Kampuni inaweza kuanzisha ligi ya mpira wa miguu tofauti na hii iliyo chini ya TFF?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Habari wakuu,

Hapa namaanisha kampuni inataka kuwekeza kwenye mpira wa miguu. Inatafita viwanja vyake, kwa kukodi au kwa kujenga. Kisha inatafuta timu na kuanzisha ligi yake.

Mapato ya mlangoni na haki za matangazo inachukua. Yaani kampuni inaendesha kila kitu, inakuwa haiko chini ya TF wala vyama vya mipira vilivyo chini ya TFF. Inawezekana au TFF wana hakimiliki ya masuala ya mpira TZ?
 
Hivi Azam Federation haitambuliki FIFA?
Azam Federation imeitwa Azam kwasababu ya udhamini wake ila ki uhalisia iko chini ya TFF

So Azam Federation inatambulika na CAF mpaka FIFA kwa maana mshindi wake anaenda kushiriki mashindano ya CAF.

I hope nmekusaidia kuelewa.

Peace & Out!!
 
Mfano wa hivi karibuni ni sakata la ESL (Europian Super League) si umeona ilivyoshindikana? Na pesa iliyokua inatoka pale ni nyingi ya CL cha mtoto.

Yaani labda hiyo kampuni iamue kudhamini michuano ambayo ipo tayari mfano FA halafu ifanye iitwe kwa jina lao.

Nje ya hapo hilo litakua bonanza.
 
Mfano wa hivi karibuni ni sakata la ESL (Europian Super League) si umeona ilivyoshindikana? Na pesa iliyokua inatoka pale ni nyingi ya CL cha mtoto.

Yaani labda hiyo kampuni iamue kudhamini michuano ambayo ipo tayari mfano FA halafu ifanye iitwe kwa jina lao.

Nje ya hapo hilo litakua bonanza.
Kwahyo we unahisi super League ingefanikiwa kuanza ingekuwa bonanza?
 
Kwahyo we unahisi super League ingefanikiwa kuanza ingekuwa bonanza?
Nahisi utakua haujafuatilia ishu nzima.

Michuano ilitaka timu zinazoshiriki ligi kuu nchini mwao ndiyo zishiriki ESL.

Fifa ikaona ESL itaua mvuto wa CL na kutokana na wingi wa pesa timu zingefocus na ESL kuliko CL.

Hivyo likawekwa zuio kwa kila atakayeshiriki hatocheza WC. Perez akasema watatengeneza WC yao.

Pia wakasema timu shiriki za ESL zitashushwa daraja mpaka la 5.

Hayo yote yangetokea ESL ingekua nini?
 
Sio lazima...

Umiseta ..
Umishumta..zote haziko chini ya Tff..

Binafsi nawaza kuanzisha ligi ya Vyuo..

Mfano Fainali udsm na Udom..
Hii Tff haitahusika..
Wanahusika BMT Tu..
Hata TFf iko chini ya BMT
Timu ikishiriki ligi ya Tz ikiwa ya kwanza au ya pili inaenda shiriki michuano ya CAF.

Timu ya daraja la kwanza ikishinda inakua promoted ligi kuu.

Hii ligi ya vyuo bingwa anapata nini? Si inakua haina tofauti na ligi za ng'ombe zilizosambaa mitaani?
 
Back
Top Bottom