya, Iringa, au Songea

Hii biashara ina vipengele vyake usione kwanini Abood amekomaa na Moro au Shabiby na Dodoma agents wanahusika sana
Siku hizi watu wanakata ticket online, mambo ya agent hayana nguvu kwemye kampuni kubwa
 
Mwamba huyu hapa pamoja na kusua sua DRH ashashusha saa hizi saa kumi na nusu jioni na anaingia sheli hapa mbeya leo tarehe 19.2.2024
IMG_20240219_162748_102.jpg
 
Jamaa anashindwa kuongeza bus mpya?
Atatuangusha wanazi wa Sauli
Nilikuwa kijiweni leo nasikia jamaa anajipanga kuzileta wanasema hizi ni za ndaaaaaani kabisaa muda si mrefu anashusha vyuma. Ngoja tuone kama ni kweli
 
Back
Top Bottom