Uchaguzi 2020 Kampeni za Uchaguzi mkuu - 2020 mitandaoni ni mtifuano wa kufa mtu kati ya TEAM Tundu Lissu (CHADEMA) vs TEAM John Magufuli (CCM)

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
This is very interesting, kwa kweli...

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC), kampeni rasmi za kila mgombea za nchi kavu, angani au majini za kutembea kijiji kwa kijiji, kata kwa kata, jimbo kwa jimbo Tanzania nzima zitaanza trh 26/8/2020....

Lakini kampeni zisizo rasmi za MTU kwa MTU au NYUMBA kwa NYUMBA na hasahasa za kupitia mitandao ya kijamii (social media) zenyewe hazihitaji ruhusa ya mtu ama chombo chochote cha kisheria. Hizi zilishaanza muda mrefu tangu ama pengine labda kabla hata ya mwezi May, 2020...

Nimefanya utafiti wangu fast fast kwa kupitia baadhi mitandao ya kijamii maarufu zaidi kama JF, Instagram, Twitter, Facebook, Telegram, YouTube nk, mjadala unao - trend kwa sana ni uchaguzi mkuu Tanzania - 2020....

Mijadala hii inawahusisha wagombea wawili; Tundu Lissu (CHADEMA) na Magufuli Pombe ( CCM)....

Kwa uwazi kabisa, mtu aweza kusema kuwa ni timu mbili zinazotifuana na kupambana vilivyo....

Upande huu ipo TEAM TUNDU LISSU - CHADEMA + vyama shindani vilivyo nje ya serikali...

Upande wa pili ipo TEAM POMBE MAGUFULI + serikali nzima + NEC + baadhi ya TISS waasi wa ethics za utumishi wao + baadhi ya maafisa wa polisi waasi wa ethics za Utumishi wao + mahakama ikihusisha baadhi ya Mahakimu/majaji waasi wa ethics zao za utumishi + Msajili wa vyama vya siasa + vyama washirika vilivyo nje ya serikali kama UDP ya Cheyo, TLP ya Mrema, NCCR - Mageuzi ya Mbatia na vingine...

JWTZ sitawaingiza hapa kwa sababu, ktk uchaguzi wa mwaka huu 2020, hawa wameshatoa clear statement kuwa, JESHI HALINA CHAMA CHA SIASA. Kwa hiyo tunawapa "benefit of doubt" ya kuwa wanamaanisha walichokisema....

Mijadala ni mikali sana ktk kila mtandao. Upepo unaonekana kuivumia vibaya TEAM POMBE MAGUFULI - CCM. Wanaonekana kuzidiwa kwa hoja ktk kila idara na mpinzani wao TEAM TUNDU LISSU - CHADEMA....

Sasa waneona, the best option kwao ni kuanza kurusha matusi ya nguoni wakijifaragua na kudhani hiyo ndiyo njia ya ku - neutralize hoja za washindani wao. Huu ni utoto wa shule....!

Imefikia mahali wanatishia kuua mtu kwa RISASI za SMG ama AK47. Na pia wanatisha vyombo vya habari Redio na TV kutorusha lolote kuhusu Tundu Lissu. Magazeti yote neutral yalishauwawa na kuzikwa. Kwa kweli hali ya mgombea wao na CCM kwa ujumla haileti matumaini SI NZURI, ni MAHUTUTI inaweza "kufa" wakati wowote....!

Mtifuano wa timu hizi mbili wiki mbili zilizopita ulikuwa unaonesha kuwa PRAISE TEAM MAGUFULI - CCM ingeweza ushinda kwa goli la mkono huku TEAM TUNDU LISSU - CHADEMA, wachezaji wake wakiwa wanyonge na wasio na ari ya mchezo kabisa kutokana na mashambulizi ya wapinzani wao....

Wapinzani wa TEAM TUNDU LISSU - CHADEMA yaani TEAM MAGUFULI - CCM ktk namna fulani ya ajabu, ilianza kupata "back up" kutoka TEAM MEMBE - ACT WAZALENDO....

Lakini baada ya ujio wa Tundu Lissu, hiyo "back up" haina kazi tena. Iko kila dalili kuwa, TIMU MEMBE itaungana na TIMU LISSU dhidi ya TIMU POMBE - CCM....

Mashambulizi ya TEAM PRAISE MAGUFULI - CCM yalilenga zaidi kukata stimu na ari ya TEAM TUNDU LISSU. Hoja zao zilikuwa hizi. Kwamba, TUNDU LISSU;

å Hawezi kurudi huyo toka Ubelgiji...

å Ni mkimbizi wa kisiasa huyo, harudi TZ ...

å Kanunuliwa na "mabeberu" huyo, harudi....

