Kampuni inayomiliki Tigo yabadili jina, sasa ni Honora Tanzania

Mwekezaji mpya hupewa likizo ya Kodi Kwa miaka mitano.Hivyo Kila ukibadilisha jina unapata tax exemption ya miaka hiyo mitano.
Lakini Kwa hapo nilivyosoma taarifa yao naona si mwekezaji mpya ni Jina Tu limebadilika ,tin inabaki ileile,faili Lao brela inabaki hilohilo sababu kubadili Jina hakubadili incorporation no ,sasa Kwa hapo tax exemption inakuaje
NB :Nimefanya kazi ya kubadili majina ya makampuni Kwa miaka isiyopungua 10
 
In a positive side of this ni kuwa Mauritius waliamua kupunguza viwango vya kodi ambapo makampuni makubwa yanakimbilia kuweka makao makuu ya bishara zao huko kwa security hii na kutozinguliwa na mauzauza kama ya TRA yetu.

Mimi nikipata nafasi ya kumshauri Rais nitamueleza manufaa ya kushusha viwango vya kodi ili siyo tu ilipike bali kushawishi wawekezaji wakubwa na kuongeza ajira.

BOT pia ni kikwazo kwa sekta ya fedha nchini. Inatumika sana na watawala kudhibiti watu wanaosakamwa na serikali
Cayman, Mauritius, New Jersey Islands, Dubai wanafaidi kampuni nyingi sababu ya kodi ndogo na usiri
 
Ni kwamba wawekezaji hupewa miaka 5 ya operation bila kulipa kodi then baada ya huo mda ndonhuanza kulipa kodi. Jamaa wanafanya 3 ama 4 years wanauza kwa madai wamepata hasara. Atakayekuja anaaza tena miaka 5 bure kudadeki
Inakuwaje hasara wakati kila kitu chao kiko monitored na TCRA?
MIC Tz ipo muda mrefu sana zaidi ya miaka 20
Hapo wamebadilisha jina la biashara ila shareholders ni wale wale
 
Unaweza kuwa na PhD ikawa sio ya hiyo fani na usijue Mkuu au nakosea ukiwa na PhD ya vitunguu lazima ujue mambo ya upasuaji kwa kuwa una PhD tuu..
Kuna wapumbavu humu wala hawastahili hata kujibibiwa.

TRA wana Chuo kabisa cha Taxation, Nina rafiki yangu ni Advocate huwa nikimpelekea kazi kwa sababu tunaheshimiana huwa ananitafutia Wakili aliyejikita kwenye angle hiyo mawakili wanajuwana vizuri sana nani bora kwenye case zipi, kwa sababu yeye anadeal na corporate, huwezi kumpelekea criminal case akaingia tamaa, haendi mahakamani kusimamia criminal case hata siku moja.

Kuna mawakili wa mirathi na ndoa wamejikita hapo, kuna mshuwa wangu alikuwa ni Mwalimu wa Chuo cha Ardhi wakati huo wao ndio waanzilishi wa savey na sasa ni advocate, huyo ukipambana naye kesi ya Ardhi lazima akukalishe.

Tundu Lisu licha ya kuwa ni Wakili bora lakini inasemekama angle yake ni upande wa mazingira.

Sasa JF imevamiwa na vichaa inabidi tuwavumilie.

Yani sasa kila msomi analazimika kujuwa mambo ya Taxation, hizi sijui ni akili za wapi?
 
Watu wanakwepa kodi kizembe sana. Alaf badala bunge lishughulike na kurekebisha sheria mbovu za namna hii wako busy wanataka kuuza bandari. Tuna bunge la kipumbavu sana
 
HOME SHOPPING CENTRE walishamili sana enzi za VASCO DAGAMA; alipoingia JIWE kama Rais kumbadili Kikwete nao wakabadilika na kuitwa jina jipya la GSM!!!!
Home shopping center siyo GSM ingawaje wamiliki ni wale wale.

Home shopping center ilifungwa kisheria kwa kufuata taratibu zote za kisheria.

Wengi hawajaelewa swali langu la msingi hapo juu, Mimi ni mnufaika wa kampuni moja kubwa sana ambayo makao makuu yake hapo ulaya, tuliingia mgogoro mkubwa sana wa kikodi mpaka kufikia kufunga kampuni lakini taratibu zote za kulipa kodi ya serikali zilifuatwa na serikali ikalipwa kodi yake na kuifunga kampuni.

Zipo some cases kampuni inanunuliwa na kampuni nyingine, mfano ni SDV NOTCO imenunuliwa na Bollore ya Ufaransa na sasa inaitwa Bollore hapa unakwepaje kodi?

DAHACO imenunuliwa na Swiss port na sasa inaitwa Swissport hapa unakwepaje kodi?

Ndio sababu nikaomba kuelimishwa, kwa sababu hii ni issue tofauti kabisa na hiyo Tax holiday otherwise Wahindi wangekuwa wanabadilisha majina tu kama ni kitu rahisi hivyo.
 
Back
Top Bottom