Kampuni ya basi Sauli zinaadimika barabarani shida nini?

Kampuni ya basi Sauli zinaadimika barabarani shida nini?

Scania moja unapata Mchina mbili moja nyongeza ya mkopo,
Wakati wakat scania anajaza siti 60 mchina anajaza mara tatu ya siti hizo yaaani 180 kwa nauli sawa.
Zikipishana mbili zinaendana moja inarudi.
Ndani ya mwaka Hela ya Mchina imerudi Scania utasubiria miaka sita au Tisa ndipo pesa irudi.
Biashara ya malori chukua scania ya mabus chukua mchina
Duuh! Punguza chumvi kidogo
Yaani scania inachukua miaka 6-9 kurudisha pesa?
Basi Akina superfeo,katarama Nacharo Na zuberi wasingenunua izo scania
Mchina anachomzidi scania Ni kwenye interior design basi.
 
Hivyo ndivyo inatakiwa iwe. Serikali nyingi zinaanzisha investment banks kwa ajili ya kuwa support watu kama Saul. Hao wachina ukifuatilia kuna support nyuma yake.
Kampuni/ biashara nyingi nyuma huwa kuna serikali nyuma yake
Biashara zinazoeleweka siyo? Tatizo letu ni kuwa biashara kama hii inaendeshwa kimagumashi na hata rekodi za kihasibu hazieleweki. Na nyingi huwa ni zile zenye kufikia masoko ya kimataifa. Kwa Tanzania wanatakiwa wawalinde wafanya biashara wa ndani.
 
Umewahi kupanda NEW FORCE juzi kati mpaka wameandikiwa na trafiki abiria walijaa mpaka wengine wamekaa chini pale katikati ya seat za kushoto na kulia
Na wewe bhana tofautisha kujaza Gari kabla ya Safari Na kuokota Abiria wa njiani ili kujaza Gari
Sauli anajaza gari kabla ya Safari Ata New force zike za alfajiri uwa zinajaza.
 
Dar lux nae kaingia mitini.
Hii biashara inataka uwe na akili kama ya kuku kama alivyo zuberi, new force.
Abiria wanaangalia luxuries and comfortability yaani Ndege ya chini unatoka safari hakuna hata vumbi Sasa kwa Scania anaemfikia viwango vya mchina si chini ya bilioni moja Macopolo G7 ambayo bongo hailipi.
Mkuu unasemaje kuhusu Katarama naye anasumbua route ya Mwanza kwa sasa na Scania zake.
 
Utarudishaje pesa haraka kwa chombo isiyodumu?
Gari Zina warrant ya mwaka mmoja.
Life span ni miaka 3 in good condition zinaenda hadi miaka 7 hadi 10.
Faida zinarudi mapema kwa wingi wa mabus uliyonunua.
Mfano Scania moja unapata Mchina mbili moja ya mkopo so jumla siti 180 kwa siku.
Nauli ya elf 50 kwa mfano.
So scania anatoa gari moja anapata milion 3, mchina anatoa gari tatu kauza siti 180 kaingiza milion 9 kwa mwezi scania milion 90 Mchina milioni 270 toa gharama za uendeshaji ndani ya miezi 6 pesa imerudi kwa Mchina unakamata zingine sita.
Scania kurejesha milion 700 itahitaji miezi mingapi.
 
Hakuna tajiri anaweza shindana na new force kwa vyuma bongo.
New force ni kampuni ya promotion na mauzo ya viwanda vya mabus vya China zile zinatembea huku zipo sokoni ukifika Bei unauziwa thus anawapa sana headache matajiri wa mabus bongo, huwezi ukashindana na viwanda vinavyofyatua matoleo mapya.
Na abiria wanafata kitu kipya kitu kizuri.
Hao new force zamani madereva wao walikuwa wachina walikuwa hawapati ajali ,sema sheria za nchi tu ndo zinawabana madereva lazima, wawe wabongo.
Walitamani madereva wao professional toka China ndio wazipelekee moto, sheria inawabana
Mwaka 2011 na 2012 nilikuwa napita kwa mguu kila siku pale shekilango nilikuwa naona hizo basi zinafanyiwa service na wachina tupu.
 