å Akija lazima tumuue huyo, na safari hii hatukosei target...

å Akija huyo, pingu zinamsubiri hapohapo uwanja wa ndege....

Eti hoja yao ikiwa ni "kwa kuichafua serikali na Rais wao" akiwa nje ya nchi....

Looh, hawa jamaa mazuzu kweli kweli. Na hawa eti ndiyo "think tank" ya "JIWE" naarufu kama LB7 FC..!!

å Akija, hana sifa ya "kimaadili" ya kugombea Ubunge ama Urais....!!

HOJA hizi ziliinyong'onyeza kuvunja ari ya mpambano kabisa TEAM TUNDU LISSU - CHADEMA....

Tangazo la kurudi nyumbani tarehe 27/7/2020 la Tundu Lissu, lilianza kuamusha ari ya vita ya TEAM TUNDU LISSU - CHADEMA....

Matumaini ya TEAM TUNDU LISSU - CHADEMA yaliyokuwa ya mashaka, yaligeuka kuwa ya KWELI, HALISI na HAKIKA tarehe 27/7/2020 saa 7.30mchana pale Tundu Lissu alipoikanyaga ardhi ya Tanzania baada ya miaka mitatu kuwa nje kwa matibabu...

Hii iligeuza kabisa sura ya mpambano. Unyonge, kunyong'onyea na kukata tamaa na kukosa ari ukawa upande wa TEAM POMBE MAGUFULI - CCM. Wakawa "paralyzed" ghafla wasijue nini cha kufanya. Ndipo walipogundua kuwa assumptions zao zote zile hapo juu kwa wafuasi wao ilikuwa ni UONGO na KUWALISHA upepo tu....!

Mgeuko huu hasi na wa ghafla dhidi ya PRAISE TEAM MAGUFULI - CCM ukanikumbusha fainali ya mwaka 2004/2005 ya UEFA Champion League kati ya AC MILAN FC (Italy) vs LIVERPOOL FC (England)...

Hii ilikuwa moja ya historical UEFA Champion League finals kuwahi kushuhudiwa na wapenzi wa soka duniani...

Mpaka kipindi cha kwanza kinaisha, AC MILAN FC walikuwa mbele kwa goli 3 huku LIVERPOOL FC wakiwa hawana goli (0)...

Second period ilipoanza, wapenzi wa AC MILAN na wachezaji wao, hawakuamini kilichotokea uwanjani. Liverpool FC, walirudisha goli zote hadi dakika 45 za kipindi cha pili zinamalizika....

Dakika 30 zikaongezwa bila mshindi kupatikana. Wakaingia kwenye matuta (penalties). Liverpool FC wakiubuka kidedea kwa ushindi wa penalties 4 - 2 na kutawazwa mabingwa wa Ulaya msimu wa 2004/2005....!!

Huu mpambano wa TUNDU LISSU vs POMBE MAGUFULI naufananisha pia na fainali hii. Tundu Lissu - CHADEMA (Liverpool FC) na Pombe Magufuli - CCM (AC Milan FC)....

Mpaka mwezi Jana (July), Team Pombe Magufuli - CCM walikuwa mbele kwa goli 3 bila. Wiki mbili tu zimepita, Team Tundu Lissu - CHADEMA wamesharudisha goli zote. Tupo kwenye penalty shoot out na mpaka sasa LIVERPOOL FC TEAM TUNDU LISSU wanaongoza kwa goal penalty 3 dhidi ya 1 PRAISE TEAM MAGUFULI - CCM....

Mashabiki wa TEAM POMBE MAFUGULI CCM hawaamini kinachotokea. Vichwa vimeinama chini. Wenye roho ndogo wanarusha chupa za maji uwanjani. Wengine wanarusha matusi kwa wapinzani wao na wachezaji na kocha wao wakiwatuhumu kwa uzembe..

Kwa kifupi hali si shwari kabisa kwa TEAM POMBE - CCM. Ishara na dalili zote zinaonesha kuwa wanapoteza pambano hili ambalo walilitawala sana kipindi cha kwanza....!!

Heko TEAM TUNDU A.M LISSU - CHADEMA....
 
Mkuu,,! Tangu technology hii ya simu za smart iingie nchini utaona tangu 2015 chadema ni washindi wa mitandaoni!

Ccm si watu wa makelele, kuna vigogo wako huko ccm wanajua nini cha kufanya ili kupata ushindi! Wanajua ushindi hauko kwenye kelele za mitandaoni kama chadema wafanyavyo!

