Fahamu Tofauti kati ya Jina la Biashara na Kampuni

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,525
5,579
Habari za wakati huu;

Ni matumaini yangu kwamba mko salama na mnaendelea na shughuli mbalimbali za Ujenzi wa Taifa.Wakati ninapofanya kazi na watu ya kusimamia mchakato waowa usajili wa Kampuni na majina ya biashara huwa ninakutana na maswali mbalimbali kuhusu tofauti iliyoko kati ya Jina la Biashara na Kampuni.

Usimamizi Kisheria
Kwa Tanzania kuna sheria mbili zinazohusiana na Usajili w Kampuni na Majina ya Biashara.Sheria hizi ni Sheria ya USajili wa Majina ya Biashara(Business Names Registration Act Cap 213) na Sheria ya Makampuni(Companies Act 2002)

Sheria hizi ndizo sheria ambazo zinaongoza Usimamizi wa Majina ya Biashara na Kampuni kwa Tanzania na Hiyo ni Tofauti ya kwanza.

Hivyo basi matumizi yote ya Jina la Kampuni lazima yazingatie sheria husika na Matumizi yote ya Kampuni lazima yazingatie Sheria ya Makampuni.

Ukomo wa Umiliki/Dhamana

Kampuni huwa na Ukomo wa Hisa(Hisa ni kiwango cha Umiliki wa Mtaji/Dhamani ya Kampuni).Hii inamaanisha kwamba Unapoanzisha Kampuni wewe kama Mwanahisa unakuwa umeweka kama Dhamani Kile kiasi cha hisa ambacho umenunua na kulipia(Issued and Paid Up).Kwa hiyo ikitokea Kampuni imefilisika Utapoteza Hisa zako tu na mali zako binafsi ambazo ziko kwa Majina yako Binafsi hazitaathiriwa kabisa.Hivyo kampuni inalenda Wamiliki dhidi ya Hasara za kibiashara.Huu Ndio Msingi wa Limited Liability(UKOMO wa Madeni).

Kwa Upande wa Jina la Biashara Halina Ukomo huo.Hivyo Basi Biashara yako inaposhindwa kulipa Madeni yako ina maana kwamba wanaweza kuja kukamata mbuzi na kukuwako kwa ajili ya kufidia Madeni yote unayodaiwa.

KODI

Kampuni huwa inajitegemea katika Masual ya Kodi kwa maana ya kwamba inakuwa na TIN number yake pamoja na kujisimamia yenyewe katika masuala yote ya kodi.Unapotumia Jina la Biashara Utaendelea kutumia TIN yako binafsi katika masuala yote ya Ulipaji na Usimamizi wa Masuala ya kodi

Pamoja na tofauti hizo chache Bado unaweza kubadili JINA la Biashara yako liwe Kampuni na Unaweza Pia kuamua kusajili Jina la Biashara linalomilikwa na Kampuni.

Kwa Ujumla Gharama za Kumiliki na kuendesha kampuni ni kubwa kuliko Kampuni ila Faida za Kumiliki Kampuni ni Kubwa kuliko za Kumiliki Jina la Biashara.


Iwap unahitaji kusajili JINA la Biashara,Kampuni,NGO,Foundation etc Tafadhali wasiliana nasi kwa Email:masokotz@yahoo.com

Tunakutakia Kila la heri katika Majukumu Yako
 
Back
Top Bottom