Na wewe bhana tofautisha kujaza Gari kabla ya Safari Na kuokota Abiria wa njiani ili kujaza Gari
Sauli anajaza gari kabla ya Safari Ata New force zike za alfajiri uwa zinajaza.
Gari ilijaza tangu ilipotoka ilipoanzia

Mtu ana mabasi 20

10 zinashuka 10 zinapanda zote zimejaa abiria na bado kuna hao wa njiani sio poa
 
Umeonaee

Ok tuseme gari linadumu lakini mwonekano wake unakuwa wa kizamani kadiri miaka ianenda

Mshindani wako analeta Mchina mpya wa kisasa lazima abiria wakukimbie wakapande basi la kisasa
Ivi Scania Marco Polo G7 Ina mwonekano wa kizamani?
IMG-20230915-WA0007.jpg
 
Mchina anaweza piga miaka 3 nenda rudi mbeya? Sidhani, New force anapumzisha gari zake kwa sababu uwezo anao na siyo ubora wa gari zake.
Sauli angelikuwa na mchina angelipaki baada ya mwaka. Mchina hawezi pigishwa mwaka mzima DAR - Mbeya-DAR akabaki kwenye game
Hivi hizi Machungwa Dar-Mwanza si mchina hizi!
 
Kwanini unasema ni kichaa? Inaweza kuwa pengine hata hujawahi kuifanya. Mimi nadhani tatizo ni watanzania wengi kuingia kwenye biashara bila kufanya research ya kina bali kwa kufuata mkumbo. Na siyo mabasi tu. Ukiangalia biashara kama maduka, bars, hotels nk zinazofunguliwa na kufa ni nyingi pia. Biashara ya mabasi ikifa inakuwa noticeable kwa haraka na kwa watu wengi kwa sababu gari linatembea barabarani na linaonekana na wengi tofauti na duka ambalo sanasana watu wa mitaa ya karibu ndiyo wanaweza kujua.


Ni mara ngapi unasikia household names kwenye biashara fulani zinakufa? Ni hotels ngapi au maduka mangapi makubwa on the par na kampuni kama Scandinavia, Hood au Sumry zimekufa?

Kwamba Scandinavia na hood hawakufanya research vizuri? Hadi leo hakuna basi linafikia Scandinavia kwa ubora wa huduma, hawa ndo walikua game changer. Kipindi kile ilikua bora upande hili basi kuliko ndege if you had that choice. Mtu unawaza likizo ifike upande Scandinavia uende mikoani na lilikua linapendeza kweli kweli na mwendo mzuri ila lilikufa kifo cha mende.

Dar express nasikia inapumulia machine, Mbunge Msukuma aliuza basi zake karibu zote. The list is endless mkuu, the writing is on the wall, hii ni biashara kichaa.
 
Gari Zina warrant ya mwaka mmoja.
Life span ni miaka 3 in good condition zinaenda hadi miaka 7 hadi 10.
Faida zinarudi mapema kwa wingi wa mabus uliyonunua.
Mfano Scania moja unapata Mchina mbili moja ya mkopo so jumla siti 180 kwa siku.
Nauli ya elf 50 kwa mfano.
So scania anatoa gari moja anapata milion 3, mchina anatoa gari tatu kauza siti 180 kaingiza milion 9 kwa mwezi scania milion 90 Mchina milioni 270 toa gharama za uendeshaji ndani ya miezi 6 pesa imerudi kwa Mchina unakamata zingine sita.
Scania kurejesha milion 700 itahitaji miezi mingapi.
Mkuu ungeweka na running cost ya hizo gari kwa mwaka ingelikuwa ni bora sana. Unaweza kuta scania anatumia kiasi kidogo sana kwenye matengenezo kwa mwaka kuliko mchina. Ila mchina kuwa road for 7 years haiwezekani labda awe branded na scania kwa baadhi ya vipuri
 
Back
Top Bottom