Kampuni ya basi Sauli zinaadimika barabarani shida nini?

Kampuni ya basi Sauli zinaadimika barabarani shida nini?

Hali ya Mgonjwa Kwa Sasa ilivo ni kuzidisha Maombi tu
FB_IMG_1707117285477.jpg
 
Kulikuwa na mwamba wa kuitwa Masia, Sumry wote hao walirusha vitaulo kama akina Color Star na JM
Summry nasikia amejikita kwenye kilimo sumbawanga.
Miaka ya 2000 ndio walikuwa wanachuana na akina Abood na Hekima.

Summry alileta bus lake kule milimani kwetu Songwe Undali..
Lilipiga route wiki haikuisha,dereva akalilaza chini.
Hakurudisha gari tena hadi leo.
 
Hii biashara sio poa niliwahi kuwa na mazungumzo na bosi wa zilizokuwa basi za Hekima zilitamba sana miaka ya 2000 mwanzoni route ya Dar-Mbeya-Tunduma.

Akaniambia msione vyuma tu vinapita barabarani ila mjue wakurugenzi wa mabasi wote tuna sonona

Mara ya mwisho niliona kawekeza zaidi kwenye usafirishaji wa malori, mabasi alipiga chini
Sisi abiria tunashangilia tu ligi😂
 
sauli AKA tege boy sasa ivii amefulia fine zimekuwa nyingi na ajali
Nadhani fine...!!! Maana niliwahi kumpanda Toka Morogoro... kumbe alikuwa nafuatiliwa Toka Dar es Salaam...mpaka tunafika Chimala Kasimamishwa na kuambiwa amefanya makosa 63 ya barabarani Toka ameanza safari....!!! You can imagine...!!! Wafuatiliaji walikuwa tayari " tuondoke" kwa kosa lolote la barabarani lakini watimize azma yao.
 
Huyu mwamba wa ABC route ya Mbeya kaipania juzi kati kashusha vyuma 6, na tayari kashajenga terminal yake pale Mbeya.

Ila ajue abiria wa Mbeya wanachotaka ni mbio mbio sio mwendo kama route za Kaskazini
Gari zake nzuri sana
Ndiye chaguo langu kwa sasa.

Mwendo hapishani sana na Achimwene,anapaa ila siyo kama New force .
Gari inayokimbia kupita kiasi kama new force hapana kwa kweli
New force ndio gari pekee sijawahi kupanda.
 
Back
Top Bottom