Kingine, mashabiki wa Lisu hawana tofauti na wale wa Bob Wine yule wa uganda!
Ni mashabiki mihemuko, hutawaona kwenye foreni ya kupiga kura! Mfano kuna mmoja humu ni mshabiki wa Lisu na anajipinda kweli kushambulia hapa jf, lakini juzi nlishangaa anaulizia kitambulisho cha kupigia kura atakipataje .
Hao ndio mashabiki wa chadema.

Kwangu mimi 2015 ilinipa somo kubwa sana na inafanya nisiwe na wasiwasi juu ya ushindi wa ccm hapo oktoba.
 
Mkuu, you have nailed it! Kama kungekuwa na uwezo wa kutoa "like" zaidi ya moja, ungezipata nyingi kutoka kwangu. Kongole nyingi zikufikie.

Hata kule upande wa Zanzibar, kwa mapokezi ya leo ya ACT Wazalendo, CCM mwaka huu wanalo. Kama kwa kupitia mbinu za medani za kivita, wameshakuwa "manoeuvred" ktk uwanja wa mapambano. Ni Hayati Benjamin William Mkapa pekee ndiye jemedari ambaye angaliweza kuikoa CCM ktk hii hali ya jahazi kutaka kuzama.
 
Mkuu,,! Tangu technology hii ya simu za smart iingie nchini utaona tangu 2015 chadema ni washindi wa mitandaoni!

Ccm si watu wa makelele, kuna vigogo wako huko ccm wanajua nini cha kufanya ili kupata ushindi! Wanajua ushindi hauko kwenye kelele za mitandaoni kama chadema wafanyavyo!

Kingine, mashabiki wa Lisu hawana tofauti na wale wa Bob Wine yule wa uganda!
Ni mashabiki mihemuko, hutawaona kwenye foreni ya kupiga kura! Mfano kuna mmoja humu ni mshabiki wa Lisu na anajipinda kweli kushambulia hapa jf, lakini juzi nlishangaa anaulizia kitambulisho cha kupigia kura atakipataje .
Hao ndio mashabiki wa chadema.

Kwangu mimi 2015 ilinipa somo kubwa sana na inafanya nisiwe na wasiwasi juu ya ushindi wa ccm hapo oktoba.
Sema CCM wengi ni mafukara hata mlo wa siku unawashinda wataziweza smartphone?

Wewe ushukuru tu hilo bando la Lumumba vinginevyo tusingekusoma humu!
 
Sasa sijui ni kwa vigezo gani Chadema wanadai wameshinda Mitandaoni labda kwa kutukana Sana , hapo nakubali.

Jamaa wanajua kutukana bwana asikwambie mtu.
Sasa kama jamaa yenu pale dumila anawambia wakinamama panueni haya si matusi ya nguoni kabisa?
 
Sasa kama jamaa yenu pale dumila anawambia wakinamama panueni haya si matusi ya nguoni kabisa?
Nadhani huko Kuna vyeo vya matusi,

Maana mtu anatukana tokea Uchaguzi mmoja mpaka mwingine unakuja halafu kibaya sasa unakuta anaowatukana wanashinda chaguzi zote anazoshiriki kutukana.

Mfano huu, CCM itashinda majimbo mengi, kwa nafasi za Ubunge,

Kwa Urais hata tusipopiga kampeni kabisa.
 
Ni mitandaoni siyo huku field ambako kombe ndio linakopatikana!
Isitoshe Uchaguzi Mkuu ujao si kati ya Lissu na Magufuli bali Lissu dhidi ya wagombea wengine wa Urais.

Nguvu na muda mwingi unatumika kumpamba Lissu kupitia mgongoni mwa Magufuli na Lissu naye kakamatwa na ugonjwa huo. Mwisho wa siku Lissu na wapambe wake watashangazwa na matokeo. Kwa utabiri wangu Lissu atapitwa kura na wagombea wengine
 
Katika hali ya kawaida CCM itakuwa inajidanganya sana kudhania watanzania na ugumu wa maisha ya watu ulivyo hii awamu wanayo hamu hata kusikia hicho chama. Kila mtu amechoka mno tuvumiliane ifike tu October siyo mbali.

Kwa ugumu wa maisha sasa hivi hata angekuwa amejenga flyover mikoa yote na kukamilisha kabisa ujenzi wa SGR asingeweza kupata kura watu wameumizwa sana na ugumu wa maisha.

Jana kuna doctor mmoja alisema kuna mgonjwa aliletwa hospitalini mme akawa amebeba kuku kwamba atauza apate pesa ya matibabu alizunguka na kuku siku nzima bila kupata mnunuzi ikabidi amuombe doctor achukuwe huyo kuku na kumtibu mgonjwa wake. Maisha kama hayo ndo mwananchi atapigia kura CCM kweli tusuburi tuone.
 
Back
Top Bottom